Swali kwa wapendanao

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,016
1,501
Habari wakuu?

Natumai mpo safi baada ya mapunziko mafupi ya week-end, na mpo tayari kuendelea kupeana maarifa au kubadilishana mawazo na kupeana mbinu za kukabiliana na changamoto za kila uchao katika maisha.

Kuna hili suala ambalo mara nyingi tunalizungumzia pasi kulitilia maana ingawaje ni jambo muhimu sana linaloweza kumtokea yeyote kati yetu na kumsababishia matatizo makubwa baina yake na mwenza wake na hata uhusiano kufa kabisa na kusambaratisha familia ambayo iliishi kwa amani na upendo wa hali ya juu.

Naongelea "FUMANIZI" Hivi ikitokea umefumaniwa na mwenza wako, "kipenzi chako" ni Utetezi gani mzuri na wa busara unaoweza kuutoa kwa mwenza wako na kunusuru uhusiano wenu!?

Binafsi sina maelezo zaidi ya "SAMAHANI; eee! Ndio, nisamehe mpenzi, mke wangu najua nimekukosea. Samahani sana. Haya nanyie wenzangu mnatokajetokaje hapo!?
 
Mke akinifumania, kwa jinsi nilivyo kauzu ataniomba yeye msamaha na itachukua siku kadhaa kumsamehe

Ila yeye nikimfuma, nitaenda ukweni kuomba msamaha kua sikukusudia kufanya vile kwa mwanao

It's Scars
 
Personally sitaki kujitaftia matatizo nilishawahi kumkuta ex na msichana getto yaliyotokea baada ya hapo sitaki kukumbuka since then siendi kwa mwanaume kabla sijampigia simu anipe go ahead ya kwenda kwake otherwise nakituliza natafuta kitu kingine cha kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke akinifumania, kwa jinsi nilivyo kauzu ataniomba yeye msamaha na itachukua siku kadhaa kumsamehe

Ila yeye nikimfuma, nitaenda ukweni kuomba msamaha kua sikukusudia kufanya vile kwa mwanao

It's Scars
Aisee, ubinadam umekushinda kabisa, MKUU!!?
 
Personally sitaki kujitaftia matatizo nilishawahi kumkuta ex na msichana getto yaliyotokea baada ya hapo sitaki kukumbuka since then siendi kwa mwanaume kabla sijampigia simu anipe go ahead ya kwenda kwake otherwise nakituliza natafuta kitu kingine cha kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana, ila vipi ukinaswa wewe ndio unagawa pipi ya watu, utajiteteaje!?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom