jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,412
- 5,013
Albert msando alitukanwa sana hapa jukwaani kuwa ni msaliti kwa kumtetea zitto kabwe, je na sasa anapomtetea Mbowe je bado ni msalit?
Hai. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameingia matatani baada ya Mahakama ya Wilaya ya Hai kuona ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya kumshambulia mwangalizi wa ndani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Uamuzi huo ulitolewa jana na hakimu mfawidhi wa wilaya hiyo, Denis Mpelembwa mbele ya Mbowe, wakili wake, Issa Rajabu na mwendesha mashtaka, Inspekta Marwa Mwita.
Mpelembwa alisema mashahidi saba wa upande wa mashtaka wameishawishi mahakama kuwa siku hiyo kuna tafrani ambayo ilitokea na ambayo Mbowe
atatakiwa kutoa ufafanuzi wa kuhusika kwake.
Alisema ingawa upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Albert Msando na baadaye Rajabu, ulitoa hoja kuwa ushahidi wa Jamhuri uliacha mashimo mengi, yeye anaona Mbowe ana kesi ya kujibu.
Katika hoja zao (utetezi) wanaona ukiacha ushahidi wa Nassir Yamin, hakuna shahidi mwingine aliyethibitisha kushuhudia Nassir akipigwa, alisema akinukuu hoja za mawakili wa utetezi.
source: Mbowe matatani wilayani Hai