Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of Convenience?.-Ni Swali Tuu!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Huu ndio mwaka wa uchaguzi, matumaini yote ya upinzani nchi Tanzania kuweza kushinda Uchaguzi Mkuu na kuingia Ikulu yetu ya Magogoni ni kupitia ushirikiano wa vyama kuunda umoja wenye nguvu kwa kusimamisha mgombea mmoja wa upinzani anayekubalika na kushindana mgombea wa CCM, kupitia huu ushirikiano wa vyama unaoitwa UKAWA, ulioasisiwa na Mchakato wa Katiba Mpya. Swali ni je UKAWA is it for real? au ulikuwa ni ushirikiano wa just a marriage of convenience za katiba tuu, katiba mpya ikiishapatikana, ile convenience itakuwa imekwisha hivyo sasa kila mtu, atashika lwake kwa kuianza safari ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 huku kila mmoja kivyake vyake huku ameshika njia yake?!.

Kwa wajuvi wa mashirikiano yoyote, mashirikiano yoyote ili yalete manufaa ni lazima yajengwe kwenye misingi imara na sio kwa misingi ya conveniences ili hata hizo conveniences zikiisha, mashirikiano yaendelee.


Mfano mzuri ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, uliingiwa kwa security conveniences za kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, lakini sasa muungano wetu unaendelea bila uwepo wa any security threats kwa Zanzibar.

Sasa kwa wanaojua misingi ya mashirikiano kisiasa, jee mashirikiano haya ya UKAWA yamefuata misingi hiyo?!.

Kajiswali haka ni kufuatia mmoja wa washirika wa UKAWA, chama cha CUF, tayari ni mke wa mtu huko upande wa pili wa Zanzibar, ambapo CUF imefunga ndoa na CCM iitwayo SUK, (Serikali ya Umoja wa Kitaifa), ndani ya mfumo huo wa SUK, mwenye kura nyingi ndie mume, na anayefuatia ndiye mke, hivyo kwa serikali ya SUK ya Zanzibar , CCM ndiye mume na CUF ni kama mke imeolewa na CCM!. Mawaziri wa CUF waliondani ya serikali ya SUK, wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM!, hivyo kwa muktadha wa bandiko hili, CUF ni kama mke wa mtu kule Zanzibar!.

The real life scenario iko hivi:

Ndani ya mashirikiano haya mapya ya UKAWA, mmoja wa washirika wake CUF tayari ni mke wa mtu kwenye ndoa nyingine na CCM Zanzibar ambayo mumewe, CCM ndiye mpangaji rasmi wa ile ile nyumba yao ya ndoa, Ikulu ya Zanzibar.

CUF kuingia kwenye mashirikiano ya UKAWA huku bara ni kama mwanamke kuingia kwenye mahusiano nje ya ndoa kila anaposafiri nje ya Zanzibar, huku tayari ni mke wa mtu!.

Ndoa ya namna hiyo inaweza tuu kudumu iwapo mwanamke huyo na mahusiano hayo mapya, ataendelea kuishi huko huko alikotorokea, nikimaanisha, huu ushirikiano wa CUF ndani ya UKAWA utawezekana tuu kwa CUF kwenye uchaguzi wa JMT kwa huku bara tuu, lakini kwa Zanzibar CUF ni mwanandoa halali ndani ya SUK na uchaguzi wa 2015 CUF ana fursa ya kugeuka mume na CCM kugeuka mke.

Nguvu ya CUF ni Zanzibar, hivyo kama CUF ambaye ni mke wa CCM Zanzibar ndani ya ndoa ya SUK, lakini akivuka kuja Bara na anaingia kwenye mahusiano nje ya ndoa ya UKAWA ambayo CUF na mshirika wake huyu mpya wa UKAWA anatagemea akishinda Zanzibar ni lazima aendelee kuishi na CCM kule Zanzibar, na CUF huyu huyu kuja kuishi mume mpya, huku Bara, holi litawezekana vipi kwa kule Zanzibar iwapo CUF itashinda uchaguzi wa Zanzibar na kuishi kwenye ile ile nyumba yake ya ndoa ya mke mmoja mume mmoja wa CUF na CCM ndani ya Ikulu ya Zanzibar halafu huku bara iwe ni CUF na Ukawa?.

Mke huyu CUF akiwa upande mmoja kule Zanzibar ni mke mwaminifu kwenye ndoa yake ya SUK lakini akivuka upande wa pili, huku Bara, yuko kwenye ndoa nyingine ya UKAWA, huku sio kuchepuka?.

Tabia za wanandoa kuchepuka kidogo nje ya ndoa kwa lengo la kubadili mboga ni jambo la kawaida, lakini kitendo cha mke wa mtu mwenye ndoa yake kujulikana wazi kuwa anachepuka kwa kwenda nje ya ndoa wazi wazi kila awapo safarini bara, huku kutahesabika ni kumuhujumu mumewe halisi CCM na kuisaliti ndoa!. Kitendo cha mke wa mtu kutoka na mwanaume mwingine waziwazi huku tayari ni mke wa mtu, sio jamba la kawaida linanoweza kuvumilika hivyo huyu mke wa mtu CUF ndani ya UKAWA, is CUF there for real ndani ya UKAWA huku ni mke wa mtu ndani ya SUK?.

Nikiifuatilia kwa karibu hii ndoa ya CCM na CUF kule Zanzibar, najiuliza, jee ndoa hiyo inaweza kuendelea kudumu hata baada ya mumewe CCM kugundua mkewe CUF, ni mke mwaminifu Zanzibar tuu ndani ya SUK, lakini akivuka tuu bahari, akiwa kule upande wa pili wa Bara, huchepuka nje ya ndoa na mwanaume mwingine UKAWA ambaye sasa ndiye anayepanga nae kuja kumpindua yeye CCM na kuishi na UKAWA ndani ya nyumba ile ile yao ya ndoa ya Ikulu ya Zanzibar?!. CCM itakubali?. Hii maana yake matokeo ya uchaguzi Zanzibar, kuna kila dalili za CUF kushinda lakini... ( hili naomba nisilimalizie maana mimi ndie yule mtangazaji aliyetangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar ile 1995, hivyo nisije kutangaza kitakachotokea kwenye matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa 2015 nikaja kunyooshewa kidole tena kama ile ya 1995).

Kwa vile anayechagua mke ni mwanaume, anayeandika barua ya posa ni mwanaume, anayelipa mahari ni mwanamume, na anayeoa ni mwanaume, kikawaida mke akileta shida ndani ya ndoa, mke huachika na na hata kama aliyeleta shida ndani ya ndoa ni mwanaume, mke huomba talaka, na akipewa talaka yake, bado jamii itamuhesabu huyo mke kuwa ameachika!, hata kama kiukweli ni mke ndie amemuacha mume!. Kupitia huu ushirikiano mpya wa UKAWA, Luna mke wa mtu anakwenda kuachika 2015!.

Baada ya mke kuachika, mke ndie hutoka ndani ya nyumba ya ndoa na kurejea kwao, hivyo kumpa fursa mume au kumrejelea mkewe, au kuoa mwanamke mwingine na ndoa kuendelea, lakini kwa mwana ndoa huyu CUF msharika wa UKAWA, yaani mke huyu, hana mpango wa kutoka ndani ya nyumba yao ya ndoa, Ikulu ya Zanzibar bali CUF ndio imepanga kumfurusha mumewe wa ndoa CCM ndani ya ndoa yao ya SUK kwa CUF ndie ageuke mume na CCM ageuke mke na kuendelea kuishi ndani ya nyumba yao ya ndoa, Ikulu ya Zanzibar kwa hoja kuwa hata huyo mumewe wa sasa CCM, sio mmiliki wa hiyo nyumba yao ya ndoa ya Ikulu ya Zanzibar bali ni mpangaji tuu!, aliyepangishwa na umma wa Wazanzibari ambao ndio wenye nyumba!. Kwa mtazamo wako, jee mumewe huyu CCM atakubali kugeuzwa mke baada ya uchaguzi wa 2015?. Jee atajikalia tuu kimya kutazama na kushuhudia haya yamfike?!.

Jee mumewe CCM aendelee tuu na ndoa ya CUF ndani ya SUK kwa kujikalia kimya as if nothing has happened kwa vile tuu anampenda sana mkewe?, lakini huku akiumia moyoni?!.

Swali la msingi la kujiuliza pale unapobaini mkeo anachepuka nje ni jee huyo mke wako anayechepuka huko nje, ni anachepuka kubadili tuu mboga , ama ana nia ya dhati ya kulitunza penzi la jipya la mchepuko wake mpya wa UKAWA, hivyo wewe mume kuamua kumpa option ya kuchagua moja tuu, ama kuachana na ndoa yake ya kwanza na kufunga ndoa ya pili na huo mchepuko wake wa upande wa pili, au aamue kuachana na huo mchepuko na kutulia ndani ya yake?.

Au kwa sababu mumewe CCM anampenda sana mkewe CUF ndani ya ndoa yao ya SUK kwa mustakabali wa amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar, na anamtegemea sana mkewe huyo kwa amani na utulivu wa nyumba yao, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa mume CCM amejinyamazia tuu licha ya kuyabaini mahusiano ya nje ya mkewe CUF, kwasababu sio mahusiano ya siri, ni mahusiano ya wazi na yanajulikana bayana, hivyo kwa mume CCM kuhofia kutupwa nje, mtaani, akawa hana pa kuushi, hivyo anaamua bora kujinyamazia tuu kimya, ndani ya ndoa ya SUK huku akimlaumu huyu mke wa mtu kuziendeleza zile za "huku wataka na kule wataka!", lakini mume CCM anakijua atakachomfanya huyu mke mchepukaji come October 2015, ndio maana nawauliza waungwana humu, is this for real? hii ni kweli, na itadumu kwa muda gani?, nauliza tuu?.

Swali hili linafuatia washirika wawili wakuu wa UKAWA, CHADEMA na CUF, kila mmoja kukumbwa na tatizo la "superiority complex" kwa kujiona yeye ni bora zaidi, hivyo kutaka kujimegea pande kubwa!. Conveniences hizi zitafikia peak wakati wa uteuzi wa mgombea urais JMT. Kwa Zanzibar, CUF tayari wakiwa na wagombea wao wa kudumu anayekubalika kwa upande wa Zanzibar, hakuna ubishi kuhusu kukubalika kwa Maalim Seif, jee kwa upande wa bara, mgombea wa kudumu wa CUF Prof Lipumba ambaye hakujawahi kukubalika, atakubali kujishusha na kuruhusu mgombea wa ushindi anayekubalika ndie aibebe UKAWA?. Chadema nao wanaye mgombea wao ambao wanaamini alishinda ila akapokwa ushindi, kwao huu ni muda wa kumalizia alipo ishia!, jee mafahali hawa wawili wanaweza kuishi zizi moja la UKAWA?.

UKAWA wakiweza kulimaliza hili la uteuzi wa mgombea urais 'wa JMT salama, then angalau kutakuwa na matumaini ya mabadiliko!, lakini kwa ubinafsi wa viongozi wa upinzani, nina mashaka kama hili litapita salama, hivyo wale wote wenye matumaini na upinzani kuingia ikulu October, keep high hopes for best, but get prepared for the worst, iwapo watashindwa kumpata mgombea muafaka wa kuwaletea ushindi, 2015 ni CCM tena!.

Pasco.
 
"kwa sababu wenzetu wameamua na sisi tunashirikiana nao basi hatuwezi kuwapinga juu ya hilo. . . hivyo tunawaunga mkono". . . . . . . .majibu kama hayo yanakuonesha nini Pasco??!!!
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Huu ndio mwaka wa uchaguzi, matumaini yote ya upinzani kuingia Ikulu yetu ya Magogoni ni kupitia ushirikiano wa vyama unaoitwa UKAWA, ulioasisiwa na Mchakato wa Katba Mpya. Swali ni Jee UKAWA is it for real, au ulikuwa ni ushirikiano wa conveniences za katiba tuu, katiba mpya ikiishapatikana, ile convenience itakuwa imekwisha hivyo sasa kila mtu, ataanza safari kushika njia yake?!. Kwa wanaojua misingi ya mashirikiano kisiasa, jee mashirikiano haya ya UKAWA yamefuata misingi hiyo?!.

Nina haka kajiswali kadogo kwenu, Swali hili ni kufuatia mmoja wa washirika wa UKAWA tayari ni mke wa mtu huko upaqnde wa pili!.

The real life scenario iko hivi: Kuna mke wa mtu, mke huyu akiwa upande mmoja ni mke mwaminifu kwenye ndoa yake lakini akivuka upande wa pili, anachepuka na kwenda nje ya ndoa!.Nfuatilia kwa karibu ile ndoa yao kule idaweza kudumu hata baada ya mumewe kugundua mkewe akiwa kule upande wa pili huchepuka nje ya ndoa!, jee aendelee tuu na ndoa kwa kujikalia kimya as if nothing happened kwa vile tuu anampenda sana mkewe, huku akiumia moyoni?!. Na jee huyo mke anayechupuka huku, ana nia ya dhati ya kulitunza penzi la mchepuko kwa kuamua moja kuachana na ndoa yake na kufunga ndoa ya kweli na huo mchepuko wake wa upande wa pili?!. Au kwa sababu mumewe amejinyamazia tuu licha ya mahusiano yake haya mapya kujulikana bayana, hivyo huyu mke wa mtu ataziendeleza zile za "huku wataka na kule wataka! is this for real?!, nauliza tuu?!.

Pasco.
Hivi Katiba ya Zanzibar iliyoanzisha SUK ilikuwa ni ya miaka mitano tu au haikuwa na kikomo? Kama si ya miaka mitano ina maana baada ya Uchaguzi SUK ipo pale pale. Huku uko SUK huku UKAWA!
SUK ipo kisheria, UKAWA ni mchepuko.
 
Kwani we.w.e unawezaje kumudu mabwana za.ko wawili?
Ndoa ya mume w.a.ko White Head na mchepuko Presidaa MM?
Huoni kuwa huyo mshirika wa UKAWA atakuwa k.akuiga?
 
"kwa sababu wenzetu wameamua na sisi tunashirikiana nao basi hatuwezi kuwapinga juu ya hilo. . . hivyo tunawaunga mkono". . . . . . . .majibu kama hayo yanakuonesha nini Pasco??!!!
Mkuu unakumbuka siku JK anahutubia Bunge la Katiba, Maalim Seff alikuwepo jukwaa kuu akimuunga mkono mkuu wake?
 
Sheria gani inayokataza vyama kuungana wakaita jina moja. Kinachosajiliwa ni UKAWA, ni muungano huu wa kupiga mande chama kimoja kwa kushirikiana kupanga matokeo ndio haukubaliwi. Subirini uchaguzi mtanambia ama kama kweli unayo hiyo sheria naomba utuwekee hapa.
.
Mkuu Mkandara, kwanza heshima mbele!, pili nakubaliana na wewe kwa asilimia 100% kuwa UKAWA ni kiini macho, ila sikubaliani na wewe kwa jinsi ulivyojenga hoja kuhusu huu ukiinimacho wa UKAWA, ukiini macho wa ukweli wa UKAWA, ni "UKAWA is un constituted " yaani it doesn't exist in reality bali ni wazo tuu, yaani it is an idea ya vyama kushirikiana kwa malengo maalum, ila in reality kitu kinachoitwa UKAWA, haki exist in reality hivyo ni kweli ni kiini macho tuu!.

Kwanza kama sikosei, mimi ni mmoja wa watabiri wa mwanzo kabisa wa kuzaliwa kwa UKAWA, nilisema hapa.
Vurugu Bungeni-"Blessing in Disguise!"
Kisha nikaja kuuliza kuhusu huu UKAWA
Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of Convenieces?!.
Maana ya kuwa un constituted maana yake UKAWA haija undwa, haipo kisheria, ila ipo kwenye mawazo ya watu, yaani wana ukawa, na tatizo kubwa kabisa la kutoundwa ni sheria zetu mbovu kandamizi!. Hili nimelipigia kelele sana humu kuwashauri wapinzani, badala ya kudeal na the real issues, wao wanaongozwa na matukio!.

Nilitolea mfano wapinzani siku zote wanaelewa the playing ground or the playing field ya the game of politics in Tanzania, is not level!, licha ya wapinzani kulijua hili, lakini kila uchaguzi huwa wana sign kukubaliana the rules of the game, na mwisho wa siku wanapigwa wanaishia kulia lia!.

Uchaguzi wa 2010, waliosaini rules of the game za NEC kwa Chadema ni Mbowe na Dr. Slaa, walipopigwa Dr Slaa akasusa kuyatambua matokeo, nikasema kama hapo mwanzo ulikubali kanuni za mchezo na ukapeleka timu uwanjani, ukipigwa, huwezi kukataa kuyatumbua matokeo!. Baada yakugundua the playing field is not level, dawa pekee ilikuwa ni kutokubali kwanza kusaini kanuni za mchezo hadi uwanja usawazishwe, na kama bado haujakaa sawa, kutopeleka timu uwanjani ili game lisichezwe hadi uwanja usawazishwe!. Tunaingia tena kwenye uchaguzi mwingine, timu ni zile zile, uwanja ule ule, wachezaji wale wale, refa yule yule na rules of the game zile zile, hivyo mtu anayeyajua haya bado akapeleka timu kwa kutegemea matokeo tofauti, huyo atakuwa ni kichaa!.

Niliwapongeza sana wapinzani walipopata fursa kwenda ikulu nikidhani sasa watapigania kusawazishwa kwa uwanja, kumbe wenzetu walikwenda kufakamia tuu juisi, chai na vitafunwa, as if all is well!. Adui mkubwa wa hiki kiini macho cha UKAWA ni sheria zetu kandamizi, ambazo CUF, NCCR na Chadema wanazikumbatia to their advantage, pale wanapopata fursa kuzitumia kwa kuchinjia!, ila unapofikia wakati wa wao kuchinjwa, kazi yao ni kulia lia tuu!. Huu mimi nauita ujinga!.

Katiba yetu ilitoa haki ya uhuru wa kila raia kushiriki kwenye kuunda serikali toka ya mitaa, kijiji, hadi serikali kuu unconditional!. NEC iliposema lazima adhaminiwe na chama cha siasa, mahakama kuu kupitia ile kesi ya Mtikila ilisema sharti hilo ni unconstitutional!. Serikali ukakimbilia kuibadili katiba kifungu hicho batili kikaingizwa kwenye katiba, hivyo mahakama kuzimwa na supremacy ya katiba!.

Kiukweli mgombea akishadhaminiwa na chama kugombea, mwisho wa mkataba wake na chama chake ulipaswa kuishia hapo, akiisha chaguliwa, anachaguliwa na watu, hivyo sasa sio mtumishi tena wa chama chake bali sasa ni mtumishi wa watu!, chama chake kinapaswa kiwe na uwezo wa kumfukuza chama bila kuupoteza utumishi wa watu!. Sheria mbovu hii isingekuwepo, kungekuwepo na uwezekano wa mgombea wa Chadema kusimama urais na mgombea wa CUF kusimama mgombea mwenza. Kwa sheria jinsi ilivyo, kama ni kweli UKAWA wamedhamiria kusimamisha mgombea mmoja wa urais, then huyo mgombea na mweza lazima watoke chama kimoja, ndani ya UKAWA CHadema na CUF ndio ma giant, NCCR ni minority, CUF hawawezi kukubali kuwachagua Chadema kwa sababu hawa ni ma fundamentalists na wameishakuwa indoctrinated kwa muda mrefu hadi kuwaabudia Lipumba na Maalim, kinyume cha hapo hawatakubali!. Chadema nao ni mijitu ya vimba mibichwa na kujisikia wao ndio wao, asipoteuliwa Dr kuwa mgombea wa UKAWA, sina ukakika wale kina Mangi kule mgombani watampa kura Lipumba!, hivyo mgombea kutoka NCCR ndio atakuwa compromising candidate, sasa hao NCCR wana nani strong anayeweza kugombea akakubalika?!, unless kama watamchagua yule kibaraka!, na hicho ndicho kifo cha UKAWA kwa kupata kipigo cha mbwa mwizi!.

Ukawa hivi ulivyo ni kama mwanamume amempenda mwanamke akamtongoza na kumuahidi kumuoa, na hatimaye wakachukuana na kuishi pamoja kinyumba kwa dhana ya ndoa tuu lakini bado sii ndoa hadi ndoa kweli ifungwe!. Hivyo huu muungano wa UKAWA ni dhana tuu kwa lengo la kushirikiana lakini is not real!. Namna pekee ya kuifanya iwe real ni kwa sheria zetu kandamizi zifumuliwe, muungano na ushirikiano wa vyama uruhusiwe!.

Pasco.
 
PASCO: Inaonekana unapendelea sana story za kuolewa.

Je umeshaolewa kama ulivyoahidi hapa, baada ya mgombea wako KUKATWA na yeye akakubari KUKATIKA?!
 
Pasco katika ukawa mwenye dhamira ya kweli ni Lipumba peke yake, but Mbowe si mtu makini. Mbowe anamlazimisha Dr Slaa kugombea urais akielewa wazi Slaa anapungukiwa sifa lukuki kiimani,kindoa na kimaadili! Anachowaza Mbowe ni ruzuku tu!!
 
Wanabodi,

Huu ndio mwaka wa uchaguzi, matumaini yote ya upinzani kuingia Ikulu yetu ya Magogoni ni kupitia ushirikiano wa vyama unaoitwa UKAWA, ulioasisiwa na Mchakato wa Katba Mpya. Swali ni Jee UKAWA is it for real, au ulikuwa ni ushirikiano wa conveniences za katiba tuu, katiba mpya ikiishapatikana, ile convenience itakuwa imekwisha hivyo sasa kila mtu, ataanza safari kushika njia yake?!. Kwa wanaojua misingi ya mashirikiano kisiasa, jee mashirikiano haya ya UKAWA yamefuata misingi hiyo?!.

Swali hili linafuatia washirika wawili wakuu wa UKAWA, CHADEMA na CUF, kila mmoja kukumbwa na tatizo la 'superiority complex' kwa kujiona yeye ni bora zaidi, hivyo kutaka kujimegea pande kubwa!. Conveniences hizi zitafikia peak wakati wa uteuzi wa mgombea urais, CUF tayari wakiwa na mgombea wao wa kudumu!, jee atakubali kujishusha na kuruhusu mgombea wa ushindi ndie aibebe UKAWA?!. Chadema nao wanaye mgombea wao ambao wanaamini aliisha shinda ila akapokwa, kwao huu ni muda wa kumalizia alipo ishia!.

UKAWA wakiweza kulimaliza hili la uteuzi wa mgombea urais salama, then angalau kutakuwa na matumaini ya mabadiliko!, lakini kwa ubinafsi wa viongozi wa UKAWA, nina mashaka kama hili litapita salama, hivyo wale wote wenye matumaini na upinzani kuingia ikulu October, keep high hopes for best, but get prepared for the worst, iwapo watashindwa kumpata mgombea muafaka wa kuwaletea ushindi, 2015 ni CCM tena!.

Pasco.
Hili lilikuwa ni swali tuu, natumaini sasa karibia litapata majibu!.

Pasco
 
Kwenye hili la UKAWA, naamini very soon, mtashuhudia watu wakiachana na michepuko ya pembeni na kuzirejelea ndoa zao, ambapo mtawashuhudia watu waume wakiandamana na wakeze, au watu wake wakiandamana na waume zao!.

subirieni tuu, tarehe 25 sio mbali!.

Pasco
 
Kwenye hili la UKAWA, naamini very soon, mtashuhudia watu wakiachana na michepuko ya pembeni na kuzirejelea ndoa zao, ambapo mtawashuhudia watu waume wakiandamana na wakeze, au watu wake wakiandamana na waume zao!.

subirieni tuu, tarehe 25 sio mbali!.

Pasco

Bro Pasco kwanza pole. Pole sana kaka yangu maana umepigwa nyundo ya utosi hutaamka tena. Usalva ushapotea labda ukaroge sana kwenu Ibinzamata.

Pili kaka Pasco nikuulize tu, kwa mustakabali mwema wa Taifa letu, ungeitaka Ukawa ya namna gani?
 
Last edited by a moderator:
Bro Pasco kwanza pole. Pole sana kaka yangu maana umepigwa nyundo ya utosi hutaamka tena. Usalva ushapotea labda ukaroge sana kwenu Ibinzamata.

Pili kaka Pasco nikuulize tu, kwa mustakabali mwema wa Taifa letu, ungeitaka Ukawa ya namna gani?
Mkuu Mzito Kabwela, asante, hizi ndio siasa na lazima ukubali matokeo utake usitake!. Ila pia kiukweli, sijawahigi kuutamani U-Ualva kwa sababu niliondoka utumwani tangu mwaka 2002, hivyo siwezi tena kurejea utumwani!. Kutumwa ni kutumwa tuu, utumwe na yoyote hata kutumwa na rais ni kutumwa tuu, na yeyote anayetumwa ni mtumwa!.

Kiukweli nilipania CCM au imsimamishe 'jamaa yetu' na ikimkata nilitegemea 'jamaa yetu' ndie aibebe UKAWA tumwingize ikulu. He was the one and only hope kwa upinzani kuingia ikulu!. Lakini kwa vile CCM imetusimishia jembe, 'jamaa yangu' hahami tena!, na hakuna mgombea yoyote wa upinzani wa kushindana na jembe hili!, hivyo 2015 ni CCM tena!.

Pasco
 

Mkuu Mzito Kabwela, asante, hizi ndio siasa na lazima ukubali matokeo utake usitake!. Ila pia kiukweli, sijawahigi kuutamani U-Ualva kwa sababu niliondoka utumwani tangu mwaka 2002, hivyo siwezi tena kurejea utumwani!. Kutumwa ni kutumwa tuu, utume na yoyote hata kutumwa na rais ni kutumwa tuu, na yeyote anayetumwa ni mtumwa!.

Kiukweli nilipania CCM au imsimamishe 'jamaa yetu' na ikimkata nilitegemea 'jamaa yetu' ndie aibebe UKAWA tumwingize ikulu. He was the one and only hope kwa upinzani kuingia ikulu!. Lakini kwa vile CCM imetusimishia jembe, 'jamaa yangu' haami tena!, na hakuna mgombea yoyote wa upinzani wa kushindana na jembe hili!, hivyo 2015 ni CCM tena!.

Pasco
Mkuu Pasco, Mimi huwa napenda Ukweli maana Ukweli humweka mtu huru. Jamaa yako(Yetu?) alitarajiwa kujiunga na ACT. "Mahesabu" yamegoma maana yule rafiki yako ambaye ni top kwenye chama, mwenye madaraka kikatiba kupinga hata kilichoamriwa na mwenyekiti, hajatengeneza "shape" nzuri ya kukifanya chama kivutie kwa jamaa yako(yetu?) kuhamia.

Tuje kwenye UKAWA. Umeikosoa Ukawa kwa hoja nyingine nazikubali na nyingine sizikubali. Kama wewe ungetaka uwe kwenye team ya kuijenga Ukawa, ungependa kuiona Ukawa iliyo na shape/mwonekano/ inayoongozwaje? Kifupi ni Ukawa ya namna gani ambayo ingeitoa CCM leave alone uncontrolled/external factors zinazoibana Ukawa kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,
UKAWA wakiweza kulimaliza hili la uteuzi wa mgombea urais salama, then angalau kutakuwa na matumaini ya mabadiliko!, lakini kwa ubinafsi wa viongozi wa UKAWA, nina mashaka kama hili litapita salama, hivyo wale wote wenye matumaini na upinzani kuingia ikulu October, keep high hopes for best, but get prepared for the worst, iwapo watashindwa kumpata mgombea muafaka wa kuwaletea ushindi, 2015 ni CCM tena!.

Pasco.

Kuna taarifa ya dalili njema kuhusu hili ndani ya saa 24 zijazo!.
lets hope for the best!.
Pasco
 
Mkuu Pasco, Mimi huwa napenda Ukweli maana Ukweli humweka mtu huru. Jamaa yako(Yetu?) alitarajiwa kujiunga na ACT. "Mahesabu" yamegoma maana yule rafiki yako ambaye ni top kwenye chama, mwenye madaraka kikatiba kupinga hata kilichoamriwa na mwenyekiti, hajatengeneza "shape" nzuri ya kukifanya chama kivutie kwa jamaa yako(yetu?) kuhamia.

Tuje kwenye UKAWA. Umeikosoa Ukawa kwa hoja nyingine nazikubali na nyingine sizikubali. Kama wewe ungetaka uwe kwenye team ya kuijenga Ukawa, ungependa kuiona Ukawa iliyo na shape/mwonekano/ inayoongozwaje? Kifupi ni Ukawa ya namna gani ambayo ingeitoa CCM leave alone uncontrolled/external factors zinazoibana Ukawa kwa sasa.
Mkuu Mzito K., hii kitu sikuona ndio naiona leo!, you are right, ZZK is good but ACT bado sana!, hivyo 'jama yangu' ameukubali ukweli halisi, Chadema ndio mambo yote!, ndani ya saa 24 kutokea sasa, mambo yote yatakuwa hadharani!.

Kama ni kweli jamaa yangu, atajiunga Chadema, then ZZK na ACT yake watakuwa left with no options, au waipigie magoti UKAWA, ACT wawe integrated into UKAWA, or face distinction!, hawawezi kupata hata ujumbe wa nyumba kumi mbele ya Chadema imara!, vinginevyo Chadema itoe msamaha wa jumla bila masharti, Zitto na watu wake waivunje hiyo ACT yao, warejee nyumbani and fight as one!.

Jamaa akitia timu, ikulu ni ya Chadema kwa 99.9% sure!.

Pasco
 
Mkuu Mzito K., hii kitu sikuona ndio naiona leo!, you are right, ZZK is good but ACT bado sana!, hivyo 'jama yangu' ameukubali ukweli halisi, Chadema ndio mambo yote!, ndani ya saa 24 kutokea sasa, mambo yote yatakuwa hadharani!.

Kama ni kweli jamaa yangu, atajiunga Chadema, then ZZK na ACT yake watakuwa left with no options, au waipigie magoti UKAWA, ACT wawe integrated into UKAWA, or face distinction!, hawawezi kupata hata ujumbe wa nyumba kumi mbele ya Chadema imara!, vinginevyo Chadema itoe msamaha wa jumla bila masharti, Zitto na watu wake waivunje hiyo ACT yao, warejee nyumbani and fight as one!.

Jamaa akitia timu, ikulu ni ya Chadema kwa 99.9% sure!.

Pasco
Mkuu Pasco, najaribu kuwa mtulivu ili nipate kile unachomaanisha. Hapo kwenye red umetazama factor zipi?

Mimi naona Chadema tulijisahau mahali fulani.

Kwa katiba hii hii

Tume ya taifa ya Uchaguzi hii hii

Na kwa namna ambavyo chadema ili deal na jamaa (yetu?) yako kwa ku-cement ufisadi wake kwa raia, hapa yule dogo aliita "akiba ya maneno"

Kwa jinsi chama-dola kinavyo mkodolea mimacho

Suluhisho pekee labda kuikaribia japo kwa mbali hiyo 99.9% ni Jamaa yako kufunguka. Aeleze umma Richmond ni nani, ana rangi gani, aliingiaje nchini, nani alimkaribisha, na huwa wanafanya mawasiliano na nani kwa ishu za kitaifa, "mzigo" ulipokuwa unatoka nani alikuwa analamba nini. Hata kama wewe kaka Pasco ulikuwa unavuta kwa mkono wa kulia unaficha mfuko wa kushoto akutaje tuwajue. Kisha aombe radhi kwa kukaa na hiyo "siri" kwa muda mrefu then wana chadema tupime uthabiti wa kauli zake then tumpe go ahead.

Kiswahili swahili tu hiyo 99.9% itabidi utoe 98.9%
 
Ameshahama sasa.
Unasemaje juu ya hilo?


Mkuu Mzito Kabwela, asante, hizi ndio siasa na lazima ukubali matokeo utake usitake!. Ila pia kiukweli, sijawahigi kuutamani U-Ualva kwa sababu niliondoka utumwani tangu mwaka 2002, hivyo siwezi tena kurejea utumwani!. Kutumwa ni kutumwa tuu, utume na yoyote hata kutumwa na rais ni kutumwa tuu, na yeyote anayetumwa ni mtumwa!.

Kiukweli nilipania CCM au imsimamishe 'jamaa yetu' na ikimkata nilitegemea 'jamaa yetu' ndie aibebe UKAWA tumwingize ikulu. He was the one and only hope kwa upinzani kuingia ikulu!. Lakini kwa vile CCM imetusimishia jembe, 'jamaa yangu' haami tena!, na hakuna mgombea yoyote wa upinzani wa kushindana na jembe hili!, hivyo 2015 ni CCM tena!.

Pasco
 

Mkuu Mzito Kabwela,
...Lakini kwa vile CCM imetusimishia jembe, 'jamaa yangu' haami tena!, na hakuna mgombea yoyote wa upinzani wa kushindana na jembe hili!, hivyo 2015 ni CCM tena!.

Pasco

Wanabodi,

Huu ndio mwaka wa uchaguzi, matumaini yote ya upinzani kuingia Ikulu yetu ya Magogoni ni kupitia ushirikiano wa vyama unaoitwa UKAWA,
iwapo watashindwa kumpata mgombea muafaka wa kuwaletea ushindi, 2015 ni CCM tena!.

Pasco.

Kuna taarifa ya dalili njema kuhusu hili ndani ya saa 24 zijazo!.
lets hope for the best!.
Pasco

Mkuu Mzito K.,

Kama ni kweli jamaa yangu, atajiunga Chadema,

Jamaa akitia timu, ikulu ni ya Chadema kwa 99.9% sure!.

Pasco

Huyu ndiye Pasco wa jf
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom