Swali la tafsiri ya terrorism linasaidia nini kesi dhidi ya Mbowe?

Kazi ipo.
Kesi ya Shutuma za Ugaidi swali "Nini maana ya Terrorism kwa Kiswahili"...
Inamaana wewe mleta mada huoni kabisa uhusiano wa swali na kesi?

Au umepost kujitafutia ka umaarufu kako tu,?
 
Kama siloli naye anashindwa kutofautisha jinai na ugaidi basi hata watu wakiibiana wake mmoja akaanza kumtwanga ngumi huyo ni gaidi....
 
Hivi wale manjagu tuliokuwa tunawaona wanasoma vyuoni huko wako wapi waokoe jahazi maana kupeleka watu hawajui kitu na kudharirisha kada nzima ni hatari sana kwa kweli..
 
Tanzania na Africa kwa ujumla upinzani unapigwa vita sana. Mara nyingi wanaonewa kwa kubambikiwa kesi ili tu wasikosoe serikali. Watawala wa Africa wanatumia nguvu kubwa mno kuulinda utawala waoa. Hivyo atatumia kila njia kumkandamiza mpinzani. Hii inaonesha wazi pia huyu jamaa anaonewa. Hasa alipogusia swala la katiba mpya.
Chedema ni kampuni ya mtu sio chama cha siasa..alafu kwa tafsiri jingine ni chama cha kuwatete kabila fulani Tanzania.
 
Ni kwa sababu ni wanasiasa na siasa ni vita baina ya wanasiasa.
Mpira una sheria 17, siasa haina bali walio madarakani Ndio wanaoweka sheria. Hii ndio sababu ya vita.
Jogoo liloanza kuwika haliruhusu jogoo lingine kuwika.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Ndio wananchi wote wanaopenda demokrasia wanafanya makosa makubwa kulala vitandani mwao wakati demokrasia inapohujumiwa na watawala.
 
Hapo vip!!

Binafsi maswali kama haya natafsiri kama maswali ya kitoto yasiyoweza kusaidia upande wa utetezi.
Hata kama lengo nikumchanyanya shaidi ila me naona haisadie sana kwa jinsi kesi na ushaidi wa jamuhuri ulivyokaa wazi.

Cha ajabu baadhi ya vyomba vya habari vinasema shahidi ashindwa kujibu maswali kwa kuangali swali kama hili ambalo haliwezi kusaidi katika kesi hii.

Naona kuna ushabiki wa baadhi ya mitandao na vyombo vya habari kwa lengo la kutaka kutengeneza image ya kesi hii kwa wananchi pasipo kuonyesha upande mwingine wa shilingi.

Narudi hii kesi imemkalia bwana yulevibaya tuache ushabaki.
Kama unaona ushahidi wa Jamhuri umekaa Wazi si ufurahi Sasa? Unaleta thread za kifala Fala na Kuwait'a watu majina ya kutweza ili uonekand wa maana kumbe Zuzu tu. Tuoneshe hapà huo ushahidi ulio Wazi na kesi ilipomkalia Mbowe pabaya!!!
 
Swali hilo kama ilivyo maswali mengine ya Mawakilo wa utetezi Hayana Msaada Wowote kwa Mheshimiwa Mbowe hasa linapokuja Suala la Tuhuma dhidi yake

Mawakili.wa Mbowe wajikite kupangua hoja zinazowaeoloshwa.na Jamhuri dhidi ya mteja wao

Askari ambaye Ni shahidi wa Serikali amejieleza vizuri Sana na anaijua kazi yake vizuri
Hivi unajua kwamba Mbowe bado hajafikiwa katika kesi. Kwahiyo subiri zamu ya kusikilizwa mashtaka yake ndio utajua anasaidiwa au anaisaidia serikali kujijua ina jeshi la polisi la namna gani?
 
Hayo maneno yote mawili hawezi kuharibu uhalisia wa Forensic Report iliyotolewa. Report inahusu uchunguzi wa silaha yeye anauliza maana ya Terrorist na Terrorism. Ningekuwa mimi ningemuuliza maswali yanayohusiana na silaha zaidi ili kumpre-empt utaalamu wake wa silaha. Lakini wakili wa utetezi unamuuliza definition ya terrorist na terrorism ambayo haina impact kwenye utaalamu wake lakini angemuuliza maswali yanayohusiana na silaha na akashindwa kujibu then utalaamu wake ungekuwa questionable.
Ndo maana nalubaliana na wanaosema CCM imeishiwa wenye hoja. Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba Cpl Abdalla aliulizwa swali moja tu.
1.Haluulizwa Kwa nini kielelezo mahakamani ni risasi yeye kaleta maganda?
2.Hakuulizwa Kwa nini kaharibu kielelezo na ni Sheria ipi au maagizo yapi yalimruhusu kubadili Hali ya kielelezo toka risasi kuwa maganda?
3.Hakuulizwa Kwa nini Aina ya maganda ni tofauti na Ganda la risasi moja nzima iliyobaki?
4.Hakuulizwa barua ya maelekezo ya kufanya uchunguzi iliandikwa katika lugha gani akajibu ni Kiswahili?
5.Hakuilizwa alichagua kuandika ripoti kwa kiingeeeza Kwa vile anaijua lugha hiyo vizuri Sana akajibu ndiyo?
6.Hakuulizwa kama anaijua vizuri nini maana ya terrorist akajibu ni ugaidi na terrorism akasema ni Utalii?

NB: Msilete hoja Kwa kudonoa wenzenu tunafuatilia hatua Kwa hatua.
 
Kisheria ina maana kubwa sana. Ni kesi nyeti hivyo inahitaji uchunguzi makini toka kwa watu makini. Neno moja linaweza umiza mtu au kuleta maana tofauti ktk report. Hivyo wakili anajaribu kuonyesha mapungufu ya ripoti na muhusika pia ili kuipunguzia credibility ya report husika .
Darasa aliwahi kuimba, "kumwelimisha Zuzu utajipa kazi". Huyo utakesha naye.
 
Riport kaandika yeye katumia Hilo neno anaulizwa ufahamu wake kuhusu Hilo neno anaonekana hajui utaiamini hiyo ripoti?
Upo kwenye usaili (interview)
Unaulizwa Mambo yaliyopo kwenye CV yako unaulizwa mwaka uliomaliza shule unataja mwaka tofauti na uliopo kwenye CV
Unaulizwa swali la ufahamu tu kuhusu fani yako gaidi Ni Nini na Ugaidi Ni Nini unaanza kuleta stori za mtalii!
Mosi tunaanza kuwa na mashaka na ufahamu au utaalamu wako katika fani yako Kama Ni interview unakuwa ushapoteza toka dakika ya Kwanza.
Tambua kuwa hukumu ya kweli huwa Ni hukumu ya watu sio hukumu ya mtu.
haki ikitendeka watu hushuhudia kuwa haki imetendeka.
HATA MAANDIKO YANATUKUMBUSHA MUNGU ATAHUKUMU MBELE ZA BINAADAMU WOTE, NAO WATASHUHUDIA NA KUSEMA HAKIKA BWANA HUKUMU ZAKO NI ZA HAKI NA KWELI.
Kama tumeahidiwa kuipitia hukumu ya Mungu tunashindwaje kuthibitisha hukumu ya binadamu?
Akihukumiwa katika haki na kweli tutaona na asipohukumiwa katika haki na kweli pia tutajua.
Kweli kabisa ingawa wafuatiliaji si wanasheria lakini wanajua kama haki inatendeka au la.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kwani sheria inasemaje mwenyekiti akiwa kifungoni tuchague mwingine maisha ya chama yaendelee tu
 
Hapo vip!!

Binafsi maswali kama haya natafsiri kama maswali ya kitoto yasiyoweza kusaidia upande wa utetezi.
Hata kama lengo nikumchanyanya shaidi ila me naona haisadie sana kwa jinsi kesi na ushaidi wa jamuhuri ulivyokaa wazi.

Cha ajabu baadhi ya vyomba vya habari vinasema shahidi ashindwa kujibu maswali kwa kuangali swali kama hili ambalo haliwezi kusaidi katika kesi hii.

Naona kuna ushabiki wa baadhi ya mitandao na vyombo vya habari kwa lengo la kutaka kutengeneza image ya kesi hii kwa wananchi pasipo kuonyesha upande mwingine wa shilingi.

Narudi hii kesi imemkalia bwana yulevibaya tuache ushabaki.
Wew n kima hujui ktu
 
Tanzania na Africa kwa ujumla upinzani unapigwa vita sana. Mara nyingi wanaonewa kwa kubambikiwa kesi ili tu wasikosoe serikali. Watawala wa Africa wanatumia nguvu kubwa mno kuulinda utawala waoa. Hivyo atatumia kila njia kumkandamiza mpinzani. Hii inaonesha wazi pia huyu jamaa anaonewa. Hasa alipogusia swala la katiba mpya.
Mku, mfano mzuri ni rais wa sasa wa Zambia alivyotendewa na rais aliyeshindwa, Edgar Lungu

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom