The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,320
- 117,654
Wanawake wanatupiwa lawama wakati wote kwa kuwa ule mshahara wa kuvunja amri ya sita unaonekana physically kwao kwa ile mimba.Imetokea mara nyingi uchumba umevunjika kwa msukumo wa familia au marafiki eti kwa vile binti alikuwa na historia ya kuwa na wanaume wengi wakati huohuo huyo mwanaume siyo clean kihivyo.
Mfano mzuri upo kwa madenti wa kike,huwa wanafukuzwa shuleni na hata nyumbani wakipata mimba na wakati mwanaume aliyempa mimba ametulia tu na ndio kwanza anapongezwa eti kidume cha mbegu.mfano mwingine ni pale inapotokea mwanaume amepata safari ya kimasomo nje ,akifika huko anabadilisha wanawake atakavyo,na itokee mkewe akajaribu hata mara moja na kupanda mimba utasikia kasheshe yake.
Na hata hiyo bikra zamani katika makabila walikuwa wanaangalia kwa binti tu na sio mwanaume.Yani wanakuwekea mashangazi hiyo siku ya kuolewa wakukague usipokutwa nayo ni fedheha kwa familia yako yote na mwanaume hawamuangalii kama na yeye ni bikra.
kwa hayo huoni kuwa hakuna balance hapo katika hilo swala?Kama wanaume wangekuwa wanabeba mimba nao ingekuwa rahisi kuwakamata wasikane pale wanapoharibu.
bikira ya kiume inachunguliwa vipi?