NAIKATAA CCM kwa sababu imeshindwa kabisa kuboresha maisha ya Mtanzania wa chini.
CCM imeleta matabaka kati ya walio nacho na wasio nacho.
Usipo kuwa nacho hutukipata kamwe, wanao watasoma shule za hovgyo kabisa zinazoitwa za kata, zisizo na madawati, vitabu, maabara wala maktaba. Waalimu wa shule hizo ni form six leavers waliopewa mafunzo ya miezi miwili, Yaani mtoto anafundishwa na bora mwalimu, sio mwalimu bora.
Wao watoto wao hawasomi huko, wanasomeshwa nje ya nchi, na kama watasoma hapa nchini, basi ndio watasoma kwenye zile shule zenye kutumia mitala ya nje, na wakimaliza wanakuwa wamepewa nafasi nyeti, kwenye mashirika nyeti.
CCM i meshindwa kupambana na rushwa, inakumbatia rushwa na imekuwa ikiita kwa majina mazuri kama takrima. Wanyonge hatuna haki wala stahili kwenye nchi yetu.
CCM imeshindwa kulinda na kutete rasilimali za TAIFA letu, hebu tazama wanyama pori wetu wanavyopandishwa ndege na kutokomea ughaibuni, hamna anayejali. Hili lichama la ukoo wa KIKWETE silipendi kabisa