Swali kwa Nape Nnauye

gayo

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
240
225
Ndugu yangu Nape wewe kama Mtanzania unachukuliaje haya yafuatayo:

  1. Mabilioni yaliyofichwa uswisi na Watanzania
  2. Rushwa iliyokithiri na hasa serekalini na CCM (Mwenyekiti alikiri alipokuwa anafunga mkutano wa uchaguzi wa jumuiya ya wazazi )
  3. Kesi za ufisadi na Rushwa kuchukua muda mrefu wakati ushahidi uko wazi wazi
  4. Ukweli kuhusu Richmond kutokuwekwa wazi
  5. RPC Iringa kushuhudia mauaji ya David Mwangosi na hadi sasa bado yuko kazini
  6. Usalama wa taifa kuhusishwa na utekaji wa Dk Uli. Pia kwann hii issue haishughulikiwi kama ya Kamanda Barlow??
  7. Sababu zilizokufanya utake kuhamia CCJ
  8. Kwanini issue ya Majaji vihiyo inajibiwa kwa juu juu bila kuzungumzia mmoja baada ya mwingine. Mfano Jaji Mbarouk
  9. Je CCM imekuwa chama cha upinzani? (Ndg Wasira aliomba kura ili apigane nao na mkamshangilia kweli)
  10. Unafikiri vyama vya upinzani vinasaidia serikali iliyopo madarakani?
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,718
2,000
Nnauye Jr onesha ujasiri japo ujibu maswali mawili tu unayo yataka kati ya hayo yote!

Ukishindwa kabisa jibu moja kati ya yote! Najua we ni msikivu utajibu yote ndugu Nnauye Jr
 
Last edited by a moderator:

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,264
2,000
Nape anahusika vipi na mambo yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali.

magamba wali merge halmashauri kuu na serikali, ndio maana Kinana ,Nape, Mangula, wana ujumbe mzito kwa mawaziri.

Wanataka wafundisha (wana CCM wenzao/Shetani wenzao), jinsi ya kutekeleza ilani yao.
 
Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,732
2,000
Nape anajali zaidi CHADEMA na kazi yake kuliko nchi yetu Tanzania. Kama tunataka maendeleo ni lazima tuache ubinafsi na tuangalie vitu kwa manufaa ya taifa letu. CHADEMA hata kama huwapendi ni Watanzania na matatizo wanayosema ni ya kweli hayo matatizo hapo hayatapatiwa ufumbuzi kwasababu wahusika ndiyo wenye Chama. Ni Watanzania wachache sana wenye uzalendo wa ukweli. Kwa sisi tulio nje hawatupendi kwasababu wanajua fika wengi wetu hatunufaiki na chama chochote bali tuta nufaika na maendeleo ya Tanzania.
 
Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,210
2,000
Nimeona kuna topic fulani hivi ilikuwa kwa ajili ya Nape ikafutwa haraka sana. Ile ndio dawa ya wenye midomo mipana. Nape if you live in glass houses dont throw stones. Bado zitakuja mada nyingi sana na binafsi kumhusu maana bado anaishi nyumba za vioo vitupu
 
PJS

Senior Member
Mar 27, 2012
106
0
Vuvuzela Nape njoo ujibu hapa haya maswali,au hujui wajibu wako,au upo Kona Baa unaburudika na vimwana kama ambavyo mwezi uliopita nilipokuona saa nane usiku elements club masaki mkiwa wewe na Waziri wa zamani wa mambo ya Ndani Mh Masha ukimwamulia ugomvi yeye na msichana ambaye alikuwa anamtaka kinguvu kuondoka naye bwana Masha ndipo yule binti akampiga kibao cha matakoni Mh masha,ilikuwa fedhea kubwa,na ndiyo mliyokalia hayohayo
 
SHIP

Member
Nov 26, 2012
48
0
Muulize haya pia Dr. Slaa,anauchukuliaje udini ndani ya CHADEMA?

Anajisikiaje kuona vyeo vinatolewa kutokana na undugu ndan ya CHADEMA?

Anajisikiaje kuongoza chama chenye waropokaji wasio na nidhamu?
 
kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
16,140
2,000
Hawezi kujibu!, ukitaka majibu kutoka kwa nape just muulize! anapenda kula nini? anapendelea kinywaji gan? ni starehe ipi anaipenda zaidi ya taarabu. We unamuuliza maswali mazito ambayo siyo saizi yake. Poor Nape!
 
kigoda

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,782
1,195
Hana upeo wa kujibu maswali kama hayo. Yeye umulize kama dr slaa anamiliki kadi ya ccm au la. Hapo utaona anavyo tiririka.
 
Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,668
2,000
acha uvuvi wa kuwaza

CCM yabuni mbinu mpya

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kuanzia sasa, kitawashughulikia watendaji wa Serikali wanaoitwa katika vikao mbalimbali vya chama hicho, kuelezea utekelezaji wa ilani ya chama hicho, lakini wanagoma kuhudhuria na wakati mwingine kuamua kutuma wasaidizi wao.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Taifa, Nape Nnauye, wakati akifungua semina ya Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza.

Alisema kwamba, baadhi ya watendaji hao wamegeuka kuwa miungu watu katika sehemu zao za kazi na wamekuwa wakikaidi kuitikia wito wanapoitwa na viongozi wa chama katika ngazi za utawala.

"Kama kuna mtendaji ambaye anakichukia chama kinachounda Serikali anayoitumikia kisa tu chama kinafuatilia utekelezaji wa ilani yake, anapaswa kutupisha.

"Kwa hili hatutanii, tutamtimua kazi mara moja na nyie viongozi wa CCM mnapaswa kumjadili katika vikao vyenu na pale mtakapotuletea kuwa kiongozi fulani ni mzigo kwa chama, hatutaweza kuchukua zaidi ya dakika tatu kubariki uamuzi wa vikao vyenu ili iwe fundisho kwa watendaji.
 
Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,668
2,000
Nape anahusika vipi na mambo yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali.

Ukajibiwa hivi.....

Teh teh... hahusiki ila kufukuza wafanyakazi wa serikali wasiotaka kuhudhuria vikao vyao anahusika
Bila kushirikisha ubongo ukakurupuka kujibu hivi....
acha uvuvi wa kuwaza
Sasa naomba ujibu haya hapa yaliyoandikwa kwenye Mtanzania na hadi sasa Nape wako hajakanusha, kisha jipime wewe na mimi nani mvuvi wa kufikiri..

CCM yabuni mbinu mpya

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kuanzia sasa, kitawashughulikia watendaji wa Serikali wanaoitwa katika vikao mbalimbali vya chama hicho, kuelezea utekelezaji wa ilani ya chama hicho, lakini wanagoma kuhudhuria na wakati mwingine kuamua kutuma wasaidizi wao.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Taifa, Nape Nnauye, wakati akifungua semina ya Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza.

Alisema kwamba, baadhi ya watendaji hao wamegeuka kuwa miungu watu katika sehemu zao za kazi na wamekuwa wakikaidi kuitikia wito wanapoitwa na viongozi wa chama katika ngazi za utawala.

"Kama kuna mtendaji ambaye anakichukia chama kinachounda Serikali anayoitumikia kisa tu chama kinafuatilia utekelezaji wa ilani yake, anapaswa kutupisha.

"Kwa hili hatutanii, tutamtimua kazi mara moja na nyie viongozi wa CCM mnapaswa kumjadili katika vikao vyenu na pale mtakapotuletea kuwa kiongozi fulani ni mzigo kwa chama, hatutaweza kuchukua zaidi ya dakika tatu kubariki uamuzi wa vikao vyenu ili iwe fundisho kwa watendaji.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom