Swali kwa wizara ya elimu

Swali kwa wizara ya elimu

reg edit

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2012
Posts
403
Reaction score
506
Wasalam,
Hili swali limekua nikijiuliza miaka mingi mno lakini sipati majibu haswa ni nini walidhamiria wizara ya elimu.

Hivi kwa wanafunzi wanaosoma shule zenye michepuo ya ufundi kama Ifunda tech, Iyunga tech, Tanga tech, Mtwara tech n.k au shule zenye michepuo ya upishi, ushoni n.k.. Inakuaje mtoto anamaliza miaka minne hapewi cheti cha huo ufundi/stadi aliyosomea ili kama atashindwa kwenda form 5 au akiamua asiende form 5 basi aweze kwenda kuomba kuajiriwa kwa kutumia hivyo vyeti?

Maana haiingii akilini mtoto asome veta miaka miwili halafu anapewa cheti kwenda kuajiriwa lakini huyu aliyesomea miaka minne (o level) kwa masomo hayo hayo ya ufundi lakini hapewi cheti. Anapewa cheti cha jumla tu kuonyesha amepata division ngapi ambacho waajiri hawakiangalii kama ni cheti cha mtu ambaye amekuwa fundi kamili

Ushauri kwa wizara, kwanini hawa vijana wasilazimishwe wafanye mitihani kama wanayofanya veta kipindi kile cha mitihani ya form 4 ili atakapofaulu anapewa cheti kama cha veta ili kumuepushia kwenda tena veta kusoma miaka miwili wakati alishasoma hivyo vitu kwa miaka minne?

Lakini pia akipewa hiki cheti cha veta, mathalani huko mbele ya safari mambo yakamuendea kombo basi anaweza kuja kukitumia kuombea ajira.


Naomba kuwakilisha
 
Wanafanya mitihani mbona, na vyeti pia wanapewa mkuu. Fanya research..
 
Back
Top Bottom