Swali kwa wataalamu wa Mobile application

freeboy

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
242
191
Wakuu salamu kwenu,

Nikiwa kama mdau wa ICT napenda kufahamu kitu kimoja kuhusu mobile application.

Kwa mtu ama kikundi cha watu wanaomiliki mobile apps zao na kuziupload mfano google store na watu wakadownload bure kwa mfano apps za magame, chatting apps km vile whatapps.

Swali: Je hawa watu wanafaidika vip na apps zao ikiwa hakuna anayelipia ni bure kudownload

msada wadau hii kitu inanichanganya sana tuelimishane.

Asante
 
Tuseme kama vile adsense wanapewa matangazo na mtumiaji kama pengine wewe unapo click lile tangazo kwenye app yake then anaingiza hela
 
Shukran mkuu mickey nimekupata kidogo kumbe muhimu kujitangaza mwenyewe kupata hao wawekaji matangazo.
 
kuna msemo maarufu tu ukiona ni bure ujue bidhaa ni wewe, wanapata hela kupitia matangazo, wanachukua information zako kama location, namba za simu, msg nk na kuziuza wengine wanaiba hadi data kama picha na video
 
Wengi hawapati faida yoyote. Kama WhatsApp hawajawahi kupata faida, gharama za eundeshaji ni kubwa kuliko walichokuwa wanaingiza na fee yao ya $1 kwa mwaka ambayo wameifuta kabisa.

Pia hawana matangazo na wamesema kamwe hawatakua nayo na data za watumiaji hawauzi. Hawa wameshanunuliwa na facebook so hawana presha.

Instagram wana matangazo usipoangalia vizuri hauwezi kuyatambua, yapo kama post za watu. Pia wamenunuliwa na Facebook, hawakuingiza faida kabla ya kuuzwa.

Facebook matangazo yapo wazi kabisa.
 
Matangazo, kuuza info za watu na donations from donors. Kama Wikipedia inaingiza hela za kujiendesha kupitia donors.
 
kuna msemo maarufu tu ukiona ni bure ujue bidhaa ni wewe, wanapata hela kupitia matangazo, wanachukua information zako kama location, namba za simu, msg nk na kuziuza wengine wanaiba hadi data kama picha na video

Khaaaa kumbe ndio hivyo nimekuelewa sana mkuu Chief-Mkwawa
 
Hili la matangazo na donations from donors limekaa vizuri sana ila hili la kuuza info za watu kweli wanazingua somehow mkuu Bufa
 
Back
Top Bottom