Sweden yamwaga billion 436 kama msaada wa kibajeti kwenye Serikali ya Tanzania

Nilikuta matundu mawili ya vyoo katika ofisi ya mtendaji wa kata nje kuna bango kubwa limeandikwa kwa msaada wa watu wa marekani. Nilijiuliza ndo misaada tunayoambiwaga kwa mbwembwe au hii ni design nyingine. Nilienda mbele zaidi nchi iliyojaa raslimali mpaka raslimali watu ya wataalamu inashindwa kujenga matundu mawili ya vyoo mpaka msaada kutoka kwa watu wa marekani?
Nasubiri move ifike katikat maana produz wet tunamwelew
 
Itapendeza zaidi kama msaada huu utatumika kuleta maendeleo ya nchi na hasa kupunguza uhaba wa pesa katika awamu hii.
Sisi tunasubiri tuongezwe mishahara yetu. Kama kazi tunafanya kwa bidii zote hivyo tupewe stahili zetu haraka.
Pesa ya mishahara nayo tutegemee kutoka nje kweli? Hizi pesa zikahudumie miradi
 
Em nieleweshe Magufuli kanyoosha vipi mikono mipesa inajileta yenyewe unataka akatae?

Sio kwa tambo zile za kugomea hela za MCC. Unaweza ukatuambia kile kiburi cha kugomea heka la za MCC kilikuwa cha nini na leo kimeenda wapi kwa wazungu haohao?
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa kuna aliyewafuata hawa watu officeni kwao na kiwaomba watutenge, naomba nirekebishwe kama nimekosea sababu nadhani hawakueleweka
Yuko hospital bado amelazwa. Habari kama hii zinaweza kuliamsha dude ugonjwa ukaanza moja!
 
Mkuu nina hakika sikio hilohilo lilisikia mtu akisema nchi hii ni tajiri sana haihitaji misaada.
Mkuu, mtoto hata angekuwa na nguvu na uwezo kiasi gani hawezi kuanza kwa kukimbia, huanza na kusimama dede kwanza ili kuimarisha misuli, then hufuata kupiga hatua moja baada ya nyingine, baada ya hapo kutembea, na baadae kukimbia.
 
Bai mimi nikadhani sisi ndio tunasaini kuwasaidia sweden kama tulivyoaminishwa kwamba sisi ni matajiri.Na tutaanza kuwapelekea wazungu nguo za mitumba wakavae
 
SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Msaada, mkopo?
 
Nilikuta matundu mawili ya vyoo katika ofisi ya mtendaji wa kata nje kuna bango kubwa limeandikwa kwa msaada wa watu wa marekani. Nilijiuliza ndo misaada tunayoambiwaga kwa mbwembwe au hii ni design nyingine. Nilienda mbele zaidi nchi iliyojaa raslimali mpaka raslimali watu ya wataalamu inashindwa kujenga matundu mawili ya vyoo mpaka msaada kutoka kwa watu wa marekani?
We umejenga matundu mangapi mkuu?
 
Nchi nyingi tu zimetoa pesa awamu hii ila kwakuwa zinatumika kwa uamuzi wa bunge la mtu mmoja bado watanzania wasitegemee kuona pesa zikiingia mifukoni mwao kupitia biashara au shughuli zao za kimaendeleo.

Ila swali langu ni hili: Serikali imepewa msaada kama kampuni inayozalisha bidhaa gani?
Kama jibu ni kwamba serikali si kampuni sasa kwanini kiumbe hai mmoja alisema siongezi mishahara mpaka uzalishaji uongezeke?
 
SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Huenda ukajengea chato university
 
Nilikuta matundu mawili ya vyoo katika ofisi ya mtendaji wa kata nje kuna bango kubwa limeandikwa kwa msaada wa watu wa marekani. Nilijiuliza ndo misaada tunayoambiwaga kwa mbwembwe au hii ni design nyingine. Nilienda mbele zaidi nchi iliyojaa raslimali mpaka raslimali watu ya wataalamu inashindwa kujenga matundu mawili ya vyoo mpaka msaada kutoka kwa watu wa marekani?
Hayo mambo ya awamu ya nne. Kila mwezi watu walikuwa wanaenda kuomba misaada kule
 
Mkuu, mtoto hata angekuwa na nguvu na uwezo kiasi gani hawezi kuanza kwa kukimbia, huanza na kusimama dede kwanza ili kuimarisha misuli, then hufuata kupiga hatua moja baada ya nyingine, baada ya hapo kutembea, na baadae kukimbia.

Mtoto wa miaka 56 umewahi kumuona wapi? Au hujui unaloongea?
 
Sio kwa tambo zile za kugomea hela za MCC. Unaweza ukatuambia kile kiburi cha kugomea heka la za MCC kilikuwa cha nini na leo kimeenda wapi kwa wazungu haohao?
Nimeshakuambia hizo pesa za MCC hazijapunguza chochote sababu umoja wa ulaya wametoa pesa za bure vijiji vyote Tanzania vitawekwa umeme, sasa tuna shida gani? Nani anajua labda ni aibu MCC waliona sasa wameamua watuletee kwa mkono wa jirani.?
 
Hizijapunguza chochote kwani hazikuingia bali baadhi ya mipango iliyokuwa imetarajiwa kutekeleza na fedha hiyo ilikwama. Kama pesa ile ingeingia leo hivyo vijiji usingesema vitawekwa bali ungesema vimewekwa umeme tayari. Hilo kwamba ni aibu hizo ni hisia zako. Watuonee aibu kwa lipi?
 
Very very Good..!! Mh. Rais wetu hongera sana, juhudi zako zinajulikana, na ndio sababu wafadhili hutoa fedha za maendeleo nyingi bila wasiwasi.. Mungu mbariki JPM, Mungu ibariki Tz
Bajeti imetekelezwa chini ya 60% bado mijitu inasifu. Aliyewaroga
 
Back
Top Bottom