Swali la kidemokrasia: Asiyetaka kukosolewa,anataka nini?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Kauli au matendo ya watu au vyama huwa na mapungufu ya hapa na pale. Watu au vyama vingine huyasema mapungufu hayo katika namna ya kukosoa. Sasa,hapa nchini,inamea tabia ya kuchukia kukosolewa.

Kukosoa ni kuweka sawa. Kwahiyo,kukosolewa ni kuwekwa sawa. Inapotokea mkosolewaji au wakosolewaji hawapendi wala kutaka kukosolewa,wanataka nini hasa?

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
 
Ukiona hivyo ujue wanataka sifa ambazo hawana,tatizo hata wengine wamelibeba hivyo hivyo!Inakuaje uruhusu kusifia ila kukosoa mwiko?????
 
Mkuu Vutanikuvute mbona Leo unazunguka mbuyu?
Nyoosha maneno kwa kusema............

"Ni kwanini Raisi Magufuli na serikali yake hawataki kukosolewa? "

In general toka enzi za chama kimoja mpaka leo vyama vingi, yeyote anayejaribu kukosoa uongozi wa juu anachukuliwa kama msaliti either atatengwa au kufukuzwa chama.

Imekuwa ni zidumu fikra za Mwenyekiti muda wote, iwe chama tawala, iwe vyama pinzani. So, hizi ndo siasa zetu Afrika.
 
1..rais nasimama hadharani na kusema wazee ndio wameliharibu taifa hili..hivi wazee hawa ndo walilipa zaid ya bil 250 hewa kwa wakandarasi au ndio walinunua ile boti mbovu toka dar to bagamoyo?!!!
2..bunge kuwa sehemu ya idara pale ikulu ni jambo hatari sana
3. ..rais anaongea hadharani mbele ya wawekezaji/wafanya biashara eti akitokea waziri akakwamisha basi nitamfukuza mara moja mi nataka nchi ya viwanda we unakwamisha..you will go....hiyo kauli alipaswa kuotoa ndani ya kikao cha baraza la mawaziri na sio hadharani kwa kiwango kile atawaanya wasaidizi wake waanye kazi kwa uoga lakini pia wapiga dili wanaweza kutumia nafasi hiyo kufanya yao maana ...

kufika anakotka kufika itamchukua mda sana kwa mwendo huu ndna ya bunge na huko magogoni....mtaani sukari hakuna hakuna na wamecreate mess hii wao na sasa wamejikunyata...wakiambiwa wanabweka ...hatari sana
 
Kutoswa kwa Lowasa na kupatikana kwa Magufuli ni matokeo ya seikali ya CCM kukubali kukosolewa. Kushindwa kwa Chadema kwenye uchaguzi uliopita ni matokeo ya Chadema (especially mwenyekiti wao) kutokukubali kukosolewa.
 
Mkuu Vutanikuvute mbona Leo unazunguka mbuyu?
Nyoosha maneno kwa kusema............

"Ni kwanini Raisi Magufuli na serikali yake hawataki kukosolewa? "
Mengi yanayotolewa kwa serikali ya Magufuli ni malalamiko tu, si ukosoaji, kwa sababu ukosoaji huendana na kuonyesha njia mbadala. Ukisema fedha imekuwa ngumu kupatika toa na suluhisho lake, labda wapiga dili waachiwe mianya ili pesa ziingie mtaani. Ukisema sukari imeadimika toa na mbadala wako, labda turuhusu uagizaji holela wa sukari kama zamani. Mambo yanafanywa na Magufuli ni ya msingi (na ndiyo hayo yamekuwa yakiliwa na upinzani miaka yote).
 
Kauli au matendo ya watu au vyama huwa na mapungufu ya hapa na pale. Watu au vyama vingine huyasema mapungufu hayo katika namna ya kukosoa. Sasa,hapa nchini,inamea tabia ya kuchukia kukosolewa.

Kukosoa ni kuweka sawa. Kwahiyo,kukosolewa ni kuwekwa sawa. Inapotokea mkosolewaji au wakosolewaji hawapendi wala kutaka kukosolewa,wanataka nini hasa?

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
hali ya maisha imekuwa ngumu kupita maelezo
 
Ukiona hivyo ujue wanataka sifa ambazo hawana,tatizo hata wengine wamelibeba hivyo hivyo!Inakuaje uruhusu kusifia ila kukosoa mwiko?????
Ujinga una gharama kubwa katika maisha ya taifa. Kosa la kjinga lililofanywa na UKAWA katika uchaguzi wa mgombea wake katika uchaguzi uliomleta Mhe. wa sasa, unatunyima baadhi yetu uhuru wa kuchangia na kukosoa serikali hii. Itoshe kusema makosa ya serikali hii yatakuwa makubwa kuliko yaliyowahi kufanywa na awamu zote zilizotangulia.
 
Tatizo la walimu wa science wao wanajionaga vichwa hawashindwi kitu, hukumbuki zamani wakati wanafundisha hesabu hamsikilizi mwanafunzi hata kama njia aliyokariri siyo, mwanafunzi ukimweleza anakwambia yeye ndio mwalimu na anajua! Hili tatizo ni la zamani hatuwezi kulirekebisha labda tuanze kulirekebisha kwa Watoto wetu.
 
Back
Top Bottom