Nibozali
JF-Expert Member
- Oct 15, 2016
- 572
- 1,055
Kumekuwepo na hoja zisizo na mashiko ambazo zimekuwa zikitolewa na wanaccm wenzangu kwa kuwashambulia wapinzani pale wanapokuwa wanataka kuonana na Rais ili kujadiliana masuala yenye tija kwa taifa.
Moja wapo ni hili linahusishwa na vyakula. Wapo wanaowakejeli wapinzani kuwa nia yao ni kwenda kupata mlo, ( chai, juisi, chakula). Ifike hatua tuache kujidhalilisha kwa kwa kuwa na mawazo mfu huku tukifikiria kuwa chai/juisi ya ikulu ni tofauti na hizi zinazotumiwa na wengine huku uraiani. Juisi/chai ya ikulu haitoki mbinguni na wala haiandaliwi na vitu vingine nje ya matunda (juisi) Mani/maziwa ( kwa upande Wa chai)
Ningependekeza tuwe na hoja imara za kukabliana na vishindo kutoka upinzani. Kamwe hatuwezi kuupoteza upinzani kwa kuja na hoja za chai aka juisi ya ikulu wakati wapo watu wanaoishi maisha ya kifahari kuliko hata hayo ya ikulu.
Kama upinzani wana masuala muhimu ya kujadiliana na Raid waachwe na siyo kubezwa kwa maneno ya kanga.
Ni hayo tu wanaccm wenzangu