Uhusiano wa CC za gari na ulaji mafuta

Mogmazee

New Member
Mar 21, 2012
4
1
Wanajamii kuna ufanano gani kati ya CC za gari na ulaji wa mafuta?

===
Majibu

Kiasi cha mafuta kitumikacho huendana na kiasi cha CC.
  1. Gari yenye CC kubwa huchoma kiasi kikubwa cha mafuta ukilinganisha na gari yenye CC ndogo,kwa wakati mmoja, ndio sababu gari yenye CC kubwa huwa na nguvu zaidi ukilinganisha na gari yenye CC ndogo.

  2. Iwapo una umbali wa KM 500 na una gari mbili zenye CC kubwa na ndogo: Yenye CC kubwa itatumia kiasi kingi cha mafuta kuzimaliza KM 500, wakati yenye CC kidogo itatumia mafuta kidogo kumaliza hizo KM 500.

    Ndio sababu kwa mjini mweny vitz akiweka mafuta ya 20,000 atatumia hata siku 3 kwa mizunguk yake, Wakati yule mwenye gari ya CC mfano CC3000 yeye hatokwenda umbali mrefu kwa mafuta ya TSH 20,000

  3. Kadri ambavyo kiasi kingi cha mafuta kinavyochomwa kwenye cylinder kwa mara moja, ndio jinsi ambavyo utaenda KM chache kwa kila lita moja ya mafuta.

CC humaanisha ‘Cubic Centimetres’ ambayo huwakilisha sentimita za ujazo za kinu ‘cylinder’ cha kuchoma mafuta ili kuipa nguvu injini. Hivyo CC ikiwa kubwa ina maana kinu ni kikubwa na kutakuwa kinahitaji mafuta mengi zaidi ili mlipuko wake kusukuma ‘pistons’

CC Kubwa humaanisha kinu kikubwa na mlipuko mkubwa ambao huipa nguvu zaidi injini. Kwa hiyo gari yenye CC kubwa hula mafuta mengi pia huwa na nguvu

Gari yenye CC kubwa huchoma kiasi kikubwa cha mafuta ukilinganisha na gari yenye CC ndogo, kwa wakati mmoja, ndio sababu gari yenye CC kubwa huwa na nguvu zaidi ukilinganisha na gari yenye CC ndogo

Ndio sababu kwa mwenye Vitz akiweka mafuta ya Tsh 20,000 kwa mizunguko midogo midogo ya mjini atatumia hata siku 3 kwa mizunguko yake, Wakati yule mwenye gari ya CC3000 yeye hatokwenda umbali mrefu kwa mafuta ya TSH 20,000
 
Wanajamii kuna ufanano gani kati ya CC za gari na ulaji wa mafuta?
Kiasi cha mafuta kitumikacho huendana na kiasi cha CC.
  1. Gari yenye CC kubwa huchoma kiasi kikubwa cha mafuta ukilinganisha na gari yenye CC ndogo,kwa wakati mmoja, ndio sababu gari yenye CC kubwa huwa na nguvu zaidi ukilinganisha na gari yenye CC ndogo.

  2. Iwapo una umbali wa KM 500 na una gari mbili zenye CC kubwa na ndogo: Yenye CC kubwa itatumia kiasi kingi cha mafuta kuzimaliza KM 500, wakati yenye CC kidogo itatumia mafuta kidogo kumaliza hizo KM 500.

    Ndio sababu kwa mjini mweny vitz akiweka mafuta ya 20,000 atatumia hata siku 3 kwa mizunguk yake, Wakati yule mwenye gari ya CC mfano CC3000 yeye hatokwenda umbali mrefu kwa mafuta ya TSH 20,000

  3. Kadri ambavyo kiasi kingi cha mafuta kinavyochomwa kwenye cylinder kwa mara moja, ndio jinsi ambavyo utaenda KM chache kwa kila lita moja ya mafuta.
 
Kiasi cha mafuta kitumikacho huendana na kiasi cha CC.
  1. Gari yenye CC kubwa huchoma kiasi kikubwa cha mafuta ukilinganisha na gari yenye CC ndogo,kwa wakati mmoja, ndio sababu gari yenye CC kubwa huwa na nguvu zaidi ukilinganisha na gari yenye CC ndogo.

  2. Iwapo una umbali wa KM 500 na una gari mbili zenye CC kubwa na ndogo: Yenye CC kubwa itatumia kiasi kingi cha mafuta kuzimaliza KM 500, wakati yenye CC kidogo itatumia mafuta kidogo kumaliza hizo KM 500.

    Ndio sababu kwa mjini mweny vitz akiweka mafuta ya 20,000 atatumia hata siku 3 kwa mizunguk yake, Wakati yule mwenye gari ya CC mfano CC3000 yeye hatokwenda umbali mrefu kwa mafuta ya TSH 20,000

  3. Kadri ambavyo kiasi kingi cha mafuta kinavyochomwa kwenye cylinder kwa mara moja, ndio jinsi ambavyo utaenda KM chache kwa kila lita moja ya mafuta.
Umetisha fundi
 
Back
Top Bottom