Swali la uchokozi kwa UDART: Hamsini hamsini zetu huwa wanazipeleka wapi?

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,762
Imekuwa ni kitu cha kawaida sasa kila ukinunua Ticket ya mwendokasi (UDART) ambayo inauzwa TSh 650 na ukatoa hela kubwa zaidi ya hiyo utaambiwa hawana shilingi 50.

Mfano kama umetoa elfu moja utarudishiwa shilingi 300 badala ya 350 wakidai hawana shilingi 50.

Swali ninalojiuliza je hizi chenji hamsini hamsini zetu huwa wanazipeleka wapi, na kwanini hawajipangi kupata hamsini hamsini nyingi kwa ajili ya kuwarudishia wateja kama wanaona demand ya hiyo sarafu ni kubwa?

Je, huu hauwezi nao ukaitwa wizi?

1.jpg
 
Chenchi wanazo na wanakua wamezifunika na kitambaa ili WA accumulate ukitaka muende sawa piga simu ile ya customer care yao then uwaambie uone kama hujapewa fasta ni wezi tu hao attendant
 
Mimi huwa naboreka kwakweli, wameshatufanya mtaji wao ..ni bora waseme nauli 700 tujue hela inaemda kihalali kuliko kuacha 50 bila maelezo
 
Juzi nilitoa 700 pale Kimara , kwa nyodo na dharau za kijana mkatisha tiketi akakataa kunipa 50 yangu.
Nikamwambia nahitaji chenji yangu vinginevyo sitoondoka. Akahisi namtania. Nikamwambia kama umeichoka kazi yako usinipe hiyo pesa, maana unajaribu kuhalalisha dhuluma kuwa halali.
Kiukweli tuna safari ndefu sana.
Alinipatia baada ya kuona sina masihara nae.
Rudi Mbezi, huku ndio vituko vitupu. Hakuna uhakika wa vibanda vya kujazia masalio kwenye kadi za UDART. Wahusika wanafanya wanavyotaka, Mara hatuna chenji,Mara mashine IPO chaji.....tabu tupu.
UDART wameshindwa kusaida abiria wa Mbezi kwa kuanzisha route ya Mbezi- Kariakoo, Mbezi- Kivukoni....inakera mno hii hali. Wahusika wamefumba macho
 
Yaani ni changamoto sana. Bado tuna safari ndefu
 
Wafanyakazi hawa wanaokatisha tiketi nadhani wamefanya shilingi hamsini kama mradi wao wa kujipatia kipato cha ziada kisicho halali.
 
Da hio ni changamoto waitatue ila kuepukana na yote ni kubeba chenji kamili Au wapunguze iwe 600,changamoto nyingine ni suala LA milango ya kuingilia mingi wanafunga upande mmoja mfano mapipa pale ukishuka inakubid urudi nyuma ndo utoke wkt we unaenda mbele hii pia changamoto, pia wajitahid kurekebisha miundo mbinu yao inapoharibika mfano mashine zingine,nguzo zikianguka wazirekebishe,pia waweke uzio mdogo kwenye baadhi ya vituo Kwa usalama wa abiria wawezaanguka wakati gari likija sababu unawezapatwa na shida yeyote mfano kizunguzungu,nguvu ya uvutano au shida yeyote .
 
Back
Top Bottom