SWALI : Nini haswa kinafanyika katika udukuzi wa mawasiliano ya simu.?

Complex

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
4,118
4,765
Siku za hivi karibuni nimesikia baadhi ya marafiki na watu wa karibu wakilalamika kwamba kuna watu wamekuwa wakiwadukua mawasiliano yao.

Kwamba chochote wanachofanya wao iwe kupigiwa simu ama kutumiwa sms basi kuna mtu wa 3 (mdukuzi) anakuwa anasikiliza ama anapata content ya kinachozungumzwa baina ya hao watu.

Nilipata kudodosa hii inakuwaje na inatokeaje.? Jibu nililopewa ni kuwa huyo mtu watatu anaenda katika mitandao ya simu na kuomba namba ya muhanga iwe binded na namba yake yeye.

Ikiwa hii ni ishu ya kiteknolojia, ningependa kwa uhakika zaidi kuwauliza hili jambo linatokeaje .? Ni kwa namna gani muhanga wa hili anaeza kujinasua.? Maana privacy ni jambo la muhimu sana kwa binadamu.
 
Back
Top Bottom