Swali kwa Gwajima: Tuendelee kula malimao?

Swali kwa Gwajima: Tuendelee kula malimao?

Sisi tulishakula malimao. Sasa yeye na wenzake wale sumu.
 
Ha ha aha Gwajima alisema maneno hayo siku Lowassa alipokuwa anatangaza nia kwa mbwembwe Mjini Arusha, alisema "wasiompenda Lowassa, wakale malimao"
Gwajima na wafuasi wake na akina team Lowassa wakale sumu au wameze wembe!
 
Watakuja soon na maneno yako....., mtumishi wa Mungu..., tunaomba na kufunga mtaona kitakachowapata...., mtumishi wa Mungu nae ni binadamu huwa anakosea....! Mtumishi wa Mungu my foot! Hebu tuacheni kumdhihaki Mungu jamani!

Gwajima mchumia tumbo tu na tapeli anayetumia jina la Mungu na si zaidi ya hapo (waumini wake mniwie radhi kwa hili).

Msemo wenu wa kuwa kuna tuliokosa maarifa na tunaangamia.., hebu utafakarini kwa kina na mjiulize kama na nyie pia mmekosa maarifa na mnaangamizwa na mtu mmoja sijui amekula maharage ya wipi yule mchumia tumbo tu aliyewaaminisha kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu ilhali hastahili!

Na kesho kanisani ataendelea kuwaghilibu tu na sadaka mnampa yeye anaishi posh life nyie mwaendelea kuganga njaa!

Tena mfikishieni ujumbe kuwa aanze kula MALIMAO na PILIPILI kama alikuwa ajaanza kufanya hivyo..., na atubu!
 
Sasa tunasubiri Kula machungwa kutoka ukawa company ltd.
 
si ali.zini na mke wa mtu flolar mbasha?laana hiyo inamtafuna sasa.wakale mbilimbi sasa
 
Kitendo cha Gwajima kujipambanua kama mtabiri, mtabibu, nabiii na mfuasi wa Lowasa kwa kiasi kikubwa kimeathiri Lowasa kuingia Magogoni.
Hii ni kwa sababu watu wote wenye akiri akiwemo JK, Mkapa na Mangula watakuwa wameona ni uchuro kuchaguliwa Rais na mtu ambaye fyuzi za ubongo wake zina walakini.
Kitendo cha Gwajima kuporomosha matusi ya kihuni kwa Cardinal Pengo, mtu ambaye integrity yake Gwajima hafikii hata kwa asilimia moja, kilimwondolea heshima kwa jamii yote ya kistaarabu na hivyo mtu yeyote anayeshahabikiwa naye, lazima nae azue maswali mengi.
Taarifa za uhakika ni kwamba maaskofu Katoliki na hata wa madhehebu mengine, walikasirishwa na matusi ya Gwajima kwa Cardinal na hivyo kutoka azimio la kutounga mkono chaguo la mtumishi huyo mhuni na ndipo walipotoa misimamo yao kwa viongozi wa Serikali kuwa hawako tiyari kuchaguliwa Rais na Gwajima.
Usingekuwa wewe Gwajima, EL alikuwa na njia nyeupe magogoni.
 
Hapo hakuna uhusiano ni sawa sawa na mtu agongwe na gari harafu ukachome kituo cha polisi.
 
Usiwalishe maneno Maaskofu wa watu! Wao huwa wanatoa matamko.
 
Kwamba fyuzi za ubongo wake zina walakini....jf noma
 
Mpaka sasa Gwajima amekula malimao mangapi? Kwa walio karibu naye naomba kufahamu
 
Back
Top Bottom