Swali :kwa nini hamna os ya kichina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali :kwa nini hamna os ya kichina

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mndengereko, Oct 13, 2012.

 1. Mndengereko

  Mndengereko JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 7,127
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  nijuavyo mimi wachina ni mabingwa kucopy na kupaste katika vitu mbali mbali lakini toka nimeanza kutumia computer os ninayoijua na kuisikia sana ni za microsoft kuanzia window 95-window 8 inayotarajiwa kutoka mwezi huu sasa swali kwa nini hamna os ya kichina ambayo hawa watu wangekuwa wameicopy na kubadilisha vitu kidogo tu ili kuleta ushindani kama kawaida yao?
  then window 8 karibia inatoka ktk pita pita zangu bado sijaona kama ni free from virus kwani hawa watu nini kinachowashinda kuifanya os ya window ikawa free from virus mbona apple zao ni free from virus
  swali la mwisho naombeni mnipe elimu juu ya hili hivi copmputer za aple mtu hauformat kam hizi zetu za kawaida na ikiwa umeformata wapi unapata c.d zake za window na kama c.d ya o.s ya apple ipo hivi mtu huwezi ukainstall ios katika computer za kawaida naombeni kuwasilisha wadu
   
 2. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  huwezi kuinstall ios kwenye pc hiyo ni sababu za kibiashara, apple waliamua kuweka os kwenye hardware zao tofauti na microsoft wao wanatengeneza windows then inawekwa kwenye pc kutoka kwa watengenezaji tofauti eg dell, hp, accer etc,

  unaweza kuinstall windows kwenye mac lakini huwezi kuinstall ios kwenye pc, kuna kitu kiko kwenye hardware ya mac ambacho setup ni lazima ikidetect ndo iendelee,

  pia apple wamecopyright ios isitumiwe kwenye product zisizo za apple, ukifanya hivyo utakuwa umefanya copyright infringment unaweza shtakiwA
   
 3. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  OS za kichina zipo tena nyingi tu kuanzia za simu,computers na ata za play stations.Tanzania uzioni kwani nnani anaziitaji?.Wachina wengi nnaofanya kazi nao hapa Tanzania Laptop zao zote zina chines OS.China mpaka Laptop/PC zina BIOS za kichina.
  Computer zote pamoja na zile za Apple zote zina virus.
  CD/DVD za installation kama hizi za PC zipo na zinatumika wakati unaistall. OS au programs kwenye Apple.ila kutokana na uchache wa Apple computers hapa Tanzania ndo maana uwezi ona CD za Apple kwa wingi kama unavyoziona za PC zilivyonyingi. Ila ukiziitaji hapa Dar unaweza kupatiwa
   
 4. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Achana na mchina wewe, anatisha. Kama ana uwezo wa kurekebisha masaburi hakuna asichoweza labda kuumba mtu tu.
   
 5. i411

  i411 JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Yani umeleta mada nzuri kweli, ata mimi nilishawahi kujiuliza kwanini kun os 3 tuu za komputer yani windows,ubuntu na Mac OSX. Alafu hiyo yakwanza ikaitwa windows alafu ikawa inachorwa kama kadirisha yani kama unaingia kwenye daimension nyingine hivi mhhh. labda ni coincident tuu. Alafu upande wapili kuna Mac Osx alafu zote ni marekani tuu nayo kila nikifikiria inanikera. Lakini ka ubutu kametuokoa manake inatoka kwa tajiri wa south africa na akaipa jina la mwanafilosofia wa kiafrika na siyo la kifremansonry. Alafu kuna solaris operating system nilikuwa niisahau hii haijawai kuwa popular is based on c coding for unix ni kwaajili ya severs na work stations from Oracle...
  Kuhusu hao wachina najua wametranslet tuu zile comand zote za windows kuiweka kwenye yale maandishi/vimichoro vya kichina basi na zani wamerizika hapo, hata wajapani ni hivyo hivyo wanatafsiri tuu comand za windows kwenye maandishi/michoro ya kijapani na inaonekana kama os yao lakini ni windows kama tunayotumia hapa.
  Mimi navyofikiri sababu nikuwa bado tunatumia same coding ya 32bit na 64 bits na same chips sets zile za[h=1]x86-64 tokea enzi hizo.[/h]Tukigundua njia mpya ya coding ndo tunaweza gundua os mpya labda. Pia ile limit ya transitors inazidi kuwa ndogo ndogo nazani karibuni tutafikia tekinologia nyingine labda hata quantum computing ambapo komputers zitakuwa zaidi ya tuzijuavyo leo that is the world of quatum soma zaidi hapo
   
 6. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,795
  Likes Received: 7,119
  Trophy Points: 280
  ishu inakuja ni hela, sorry naingiza mambo ya kisiasa kidogo. Wamarekani wao wana capital kubwa sababu ya ucapitalist mtu mmoja anamiliki hela nyingi. Wachina walikua kwenye usawa zamani kila mtu ana hela sawa na wengine mpaka matajiri wao wa sasa hawana hela sana. Hii inasababisha wao wachina na wahindi kua watumwa.

  Bidhaa nyingi za windows zinatengenezwa india windows ni wahindi wahindi ni windows ukiwauliza nini wanakwambia kuna cheap labour hii inamaana angetokea mhindi mwenye capital ya kutosha kuwa organise wahindi kungekua na os ya kihindi

  Apple na wachina wachina na apple same here angetokea mchina mwenye uwezo wa kuwaorganise pia wangetoa os nzuri tu.

  hio ilikua world wide tuje china kwenyewe mainland

  Kuna operatng system inaitwa red flag linux ipo china na serikali ya china waliipa sana nguvu kwa kuwaambia internet cafe waeke os hio badala ya za kimarekani sio maarufu sana duniani ila ni maarufu china.

  kuna os nyengine inaitwa aliyun os nayo ni linux based pia sema hii ni ya smartphone imetengenezwa na alibaba sema nayo umaarufu wake ni huko huko china
   
 7. Mndengereko

  Mndengereko JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 7,127
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160


  so wchina wameshindwa kuzifanya os zao zikawa world wide from ur point of view nimeelewa kwamba os hizo zipi china na maandishi ni ya kichina design kila kitu
   
 8. Mndengereko

  Mndengereko JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 7,127
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  32 na 64 bits mh!!??? misamiati hii
   
 9. Mndengereko

  Mndengereko JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 7,127
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  vipi wadau kuhusu window 8 kuwa free from viruys kwa nini apple waweze na kwa nini microsoft washindwe au wanalipwa kidogo na antivirus companies
   
 10. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  naanza kwa kukujibu kuwa OS za kichina zipo ila si mashuhuri kwakuwa developers wengo wa application wana develope application ambazo wanataka wauze sana wapate faida na ndo maana OS za kichina si mashuhuri labda huko kwao. Na kama mdau alivyosema za simu ndo utazikuta kwenye simu zao.
  Je ni kweli kwamba windows ndiyo inavamiwa na virus peke yake?
  Jibu ni hapana, hata mac pia sio free from virus ila virus wengi wanaotengenezwa wako katika exe ambayo ni extension za software zinazofanya kazi tu kwenye windows ukiiweka kwenye mac na ubuntu haiwezi fanya kazi wala haitambuliki ni kitu gani. Hata virus anayeweza run kwenye mac ukimweka kwenye windows atakuwa hatambuliki na hawezi fanya kazi.
  Windows inashambuliwa zaidi kwakuwa ndo OS inayotumiwa zaidi na watu. Pia tatizo la windows OS kuna mambo yanaweza run bila mwenye comp kuwa na habari tofauti na mac na ubuntu ambazo zinahitaji mwenye comp kuweka password au ku accept ndo mambo yandelee mbele kama kuinstall au ku unstall kitu so ni vigumu virus kuingia bila taarifa ya mhusika.
  Je ni kweli kuwa lion OS haiwez kuwekwa kwenye PC na huwezi kuipata?
  Si kweli naomba nieleze kitu kimoja, miaka kadhaa nyumba processor za comps za apple zilikuwa zinatengenezwa na kampuni ya motorola. Kutokana na architecture ya hizo processor OS ya mac ilitengenezwa kufanya kaz kwenye hizo processor hivyo isingeweza fanya kazi kwenye pcs nyingi ambazo zinatumia intel processors. Windows ambayo inafanya kazi kwenye processors za intel, amd na ibm pia isingeweza ku run kwenye comp za mac kwakuwa zilikuwa na processors za motorola.
  Toka mac ahamie kwa intel na kuboresha os yake ili i run kwenye intel basi OS ya mac waweza install kwenye PC zenye intel kama zina viwango vinavyo faa na mjya pcbao wanasema nzuri ku run mac ni HP pro 4530S. Pia kwenye pc za mac wawezaweka windows kwakuwa hivi sasa zina intel processors.
  Kuhusu os ya mac zipo hata mimi ninao lion x niliidownload nikaiweka kwenye pc ila niliitoa aa ukieka kwenye pcs kuna keys za keyboard hazifanyi kazi cozmetengenezwa maalumu kwa winws.
  Natumai nimeeleweka.
   
 11. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  windows 8 sio virus free, inashambuliwa vilevile kama windows zilizopita, kuhusu os zingne kuwa virus free liko kimaslahi zaidi, wanaotengeneza virus wanatarget windows kwa sababu ndo os inayochukua sehemu kubwa ya operating systems, hawaangaiki na linux coz yenyewe ni open source haina faida, vifaa vya apple ni vichache so hata ukitengeneza virus kwa ajili ya ios hutafaidika, japo niliona antivirus kwa ajili ya ios,
   
 12. Mr Q

  Mr Q JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,056
  Likes Received: 7,085
  Trophy Points: 280
  chief-mkwawa samahani kwa kutoka nje ya mada. Unaweza kunipa mifano ya smartphone za kichina, na ambazo ni maarufu kwa sasa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. nxon

  nxon JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,149
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  kuna os nnayo inaitw windows ghost ni ya kichina. Yaani ni xp ila wameidevelop kmtindo
   
 14. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama hiyo ni os ya kichina ila ni windows OS ambayo imekuwa modified kwa kutumia Ghost software ambayo inachange interface.
  Zipo utility nyingi za ku customize windows ambazo hata wewe waweza tumia lakini hazibadili source code ya windows so huwea iita ya OS ya kichina kisa tu imrbadilisha graphic interface
   
 15. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #15
  Oct 13, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,795
  Likes Received: 7,119
  Trophy Points: 280
  Sjajua unataka smartphone ya kichina yenye os ya kichina au smartphone ya kichina yenye os yoyote. Huawei na zte zote ni kampuni za china so ukikuta simu yoyote yao ni ya kichina.

  Simu ya kichina hot zaidi ni xiaomi
  [​IMG]

  Nimesema ni hot kwa sababu hizi

  -pixel density 342 imezizidi simu tatu nzuri duniani yani nokia lumia 920 (332), iphone 5 (326) na samsung galaxy s3 (306). Hii husaidia kuonyesha picha clear zaidi na kuifanya screen iwe bora.

  -gpu yake (graphic processor)ni 320 adreno

  - ina processor ya 1.5 ghz quadcore

  -ina ram 2gb na camera ya 8megapixel

  -video inachukua hd na hata camera ya mbele pia inachukua full hd 1080p

  Ukimalizaaa yooote price ni euro 250 tu approximately kama laki 5 ya kibongo.

  Katika benchmark 5 iliofanyiwa na gsm arena imeongoza 3 na mbili ikashika nafasi ya 2 so ni best phone kwa specification kwa sasa

  Wakati iphine wakijisifu kuuza simu millioni 5 kwa siku 3 xiaomi yeye aliuza simu laki 3 kwa dakika 4. Hii ndio china.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,672
  Trophy Points: 280
  Habari wana jukwaa...
  Nijuavyo mimi wachina hawajawahi kutengeneza OS, lakini wanatengeneza processor(chinese innovated) ambazo huwa zinatumiwa na systems za jeshi la China pamoja na other secured systems za Beijing administration tu.
  OS(napenda tuziite cloned OS) pekee hawa mabwana wanatengeneza ni zile za mobile na smartphones tu, wao wana simu zao ambazo miaka ya karibuni zimekuwa zikiingizwa Tanzania na sehemu nyingine za Afrika.
  Hili jibu nina uhakika nalo kwa kuwa nimeishi China muda mrefu tu.

  Mkuu mleta thread, any OS is vulnerable to computer viruses, keep in mind virus huwa anakuwa programmed to function/run in a particular platform in our matter it might IOS, WIN, Google Chrome OS etc etc..
   
 17. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,672
  Trophy Points: 280
  GooPhone i5 ni mfano mwingine wa Chinese phone which was released to pre-compete with Apple iPhone 5....
  HTC ni Chinese Taiwan phones pia ambazo zipo juu.
  Huawei na ZTE
  Gionee
  n.k
  n.k
  n.k
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,672
  Trophy Points: 280
  Windows Ghost sio standalone OS mkuu, ni customized OS ambapo Ghost Software imehusika kuitengeneza.
  Nia na madhumuni ni kuweza kufanya installation ya Windows within short time halafu windows inaingia na application ssoftwares kadhaa inategemea na customization ilifanyika vipi....nyingi huwa zinaingiza softwares kama winrar, microsoft office,audio and video codecs, desktop widgets, animated wallpapers n.k n.k
   
 19. m

  mwanasubi Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  window za kichina zpo kuna 1 inaitwa ghost kna window kbao na watengenezaj n wachna.
  na khsu os ya apple n mac zle nazo hua zna corrupt ila mara chache sana ze way unavoweza kufanya kwa linux hata mac yaweza
   
 20. Mr Q

  Mr Q JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,056
  Likes Received: 7,085
  Trophy Points: 280
  chief-mkwawa na watu8 asanteni sana kwa kunifahamisha juu ya hilo inapendeza kuona mtu akimfafanulia mwenzake jambo asilo lijuwa kwa kina.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...