eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 16,678
- 15,173
Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu kuhusu mgomo wa madaktari nchini. Imefikia mahala kila upande unajiona una haki na nguvu kuliko upande mwingine. Kila mmoja anatunisha misuli. Madaktari kwa upande mmoja hawataki kurudi nyuma na pia serikali kwa upande wake mwingine imeshikiria msimamo wake.
Maswali yangu ni:
1. Mwananchi wa kawaida wa Kenya (ambao ndiyo wengi) amewezaje kuishi bila matibabu kwa kipindi chote hicho?
2. Je hakuna madhara kwa wananchi yaliyotokana na mgomo huo?
3. Kama yapo madhara, nani atawafidia wahanga?
4. Kama hospitali zote za umma zimefungwa, kwa maana nyingine hazifanyi kazi kwa muda wa zaidi ya robo mwaka. Je kuna umuhimu wa kuwa na waziri anayesimamia wizara hiyo?
5. Je nchi haina madaktari wanajeshi ambao wangeweza kuhudumu katika mahospitali ya umma?
Wajumbe naombeni tujadili tukiwa na moyo mkunjufu, huku tukiwafikiria wanawake, waja wazito, watoto, wazee na wengine wote ambao hawana uwezo wa kufanya matibabu kwenye hospitali zinazomilikiwa na watu au taasisi binafsi. Wamewezaje kipindi chote hicho kujitibu??
Nawasilisha.