swali kwa Wakristo

Mfano mtu ameoa ana wake watano na wote kazaa nao, akaamua kuwa Mkristo hao wake zake inabidi awape taraka au? Maana si ndoa ya Kristo ni ya mke mmoja/
Atapata ubatizo na kuambiwa sheria za Kanisa maana kuna wakristu wana wake zaidi ya mmoja hadi sasa japo hairuhusiwi na kanisa
 
Hakuna sheria kwenye ukristo inayozuia mtu asioe wake wengi isipokuwa kwa Padri au askofu. Hayo mengine ni mapokeo tuu ya watu. Oa kama unauwezo hata wafike mia ni wewe tuu
4 Akawajibu, “Hamjasoma kwamba aliyewaumba tangu mwanzo ali waumba mume na mke .5 akawaambia, ‘Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake na aambatane na mkewe; na hao wawili wata kuwa mwili mmoja’?
Matayo 19:4-5
 
Ndoa ni mke na mume , popote pale sio wake na waume, lakini je kuna mahali popote mtu aruhusiwi kuoa zaidi ya mmoja
 
Nitoke nje ya mada kidogo..

Kama unaruhusiwa kuoa zaidi ya mmoja kwanini upewe limit kuwa nne ndio mwisho?

Si bora uoe tu idadi unayotaka as long as ni zaidi ya mmoja!
Kama umekubali kuwa mfuasi lazima uongozwe na maandiko ya kule ulipo, vinginevyo ujiamulie mambo yako
 
4 Akawajibu, “Hamjasoma kwamba aliyewaumba tangu mwanzo ali waumba mume na mke .5 akawaambia, ‘Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake na aambatane na mkewe; na hao wawili wata kuwa mwili mmoja’?
Matayo 19:4-5

Tokea lini maneno ya Yesu yalikuwa sheria Mkuu? Yesu alifundisha lakini hakuwahi toa sheria. Unajua tofauti ya mafundisho na sheria?
 
Tokea lini maneno ya Yesu yalikuwa sheria Mkuu? Yesu alifundisha lakini hakuwahi toa sheria. Unajua tofauti ya mafundisho na sheria?
Lakini pia..hilo neno halijasema kuwa ndoa ni ya mke mmoja tu..

Kimaudhui, Ipo tofauti kati ya "hao wawili kuwa mwili mmoja" na "ndoa ni ya mke mmoja tu"

Labda kwa tafsiri ya kifani ndy unaweza ona mfanano wake.
 
Ndio maana nikamwambia hakuna sheria inayomkataza mtu wa kawaida kama mimi au wewe kuoa au kutokuoa mwanamke mmoja au zaidi isipokuwa wachungaji.
 
Sijajua ninini hasa nia ya swali lako ila nitakujibu hivi,{jibu langu halipo kiimani hivyo tegemea kuwa na maswali mengi kichwani kama ulitegemea kubishana}.

Utakachofanya ni kuchagua mmoja ktk hao wanawake zako umuowe kwa ndoa kamili ya Kikristo kisha hao wengine utatakiwa kuwapa stahiki zao zote kasoro kuwaingilia kimwili tu,malazi,chakula kutunza watoto etc ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu kuolewa na mabwana wengine.ni simple tu japo siyo rahisi kwa akili za kibinadm kuhama kutoka kituo kinachoruhusu viburudisho vingi kwenda kituo kinachoruhusu kiburudisho kimoja.

Hisia zangu zinanituma kuwa unatafuta chokochoko zisizokuwa na maana.
 
Safari ya kiroho kimsingi kila mtu anayo yake kiupekee Sana.
Kosa kubwa kujaribu kukopi au kuwafanya watu wafanane katika safari au mapito ya kiroho.
Every body got unique spiritual path!
 
Unajihami nimeuliza tu mimi mwenyewe Mkristo ila kuna kitu kimenifanya niulize na swali nimeitoa kwenye wimbo wa malebo eti baada ya kuokoka kaacha wale wanawake wengi aliokuwa nao ana mmoja ndo nikawaza hili swali, na nikawaza kama unabaki na mmoja hao wengine inakuaje na ndo maana nikauliza.
Usiogope mtu kuuliza swali hata kama ana lengo la kudebate, watu wengi ubongo unadumaa kwakuogopa kudebate. Ukitaka umfunge mtu kiakili mwambie ni kosa kudebate basi umemmaliza.
 
Sasa hao wake wengine ataendela kushirikiana nao kimwili au lah! na kama akiendelea atakuwa anafanya zinaa au hapana na kama ni ndiyo si kuwanyima haki hao wanawake
Acha kuleta uislamu wako hapa, kwani wangapi wanaoa na bado wanachepuka
 
Kuingia kwenye dini/dhehebu au chama chochote ni hiari,lakini ukishaingia lazima kufuata mashart yote kikamilifu .Ukiingia kwenye Ukristo hilo linabaki kuwa shart la lazima.
 
Hilo swali sio kwa wakristo bali nisame siye waislam ambao wanaruhusu ndoa za mitala..

Waulize je mtu akibadili dini hao wanawake wenginr inakuaje?
Kama alikuwa na ndoa alizofunga akiwa kwenye dini nyingine, basi pale atakaposilinu na wake zake wote , hatokuwa na haja ya kufunga ndoa nyingine, Bali hizo ndoa zinatambulika na zitaendelea. Kwa kuwa idadi inafahamika ni wake wanne , sina uhakika nini itakuwa juu ya huyo wa tano. Ikumbukwe Mtume Muhammad(S.A.W) alioa wake 12. Nitawauliza wajuzi kisha nitaleta mrejesho INSHA'ALLAH. Hakika ni Allah(S,.W) ni mjuzi
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…