Swali kuhusu Decoders za DSTV

Swali kuhusu Decoders za DSTV

Mrimi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
1,691
Reaction score
641
Nahitji kujua iwapo kuna uwezekano wa kuongeza FTA channels kwenye decorders za DSTV. Na kama inawezekana, je, muda wa kifurushi (packagea) ukiisha, nazo zinapotea?

Swali la pili, je,kuna uwezekana uwezekano wa kutumia chip(card ya DSTV) kwenye decoders nyingine, let's say Strong, zenye chip slot?
 
mi nimejaribu yote hayo nimeshindwa, tungoje wajanja.
 
La kwanza linawezekana hata kama kifurushi kikiisha zinaendelea kuonyesha.
Hebu cheki kwenye post za mwaka jana kuanzia mwezi 10 kuna mdau uliweka kila kitu mim natumia phone so siwezi weka link.
 
Uwezi kubadili smartcard ya dstv hasa hizi mpya labda zile za zamani 2008 kuludi nyuma
 
mi natumia decoder za strong na ina slot pot ambayo natumia smartcard ya dstv na inafanya kazi kama kawa. ila niyazamani
 
Wakuu naomba kujua,kifurushi cha dstv kikiisha na ukachelewa kununua kingine,kuna madhara gani?
 
Wakuu naomba kujua,kifurushi cha dstv kikiisha na ukachelewa kununua kingine,kuna madhara gani?

Madhara utakayoyapata ni kwamba watakukatia pindi tu muda wako ukiisha (wakati mwingine system yao inaweza ikakusahau kwa siku moja au mbili). Siku ukipata fedha za kulipia unaenda kulipia na wanaifungua decoder yako unaendelea ku-enjoy DSTV kama kawaida. Hakuna faini kwa kuchelewa kulipia decoder yako wala gharama za ziada
 
Back
Top Bottom