Sweden yaonya matumizi fedha za umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sweden yaonya matumizi fedha za umma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  BALOZI wa Sweden, Staffan Herrström amekomelea msaumari mwingine katika kuitaka serikali kuwa makini na fedha za walipa kodi aliposhauri kuwepo na umakini katika matumizi ya fedha za umma.

  Wito wa balozi huyo umetolewa siku chache baada ya nchi na taasisi hisani kwenye bajeti kuu ya serikali kutangaza kupunguza msaada wao katika bajeti ijayo ya mwaka 2010/11 kutokana na kutoridhishwa na masuala kadhaa ya kiutendaji, ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa kodi na matumizi makubwa ya fedgha za umma.

  Jana balozi huyo, akizungumza na waandishi wa habari nje ya semina ya wadau wa habari iliyokuwa na lengo la kubadilishana uzoefu juu ya umuhimu wa uwazi, uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari, alisisitizia tena umuhimu wa kutumia vizuri fedha za walipa kodi.

  Balozi Herrström alisema uwajibikaji na utawala wa sheria unaimarika kwa kulinganisha na miaka ya nyuma, lakini akatoa angalizo kuwa matumizi ya fedha za umma ni yakuzingatia.
  “Kwa upande wa mpango wa muda mrefu ndiyo, lakini suala la matumizi ya fedha za umma linatakiwa liangaliwe kwa umakini,” alisema balozi huyo.

  Balozi Herrström alisema kwa kiwango kikubwa, uwazi ni njia bora zaidi ya kuweza kupambana na rushwa nchini.
  Herrström aliitaka Tanzania kulipa kipa umbele suala la uwazi na kulitekelza kwa umakini mkubwa.
  Alisema pia vyombo vya habari vikiwa huru na kupata taarifa muhumu kwa ajili ya kuupasha umma, kwa kiasi kikubwa hali hiyo itasaidia mapambano dhidi ya rushwa.

  Balozi huyo alisifu kuwa uhuru wa vyombo vya habari nchini unakuwa siku hadi siku, lakini akasema kufungiwa kwa baadhi ya magazeti na serikali kulitia doa juhudi hizo za serikali.
  Hata hivyo, balozi huyo hakutaka kueleza hatua ambayo nchi yake na wafadhili wengine wanaweza kuchukua iwapo serikali haitatekeleza masuala hayo ya utawala bora na uwazi.

  “Serikali inatakiwa ifanye kitu ambacho wananchi wake wanataka," alisema. "Wanaweza kusema sisi tunataka rushwa; hatutaki uwazi; hatutaki uhuru wa vyombo vya habari na kama ndivyo na sisi fedha zetu hatutazitoa,” alisema balozi huyo.

  Herrström pia alisema kuwa, uhuru wa vyombo vya habari unatakiwa uendane na uhuru kwenye vyumba vya habari.
  “Inatakiwa chombo cha habari kifanye kazi yake kwa kuzingatia maadili na taaluma, siyo kuandika habari kwa matakwa ya mmiliki wala mtu yeyote; siyo kutumiwa na watu wenye fedha kwa masilai yao,” alisema Balozi Herrström.

  Sweden yaonya matumizi fedha za umma
   
 2. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  asante,nadhani wameanza kuona matatizo ya nchi hii sasa.na tutafika tu,tuendelee kulalamika:angry:
   
Loading...