Swali la fikirishi; Nini kilimsukuma Mwal Nyerere kuruhusu vyama vingi?

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Kwa mujibu wa GLOBAL POWER TREND ni vigumu mtu kukaa katika cheo muda mrefu karne ya 21 kuliko miaka ya 70,80. Ndio maana madikteta ni wachache leo kuliko miaka ya nyuma na waliobaki Wanasiku chache tu watatoka. Kuzuia Kuondoka katika cheo au mamlaka ambayo unapwaya karne hii ni sawa na Kudeki bahari ya hindi.(ukweli huu CCM walipaswa kuujua 1992 sio leo)

Nini kilimsukuma JK Nyerere kuruhusu vyama vingi bila kuwapa semina na kuwaandaa kihisia na saikolojia CCM kuwa kuna kupoteza UMEYA,URAIS na hata Kutokuwepo kabisa. Kama walimuelewa iweje wanahofu na kuwa waoga sana hata nafasi ndogo tu? Kama walimuelewa Nyerere kama sisi wananchi tulivyomuelewa,
Hawa wanaoleta haya si wale waliotusababishia Rasilimali zetu kuwa kitanzi na laana kwa mtanzania, Kuwalindia watoto na wajukuu wao yale waliochuma isivyo halali?

nabaki kujiuliza kila leo, Nini kilimsukuma Nyerere Kuruhusu vyama vingi?
 
Kwa mujibu wa GLOBAL POWER TREND ni vigumu mtu kukaa katika cheo muda mrefu karne ya 21 kuliko miaka ya 70,80. Ndio maana madikteta ni wachache leo kuliko miaka ya nyuma na waliobaki Wanasiku chache tu watatoka. Kuzua Kuondoka katika cheo au mamlaka ambayo unapwaya karne hii ni sawa na Kudeki bahari ya hindi.(ukweli huu CCM walipaswa kuujua 1992 sio leo)

Nini kilimsukuma JK Nyerere kuruhusu vyama vingi bila kuwapa semina na kuwaandaa kihisia na saikolojia CCM kuwa kuna kupoteza UMEYA,URAIS na hata Kutokuwepo kabisa. Kama walimuelewa iweje wanahofu na kuwa waoga sana hata nafasi ndogo tu? Kama walimuelewa Nyerere kama sisi wananchi tulivyomuelewa,
Hawa wanaoleta haya si wale waliotusababishia Rasilimali zetu kuwa kitanzi na laana kwa mtanzania, Kuwalindia watoto na wajukuu wao yale waliochuma isivyo halali?

nabaki kujiuliza kila leo, Nini kilimsukuma Nyerere Kuruhusu vyama vingi?

Kwa sababu alikuwa hatawali yeye, angekuwa yeye ndiye mtawala kamwe usingeona akijenga hoja kuvitaka!
 
Haki ya watu kujumuika kwa malengo ya kisiasa tayari lilikuwa ni takwa la kikatiba baada ya Tangazo la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuingizwa katika katiba ya JMT mwaka 1984. Kuhusu uchaguzi wa meya Dar, kinachofanyika ni "abuse of authority" unaofanywa na serikali ya Magufuli ambayo haiheshimu demokrasia wala haki za raia.
 
Mwalimu Nyerere alikuwa visionary, alitazama mbali. Aligundua hasara ambazo bara la Afrika linakutana nazo kwa kutegemea mfumo wa chama kimoja. Aliweza kuziona hasara za Afrika kumezwa na mfumo wa "ndio mzee", aligundua umuhimu wa bara hili (Tanzania ikiwemo), kupata maendeleo kupitia akili nyingi zenye mawazo tofauti lakini mwisho wa siku zikiwa na lengo moja la kupigania ustawi wa nchi. Mwalimu Nyerere alikosakosa kupinduliwa miaka ile ya 80 ya mwanzoni, na ni kwa sababu tu usalama wa taifa ulikuwa makini, juhudi za kuipindua serikali yake zikashindwa.

Mwalimu Nyerere alipenda sana CCM ipate upinzani makini, lakini kila kitu kina muda wake. Nyakati zile za miaka ya 90, tulikuwa bado hatujaiva kama ambavyo kwa sasa tulivyoiva kwenye siasa za vyama vingi. Na watanzania wameelimishwa sana kwenye masuala ya haki zao.

Mwalimu Nyerere alijua mengi kuhusiana na rasilimali zetu na jinsi ambavyo zinaweza kugeuka kuwa laana kwa taifa badala ya kuwa baraka, kwa kuufahamu ukweli huo alijua kuwa migongano ya hoja ndani ya vyama vingi, ingeweza kuipatia nchi yetu aina ya uongozi ulio na uzalendo kwa kila tulichonacho. Waafrika tulizoea mfumo wa uchifu, kwa maana ya amri inayotawala kuwa ni moja tu, kwa maana ya kauli ya mkuu haipingwi, lakini vyama vingi havikwepeki kwa sababu ya uwepo wa upande unaoutazama mwingine kwa nia ya kuhakikisha kilicho cha wote hakibakii kuwa ni cha wachache peke yao.
 
Alifikiri pengine vyama pinzani vitakua tofauti na chama tawala watakua na uzalendo wa kweli wenye kupenda nchi yao oooh kumbe mzee alijidanganya kabisa hakuna tofauti hata kidogo bora zimwi likujualo tu.
 
Jiulize kwanza kwa nini alivifuta 1965?
Uamuzi wa Dunia nzima hakuwa na jinsi kukubali au kukataa.
Hakuna Taifa hata moja linalofata siasa ya Soko huria ikabaki na mfumo wa Chama kimoja.
Hata ukisoma Azimio la Arusha between line unaona kabisa isingeweza ku practise mfumo wa Vyama vingi huku ukitumia sera za Azimio la Arusha ambalo msingi wake Mkuu ni Ujamaa uliokwisha kufa.
 
Mwalimu Nyerere alikuwa visionary, alitazama mbali. Aligundua hasara ambazo bara la Afrika linakutana nazo kwa kutegemea mfumo wa chama kimoja. Aliweza kuziona hasara za Afrika kumezwa na mfumo wa "ndio mzee", aligundua umuhimu wa bara hili (Tanzania ikiwemo), kupata maendeleo kupitia akili nyingi zenye mawazo tofauti lakini mwisho wa siku zikiwa na lengo moja la kupigania ustawi wa nchi. Mwalimu Nyerere alikosakosa kupinduliwa miaka ile ya 80 ya mwanzoni, na ni kwa sababu tu usalama wa taifa ulikuwa makini, juhudi za kuipindua serikali yake zikashindwa.

Mwalimu Nyerere alipenda sana CCM ipate upinzani makini, lakini kila kitu kina muda wake. Nyakati zile za miaka ya 90, tulikuwa bado hatujaiva kama ambavyo kwa sasa tulivyoiva kwenye siasa za vyama vingi. Na watanzania wameelimishwa sana kwenye masuala ya haki zao.

Mwalimu Nyerere alijua mengi kuhusiana na rasilimali zetu na jinsi ambavyo zinaweza kugeuka kuwa laana kwa taifa badala ya kuwa baraka, kwa kuufahamu ukweli huo alijua kuwa migongano ya hoja ndani ya vyama vingi, ingeweza kuipatia nchi yetu aina ya uongozi ulio na uzalendo kwa kila tulichonacho. Waafrika tulizoea mfumo wa uchifu, kwa maana ya amri inayotawala kuwa ni moja tu, kwa maana ya kauli ya mkuu haipingwi, lakini vyama vingi havikwepeki kwa sababu ya uwepo wa upande unaoutazama mwingine kwa nia ya kuhakikisha kilicho cha wote hakibakii kuwa ni cha wachache peke yao.
Hii naona kama ilikuwa ni vision nzuri lakin with pre-mature move.
kutoka chama kimoja kwenda vingi, ilihitaji transition period ya kureview kila kitu ili mambo yote yawe sawa. huwezi kubadili jina la kitabu alafu contents zikabaki vilevile huku ukikiita hiki ni kitabu kipya.

Kosa kubwa kufanyika Mwaka 1992 ndio ulipaswa kuwa mwaka wa KUTUNGA KATIBA MPYA sio leo
 
Kuna idadi ndogo sana ya Watanzania wanaoelewa kinachoendelea na walau kujitambua lakini karibia 50% wanastahili kufugwa mazizini kama ng'ombe!
Hebu fikiria leo hii kila mtu anamsifia JPM eti 'anasafisha uozo' lakini Mh. Mnyika alivyosimama bungeni kwa uelewa wake na ujasiri ambao wengi tumeukosa na kutwambia kuwa udhaifu wa rais wakati huo (JK), udhaifu wa chama (ccm) ndio umetufikisha hapa haya majamaa yote yanayomsifia JPM ndio yalikuwa mstari wa mbele kumfukuza Mnyika bungeni.
Kwa picha hiyo utajua bado tuko mbali kiasi gani japokuwa reflection ya ujasiri na mawazo ya Mwalimu ipo katika jamii yeto (i.e. Mnyika na wengine)
 
Ninachoamini mimi ni kwamba Nyerere hakuwa tayari kuruhusu vyama vingi isipokuwa vyama vingi ni shinikizo la wazungu .Wazungu zamani walituamini sana katika matumizi ya fedha za misaada kutoka kwao wakiamini kwamba kwakuwa tumetoka katika ukoloni hivo tutaweza kusimamia rasilimali na fedha za misaada lakini badala yake uzalendo ukapotea kwa viongozi na ndipo wazungu kuona kwamba ili waweze kudhibiti fedha zao n lazima wahakikishe kunakuwa na upinzani ili kufichua uozo wa serikali iliyopo madarakani .Na hili kwa kiasi Fulani limesaidia sana wananchi kupitia vyama vya upinzani kujua madudu mengi ambapo nina hakika kama tungekuwa na chama kimoja haya ya ufisadi isingekuwa rahisi kuyajua.
Hivo nyerere kama nyerere sina hakika iwapo ilikuwa n matakwa yake kukubali vyama vingi
 
Back
Top Bottom