Swali la Uchokozi kwenu wanawake

ESCORT 1

JF-Expert Member
Dec 7, 2015
1,368
2,890
Nisipoteze muda, kwa wanawake mliopo kwenye ndoa kwanini wengi wenu huwa mnawachukia sana ndugu wa mume wanapokuja kuwatembelea? Yaani ndugu wa mume akija mnapoishi hata kama ni mgonjwa mtafanya figisu mpaka aondoke lakini wakija ndugu zenu huwa hamtamani waondoke hata kidogo. Je hii husababishwa na nini, karibuni mtiririke.
 
Hapa lazima wachangiaji wapungue. Tena mi naomba niongezee tu kidogo kuwa hata kama wakikuta una mtoto asilimia kubwa huona tabu sana kutoa malezi toshelezi yenye uwiano sawia na mwanaye wa kumzaa kinyume na sisi wanaume!
 
Mbonaa moma kaolewa na baba ila wageni wakija wa upande wowote namuona mama anafurahi sanaaa na hatamani waondoke

ESCORT 1 acha kupotosha umma buana
Mkuu wazazi wetu( mama zetu wa enzi hizo) most of them walikuwa na mioyo ya kipekee ndio maana familia zetu nyingi zimeishi maisha ya extended family bila shida yaan nyumban mnahudumiwa sawa bila kujali huyu wa mtoto wa mjomba, shangaz, binamu n.k but wadada wa siku hiz japo sio wote wengi ni wachoyo na wabinafsi ndio maana hawapendi ndugu upande wa mume japo mtafutaji ni kaka mtu.

Nina experience na hilo sio kwangu tu hata kwa washkaji zangu kipindi tunasoma yani ukienda likizo design kama shemeji ananuna ila sura inaanza kubadilika taratibu ukiingia chuo. Mwisho ukishapata na kazi unashangaa cm zakutosha huku ukilalamikiwa eti siku hiz umetutenga
 
Nadhani kuna haja ya kuwepo alert kama mada iliyokwishashajadiliwa humu basi mtu anapopost uzi ajue ipo kabla ya kupost. Hii mada imejadiliwa humu ndani mara nyingi saana.
Kwa hiyo una shauri mtoa mada awe ana search thread kama ilishapostiwa before.. ila sijaona baya lolote hii mada kwangu mpya sio tatizo
 
Hapa lazima wachangiaji wapungue. Tena mi naomba niongezee tu kidogo kuwa hata kama wakikuta una mtoto asilimia kubwa huona tabu sana kutoa malezi toshelezi yenye uwiano sawia na mwanaye wa kumzaa kinyume na sisi wanaume!
Mama tu akizaa hawapi upendo sawa wanae,itakua mtoto wa mume?!, mtoto wa kambo apewe haki zake za msingi,ila kusema atapata mapenzi kama ambayo angepewa na aliemzaa..impossible!
 
Mama tu akizaa hawapi upendo sawa wanae,itakua mtoto wa mume?!, mtoto wa kambo apewe haki zake za msingi,ila kusema atapata mapenzi kama ambayo angepewa na aliemzaa..impossible!
Mbona baba wakambo kwa asilimia kubwa anaweza?
 
Mama tu akizaa hawapi upendo sawa wanae,itakua mtoto wa mume?!, mtoto wa kambo apewe haki zake za msingi,ila kusema atapata mapenzi kama ambayo angepewa na aliemzaa..impossible!
Baba mbona kwa asilimia kubwa inawezekana?
 
Hao ndugu wengi wana dharau mno kisa mume ni ndugu yake basi nae anataka aonekane ana sauti ndani ya nyumba.
 
Ndugu wa mume wana hila, hawana jema...kumfuatilia mke kafanya nini...kujitia kuwa na sauti ndani ya nyumba...umbea umbea ndiyo maana mtu unaona ni bora kujiepusha nao ingawa wapo baadhi hawana shida na wanakaa vizuri.
 
Mama tu akizaa hawapi upendo sawa wanae,itakua mtoto wa mume?!, mtoto wa kambo apewe haki zake za msingi,ila kusema atapata mapenzi kama ambayo angepewa na aliemzaa..impossible!
Wapo ambao wanapata mapenz kwa mm zao wa kambo kuliko hata kwa mam zao walowazaa
 
Hayo yote yanaweza kusababishwa na uchoyo wa vyakula ila mambo mengine inabidi utumie akili hakuna haja ya kuwaona ndugu wa mme kama shetani wakija wachangamkie wape wakula hata kama kuna maneno yatatokea mme atakutetea.

Nb hata usipowapenda jua hao ni ndugu zake na wewe ni mtu wa kuja so hakuna haja ya kuwajengea chuki
 
Back
Top Bottom