SWALI: Nini hutokea kwenye account za mtu za pesa anapofariki?

Rosicky

JF-Expert Member
Sep 21, 2015
1,159
1,945
Wasaalam waungwana

Kuna swali huwa najiuliza, katika maisha yetu ya civilization yamekuja na mifumo mbalimbali ikiwemo ya financial institution (Bank and mobile money). Hii mifumo imekuja na sheria zake moja ikiwemo usiri wa taarifa kati ya mtoa huduma na mpokea huduma. Yaani kila mteja ana namba yake ya siri ambayo hashei na mtu mwingine.

My take: Kwenye maisha watu hufariki wengine huugua ukichaa wa muda mrefu ilihali ana fedha benki au kwenye mobile account kama M-Pesa, Tigo pesa na Airtel money.

Swali: Je nini hutokea kwenye ile fedha ambayo mmiliki hayupo tena duniani au ameugua ukichaa au amepata sababu yoyote ile

NB: Nauliza tu sina nia ya kuchonganisha au kuogopesha watu.
 
Kwa Bank nilisikia ukifa ndugu zako wanazifata inaangaliwa nani aliandikwa kuwa mrithi ili apewe au wakati mwingine mahakama inahusika.

Mpesa makao makuu ukifiatilia unapewa baada ya taratibu kufuatwa,lakini swali ni je kama mhusika amepata ukichaa au kafa na haijulikani pesa kaweka wapi
 
Unapojaza fomu bank ,kuna sehemu unatakiwa kujaza na waangalizi was acc yako pindi utakapopatwa na matatzio ama kifoo.so ikatokea umefariki atakayekuwa na uwezo wa kufanya miamala ya kifedha ni Yule msimamizi uliyemwandika kule.
asante kwa mchango wa mawazo

binafsi sijawai kukutana na hio option

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa Bank nilisikia ukifa ndugu zako wanazifata inaangaliwa nani aliandikwa kuwa mrithi ili apewe au wakati mwingine mahakama inahusika
Mpesa makao makuu ukifiatilia unapewa baada ya taratibu kufuatwa,lakini swali ni je kama mhusika amepata ukichaa au kafa na haijulikani pesa kaweka wapi
asante umeniongezea kitu
hilo swali lako tusubiri maoni ya wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninavyojua mtu akifariki, anateuliwa msimamizi wa mirathi. Anapewa nguvu ya kisheria kufuatilia mali za marehemu + madeni anayodai etc, na kama marehemu alikuwa anadaiwa pia yeye atahusika.

Kama msimamizi anajua marehemu alikuwa na account za benki au mobile money kama mpesa n.k, anaenda kuomba apewe control zake kwa kujitambulisha na vithibitisho, cheti cha kifo barua yake ya uteuzi. Then mambo mengine yanaendelea.

Kama mlikuwa hamjui, mitandao ya pesa inaweka hela kwenye dormant account baada ya kupita kipindi fulani bila wewe kutumia account yako. Kama sikosei baada ya miaka 7 zinapelekwa benki kuu na kuwa mali ya serikali. I believe inakuwa hivyo pia kwa benki ingawa sina uhakika na muda wa kurudisha benki kuu.
 
naomba nijibu kwa upande wa benki.

Mtu anapofariki na ikiwa ndugu wanajua kuwa marehemu alikuwa na account bank..basi familia hutoa ombi la kefreeze au kumark no debit account ya marehemu pasipo afisa wa benki kutoa maelezo kiasi cha pesa kilichopo kwenye account.

Baada ya hapo familia huendelea na utaratibu wa kukaa vikao vyao vya mirathi na baada ya kumteuwa msimizi wa mirathi wananduku wataandika muktasari na kupeleka mahakamani kwa ajili ya msimizi wa mirathi kupewa kibali kusimamia miradhi.

Msimamizi wa mirathi atatakiwa kuleta viambatanisho vyote na majina ya msimizi wa miradhi kwenye bank husika na baada ya benki kupitia mwanasheria na idara ya compliance kujiridhisha na vielelezo pesa hutumwa kwa njia ya TISS kwenda kwenye account ya mahakama na baada ya hapo benki hufunga account ya mteja ...na familia kuendelea na mchakato wao huko mahakamani....
 
Ninavyojua mtu akifariki, anateuliwa msimamizi wa mirathi. Anapewa nguvu ya kisheria kufuatilia mali za marehemu + madeni anayodai etc, na kama marehemu alikuwa anadaiwa pia yeye atahusika.

Kama msimamizi anajua marehemu alikuwa na account za benki au mobile money kama mpesa n.k, anaenda kuomba apewe control zake kwa kujitambulisha na vithibitisho, cheti cha kifo barua yake ya uteuzi. Then mambo mengine yanaendelea...
Excellent, mkubwa
 
kwa u pande wa pesa kwenye simu ya mteja ...makampuni huruhusiwa cummonitor hizo pesa kwa kipindi fulani na kama mteja hatoonekana au hamna wanandugu wa kufuatilia basi hizo pesa hutakiwa kuhamishiwa kwenye account maalumu iliyopo BOT.

kipindi cha nyuma wajanja wachache walikuwa wanapiga sana hizo pesa ..na ndio maana serikali kupitia TCRA watunga sheria za kuzibana makampuni ya simu.
 
naomba nijibu kwa upande wa benki.

mtu anapofariki na ikiwa ndugu wanajua kuwa marehemu alikuwa na account bank..basi familia hutoa ombi la kefreeze au kumark no debit account ya marehemu pasipo afisa wa benki kutoa maelezo kiasi cha pesa kilichopo kwenye account...
dizaini kama una majibu mazuri ila maelezo yako sijayaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa Bank account,mfano mm mzazi kaniweka kwenye form yake hata nikienda mm japo yupo hai nahudumiwa vizuri tu,na lolote likitokea haina shida account nitaingia bila tatizo maana nilipeleka hadi passport size
 
Unapojaza fomu bank ,kuna sehemu unatakiwa kujaza na waangalizi was acc yako pindi utakapopatwa na matatzio ama kifoo.so ikatokea umefariki atakayekuwa na uwezo wa kufanya miamala ya kifedha ni Yule msimamizi uliyemwandika kule.
Mimi mbona sijawahi kukutana na hicho kipengele cha waangalizi au warithi.

Itakuwa bank gani mkuu?
 
Back
Top Bottom