Swali la mwaka: Nani alimleta Ballali nchini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali la mwaka: Nani alimleta Ballali nchini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 30, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 30, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu aliyetoa ushauri wa Ballali kuwa mshauri wa kiuchumi wa Mkapa na baadaye Gavana wa Benki Kuu. Mtu huyo alijua mambo kadhaa:

  a. Alijua sifa za kisomi za Ballali ambazo zingetukuzwa (kusema anakuja toka WB na mchumi aliyebeboa)
  b. Alijua udhaifu wa Benki Kuu
  c. Yuko karibu na Rais Mkapa
  d. Alikuwa na maslahi katika mafanikio ya mipango yao
  e. Alikuwa ni mtu ambaye yuko karibu na watawala kiasi cha kuweza kuaminiwa katika masuala ya kiuchumi.
  f. Alikuwa ni mtu mwenye mtandao mzuri wa wafanyabiashara ambao walikuwa tayari kufanya lolote kwa neno lake.
  g. Ni mtu ambaye kwake Tanzania ni kisima cha utajiri!


  Mkishamjua mtu huyo mtakuwa mmemkamata ring leader of organized crimes in Tanzania. Huyo ndiye atakuwa aliyebuni na kusimamia wizi wa fedha nyingi toka Benki Kuu na pia mikataba mbalimbali mibovu!

  Ni nani huyo?
   
 2. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji,

  Mie nina uhakika kabisa balali alipewa kazi kutokana na uwezo aliokuwa nao na wakati Ballali anakuja hapa Tanzania hakuja kama Msahuri wa Mzee Ben bali alikuja kufanya kazi ya World Bank kakita jitihada za WB kusaidia nchi zilizokuwa zinaendelea.

  Ballali aliletwa na World Bank na kama kuna mtu alimshauri Mkapa ampe kazi Ballali atakuwa ni Katibu Mkuu kiongozi na yeye alifanya hivyo baada ya kupatikana vetting report kutoka kwa watu wa Usalama wa Taifa.

  Nakumbuka Ballali aliitwa na Mkapa pale Magogoni siku ya Jumapili na kuambiwa ameteuliwa kuwa Gavana na hakupewa muda wa kutafakari kuhusiana na hilo ila inasemekana kuna wizi flani ulitokea pale BOT na Mkapa alikasirishwa sana na kuagiza yafanyike mabadiliko makubwa pale BOT. Sema kipindi hicho watu wa aina ya Ngurumo na Mwanakijiji, Watu wenye uwezo wa kusema yale magumu kama Kubenea walikuwa hawana meno.

  Ilikuwa ni tabia ya Mkapa kumfukuza mtu yeyote yule pindi anapokosea, mtakumbuka jinsi alivyomfukuza Mattaka pale PPF. Alivyomuomba Mboma aachie ngazi baada ya kashfa ya sukari, mie nilishangaa sana Mboma kurudi na kutaka ubunge!

  Mkuu Mwanakijiji kama utakumbuka wakati Mkapa akiwa pale Foreign alikuwa ni Waziri pekee ambaye alikuwa akirudisha pesa wizarani kila mwaka na alikuwa na rekodi safi sana katika utendaji na utumiaji wa pesa za umma, na hii ilisababisha Mwalimu kumkubali mapema sana tofauti na wengine waliogombea 1995 (kumbukeni kashfa flani za madini 1994).

  Mzee Mkapa alibadilika sana kuanzia kifo cha mwalimu, nadhani alighafirika na kupoteza mwelekeo na kuna watu walijiingiza sana pale na kujidai walikuwa watu wa karibu na mwalimu.

  The one and only person wa kulaumiwa mpaka leo ni Ruhinda!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Dec 30, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  Mmh.. ni nani nani aliyempendekeza kuwa Gavana wa Benki Kuu? Hayo unayoyasema nakubaliana nayo kwa kiasi kikubwa lakini naamini kabisa tukichora mstari wa kufuatilia utaona kwamba Ballali kuingia Benki Kuu kuwa Gavana hakukuwa kwa bahati mbaya hata kidogo. Kuna watu ambao walijua watanufaika na Ballali kuwa Gavana kuliko mtu mwingine... ni nani hawa?
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Dec 30, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,736
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  Gembe, Mwanakijiji,

  ..kuna jamaa ambaye yuko kwenye circles za watu wa BOT aliniambiwa kwamba Mkapa alishatoa statements kwamba lazima angemuengua Dr.Idris Rashid toka BOT.

  ..sasa inasemekana Mkapa hakumfukuza Dr. Rashid ila alisubiri mpaka mkataba wake ukaishi na baada ya hapo haku-renew. Magavana wa BOT hufanya kazi kwa mkataba.

  ..Ballali aliletwa toka WB na akawa mshauri wa Rais. Lakini wadau wa BOT walikuwa wanajua kwamba alikuwa ndiye Governor in waiting.

  ..binafsi sifahamu nani alipenyeza jina la Ballali kwa Mkapa, lakini inawezekana walifahamiana tangu Mkapa akiwa balozi wetu Washington-DC.

  ..kumbuka kwamba Ubalozi wa Washington-DC ndiyo unashughulika na masuala na mashirikiano ya Tanzania na WB/IMF ambako Ballali alikuwa ameajiriwa.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Dec 30, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ngoja tuweke jambo moja kwa usahihi; kuna Watanzania kadhaa ambao wamefanya kazi BoT na wengine kwa umahiri mkubwa tu (kuna yule jamaa aliyeandika hata kitabu chake kuhusu sakata lake nadhani WB au IMF) na wapo wengine wanaofanya sehemu mbalimbali. Kwanini ilikuwa ni Ballali?

  Watu waliokuwa wanafahamu mambo wanajua Ballali ndiye alikuwa ameandaliwa kuwa Gavana. Tukiangalia kwa wakati ule tuliona ni kwa sababu za umahiri wake katika mambo ya uchumi... Lakini miaka hii ya sasa tunapoangalia uozo uliofanyika Benki Kuu kwangu naamini aliingizwa pale kwa wakati kama huu! Alikuwa ni mtu wao!

  Ila hawa "wao" ndio kina nani? Sidhani kama Mkapa hakujua kilichokuwa kinafanyika BoT 2000-2005...
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkjj vp ni Sir A.C (the masonic) nini?
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Gembe mkuu heshima mbele.

  Nakubaliana na wewe mia kwa mia kuwa Ben alikuwa mtu makini na muadilifu sana alipokuwa anafanya kazi chini ya Kambarage. Hata baada ya kuwa Rais kabla Kambarage kufariki Ben bado alikuwa mtu muadilifu.

  Mtu aliyemfanya mpaka akaingia mkenge ni rafiki yake balozi mstaafu Ruhinda; Rostam Aziz alitafuta njia ya kumuingia Ben na uchochoro aliouona ulikuwa ni Ruhinda na through Ruhinda, Rostam akawa karibu na Mkapa na kuweza ku-influence mambo mengi hata kuweza kumuingia Ballali BOT.

  Ruhinda na Rostam wakawa 'business partners' kwenye magazeti na hata VodaCom. Ndio maana hata hivi karibuni Rostam alikuwa 'gallant defender' wa BWM kwenye NEC ya CCM!

  In short Ruhinda ndio alifungua njia ya RA kuweza kumuingia Ben na kufanya madudu yote haya yanayoiaibisha nchi yetu!
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Dec 30, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Sumaye?? No sitaamini kaachwa pembeni na wahujumu uchumi, ambao wengi ni wana mtandao.

  Rostam, sijui, angekuwa amempa mke wa kiarabu Mkapa, ila hachezi mbali na hili.

  Ok, kwanza ni toss, Based on JokaKuu kama hawa watu walifahamiana huko huko basi hapa ni:

  AIDHA MKAPA MWENYEWE AU CHENGE.

  Mh, swali gumu ila zuri, kafungulie kainzi basi katusaidie
   
 9. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkjj, najua unakotaka kwenda lakini, Ballali alifanya kazi za kuinua uchumi wa nchi nyingi za Africa na kusema ukweli kazi aliyofanya huyu bwana ilikuwa kubwa na WB na IMF hawakutaka kabisa Mkapa amchukue kwa sababu walitaka asaidie nchi nyingi za sub sahara Africa badala ya nchi moja tu.

  Mkapa and his family knew Ballali personally kabla ya kuwa president, na kwa kweli appointment ya Ballali ilikuwa na manufaa mno kwa Tanzania.

  What happened baada ya kuwa Governor na what happened to Mkapa baada ya JKN kufariki ni kitendawili tega.
   
 10. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2008
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ni mama wa kwanza wa zamani !!
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kuwa BMW hakupendelea kuwa Idris Rashid aendelee kuwa gavana wa BOT baada ya madudu yake aliyofanya kuhusu Meriden Biao Bank, Trust Bank, Greenland Bank and not to mention magendo ya Debt conversion.

  In the course of searching for a replacement, nadhani jina la Ballali likaibuka kwa sababu kwanza alishafanya kazi BOT kwa muda mrefu kama Research Director kabla ya kwenda IMF na pili kule IMf alifanya kazi nzuri zilizohusiana na developing countries kwahiyo, on the basis of his record na kwa vile alishakuwa bosi wa wakina Rashid, Mgonja etc he became the right person to replace Rashid in a peaceful transition.

  Ballali kwa wale wanaomfahamu, alikuwa mfanyakazi hodari na muadilifu; amekuja ingizwa sumu na genge la Rostam kwa kupitia kwa Ruhinda mpaka kumuingia BWM. Ballali was pressurized to do what he did on the understanding kuwa BWM alikuwa amebariki ukwapuaji wa mabilioni hayo ya fedha!

  Hiyo ni dilemma iliyompata Ballali na ndivyo nadhani itakavyompata huyu Ndullu; kwani sidhani kama ana ubavu wa ku-resist pressure ya CCM mafia ikiongozwa na Rostam!
   
 12. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni RA.

  Inawezekana kabisa kuwa sikupata jibu kwa 100%. But Iam also very sure kuwa sikupta 0%.

  Kuna wakati kwenye fani fulani fulani... kuna kuwa na factor ambayo ni "so common" kiasi ambacho hata swali likiulizwa kama ilivyo hapa... na hujui jibu ukiiweka factor hiyo... unakuwa umegusa jibu kwa % fulani... hata kama sio zote.

  Kwa swali lilivyoulizwa hapa... hakuna uwezekano kuwa RA hakuhusika hata kwa % 1. RA ni key maker wa ufisadi kwa kiwango kikubwa kwa taifa la Tanzania.

  Ni vipi awe hakuhusika?

  No way!!!
   
 13. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Baada ya kusoma kitabu chake nitasema ni Andy Chande! This guy was patient during the nationalizations, sasa he managed to loot more than his milling plant could have ever given him... ANDY CHANDE!
   
 14. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha swali simpleeeeeeeeeeeee

  Ni wananchi wa Tanzania ndio waliwezesha Ballali kuwa Gavana. Maana kwa kupitia kwao walimfanya Mkapa kuwa Rais wao na kwa jinsi hiyohiyo Mkapa akamweka Ballali kuwa Gavana. Kwa namna nyingine wananchi wasingemwezesha Mkapa kuwa Rais basi naye Ballali asingepata kuwa Gavana
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Dec 30, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Azimio.. umesema kitu kimoja muhimu nacho ni common denominator... swali langu kimsingi linahusu hiyo common denominator na ninaamini kuwa tukijua mazingira ya Ballali kupata kazi BoT na kuwa pale muda wote wizi unatokea na baadaye kuondoka kimya kimya katika mazingira ya shuku hatuna budi kuamini kuwa hata madai kuwa "alikuwa ni muadilifu" yanaweza kuwa si sahihi... haiwezekani watu wawili waadilifu (Mkapa na Ballali) wasimamie wizi mkubwa kabisa wa fedha za Taifa katika historia ya Afrika huru!!

  Uadilifu waliokuwa ni uadilifu kweli au kukosa nafasi ya kuwa mafisadi! Mwizi ambaye hana cha kuiba anaweza kuitwa mwadilifu?
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Dec 30, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,736
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  Bulesi,

  ..mimi nilikuwa kati ya wale walioamini kwamba Mkapa was never tested ktk hayo mambo ya ufisadi na rushwa. hakuwahi kuongoza wizara yoyote ile ambayo ilikuwa na ulaji.

  ..kama Mkapa ange-serve Hazina, Nishati na Madini, na Trade and Industries, ambako fedha ziko nje-nje na bado akatoka msafi basi ningekubaliana na zile tambo kwamba jamaa ni msafi.

  ..vilevile Mkapa alikuwa sidelined wakati wa Mwinyi kwasababu alionekana kama ni mtoto wa Mwalimu. Matokeo yake akaondolewa pale Foreign na kutupwa Sayansi na Teknolojia, ambako alikuwa akinyanyaswa na Dr.Bilali!

  ..naamini alipoingia pale Magogoni alikuwa na hasira zake na ndiyo maana mwanzoni akawatema watu wote waliokuwa sehemu za ulaji wakati wa Mzee Ruksa, the likes of George Mbowe, Mustafa Mkullo, David Mattaka, Idiris Rashid...

  ..Kifo cha Mwalimu kulitunyang'anya wa-Tanzania mtu mwenye moral authority ya kukemea rushwa na kupinga ufisadi ndani ya Chama na serikali. MWALIMU alikuwa akifanya kazi ambayo ilipaswa kufanywa na BUNGE na PRESS.

  ..wa-Tanzania tunapaswa kujilaumu wenyewe for taking too long in shaping up and taking ownership of our country baada ya kifo cha Nyerere. Mazingira hayo ndiyo yaliyompa Mkapa na wenzake kufanya yale waliyoyafanya.

  NB:

  ..tulipoteza muda mwingi kumsakama Waziri Mkuu Sumaye. Ilifika kipindi wananchi wakasema: "Mkapa ni msafi lakini anachafuliwa na Sumaye." Ikifika mahali Waziri Mkuu wa Tanzania akaiba ujue Rais na mawaziri wengine wanaiba 10 times.

  ..tena baadhi ya wabunge wa upinzani na magazeti ndiyo walikuwa vinara wa kumtuhumu Sumaye huku wakimwacha Mkapa, Ballali, Mramba, Yona, Chenge wakipora walivyopenda.

  ..Mbunge kama Wilbroad Slaa alikuwa mstari wa mbele kumsakama Sumaye kwa kukodisha shamba la eka 7 pale Kibaigwa, wakati Mkapa akicheza na Net Group na Kiwira.
   
 17. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kumbe JF watupu wa data hivyo? Hamjui jibu la swali la Mwanakijiji?

  Mhusika ni mwanamke, nipe mji nitawamalizieni. Ana jina linaanzia na M.
   
 18. v

  vstdar Member

  #18
  Dec 30, 2008
  Joined: Apr 8, 2008
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anna Mkapa...
  kwanza aliletwa ambaye baadaye kawa mke wa Ballali...Muganda, huyu alikuja km economic advisor wa mkapa....kama haitoshi ndo akaletwa Ballali......
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Dec 30, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mmmhh....wewe unaweza kuzua jambo....
   
 20. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ana jina linaanza na M na anatokea mkoa wenye jina linaloanza na M.
   
Loading...