Chachasteven
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 1,883
- 1,853
Habari wanajukwaa? Ni imani yangu kuwa mpo salama na buheri wa afya zenu. Kwa wale ambao mna utata kidogo na maisha poleni sana na kwa wale ambao mpo safi tuendeleeni na safari hivyo hivyo bila kuyumbishwa.
Kama kichwa cha huu uzi kilivyojieleza. Lengo langu ni kutaka kuweka awareness/kutoa elimu kwa watu na si vinginevyo. Kwa kuwa ninaamini humu ndani tunao watu wa kila aina basi bila shaka swali langu litapata majibu ambayo nayategemea kwa asilimia kubwa kama sio asilimia mia moja.
Turejee kwenye swali: Maisha yetu yamezungukwa na vitu vingi sana. Iwe tunavyokula au tunavyofanyia kazi. Ni kweli vinarahisisha sana shughuli lakini kuna wakati vinaweza kuwa na madhara. Kwa mfano moto na maji. Ukivitumia hivi viwili kwa usahihi ni burudani kwenye maisha yako, lakini ukijichanganya vinakuwa karaha. Hivyo nikawa najiuliza na ndio nawauliza na ninyi pia sasa hivi. Ni vitu vipi ambavyo vipo kwenye matumizi yetu ya kila siku - Kama madawa ya mifugo na sumu za wadudu mashambani - vinaweza kuwa hatari na hata kusababisha madhara, kama kifo, kwa mwanadamu. Kwa mfano kuna zile tetesi kuwa ukichanganya asali na tunda fulani ni sumu na unaweza kufa. Je ni kweli?? Kama vipo tuvitaje hapa chini kwa manufaa ya kila mmoja ili awe makini navyo kwa watoto na kwake pia.
Ahsante.