Usiwe na hofu wala usihuzunike.
Never too late dada yangu.
Maumivu ya majuto ni yenye kuendelea endapo hutochukua hatua.
Ni muda wako wa kujijenga upya.hakuna mwanamke anapoteza thamani.wanaolewa watu wa miaka 50 vipi wewe na kaumri hako unakata tamaa?
Muhimu shukuru Mungu sana kwa sababu bado ni mzima wa afya.
BIKIRA ni kama kizibo tu.mwenye haja atakitoa kizibo hicho na kunywa kinywaji chake.hakuna mwanaume anataka kukaa na mwanamke bikira ndani miaka yote.
Wanaume wote wanaotaka bikira basi lengo lao ni kuitoa bikira hiyo.kwa hvyo dada yangu kwa sasa bikira haina thamanai na wala usijute kuipoteza kwa sababu hata ungekuwa nayo angeitoa mumeo.
Lakini tu jihadhari za zinaa,mwanaume atakayekukubali kukuvumilia mpaka AKUOE KWA SASA HUYO NDO MWANAUME.kwa sababu atakuwa ame focus na wewe kuliko ngono zaidi.
Kipimo cha mwanamke anaefaa hakipimwi na ngono,kinapimwa na muonekano wa nje na tabia kwa ujumla.
Usijekubali kuchezewa kwa kigezo cha kuonjana kisha ndo ipite ndoa.wewe ni wa thamani sana,thamani yako haithibitishiki kwa ngono tu,thamani yako inaweza kuthibitishika hata pasi na ngono.
Mwanaume atakayekufuata na kutaka ngono ili athibitishe thamanai yako basi mkimbie.MKIMBIEEEE HUYOO.
Mwanaume atakayeshindwa kuthibitisha na kukubali thamani yako mpaka akufanyie ngono,basi hawezi kuthibitisha thamanna kuikubali thamani yako hata baada ya ngono.
Atakayeiona thamani yako pasi na ngono,huyo ndo mwanaume wa kweli anayekufaa.
Katika ndoa tendo la ndoa ni tendo ambalo kwa kawaida linachukua kama nusu saa ama lisaa limoja kulifanya.
Tendo la lisaa limoja haliwezi kuwa kigezo cha kuthibitisha thamani yako.baali matendo yako ya muda wote ndiyo yanaweza kuthibitisha na kuwa kigezo cha kupima thamanai yako.
Tebdo la ndoa halifanywi kila siku katika Ndoa,sasa je ni kipi kinafanywa kila siku katika Ndoa?
Basi hicho ambacho unafikiria kinafanywa kila siku katika Ndoa kama vile kupika na kukaa na mume vozuri na kutumia tabia yako kuishi naye basi hayo ndiyo ambayo yanatakiwa upate mwanaume aone umuhimu wa wewe kuwa na hayo mambo yanayoweza kuwa applied kwa siku zote katika ndoa.
Bado una thamani kubwa sana mbele ya wanaumee.bado wanakupenda sana wanaume lakini tumeumbwa na mioyo ya kioo,hatukijui cha moyoni mpaka tuseme.
Kuwa na subira,tulia,usiwe na papara.
Usikumbuke sana ndoa ukasahau anayekuoa.bali mkumbuke anayekuoa kwanza.
Ukipata mume mwema na mstaarabu basi ndoa yako itakuwa njema na ya kistaarabu pia.ndoa haiwi njema mpaka wana ndoa wawe wema pia.