Swali ilipo Stendi mpya ya Mbezi

Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,265
3,177
Ninasafiri kesho asubuhi sana. Je, nikipandia daladala za Mbezi hapa Ubungo Riverside nashukia kituo gani huko Mbezi?

Je, Daladala zinazitokea Buguruni na Mbagala kwenda Mbezi zinaishia stendi ya Magufuli/Mbezi?

Pana umbali gani kutoka stendi ya daladala Mbezi mwisho hadi stendi ya Magufuli?

Msaada wenu ndugu zangu mimi sio mtembeaji sana ndio maana nimeuliza haya.
 
Mwambie konda "Hoya konda siyo unapiga kelele njiani hatusikilizani kwenye gari na harufu yako ya jasho na mdomo. Hebu nambie napotaka kwenda kituo cha ma bus ya mkoani Mbezi mwisho nishukie wapi?"

Hapo atakupeleka mpaka kwenye bus unalotaka kupanda atakuogopa.
 
Mwambie konda "Hoya konda siyo unapiga kelele njiani hatusikilizani kwenye gari na harufu yako ya jasho na mdomo. Hebu nambie napotaka kwenda kituo cha ma bus ya mkoani mbezi mwisho nishukie wapi?"

Hapo atakupeleka mpaka kwenye bus unalotaka kupanda atakuogopa.
Ha ha ha tena saa 11 asubuhi kaamka na double kick kichwani lazima akusemee maneno mabovu.
 
Ndio Daladala zinazo toka njia ya Buguruni(kutoka G/mboto, Temeke nk) kuelekea Mbezi huwa zinafika mwisho wa Mbezi(kama kituo Cha daladala ya Mbezi). Ukishafika kituonii hapo upande wa kaskazini Magharibu utaona jengo La stendi hiyo ya Mabasi maana ni kubwa na lina muundo tofauti na majengo mengii(unaeza uka google picha yake kukuona ili upate picha ya utakachotegemea kukiona ukifika) pia utawaona madalali wengi tuu na utaona hata watu wengine wakielekea huko maana kunahitaji kuvuka barabara ya Morogoro ili kwenda stendi hiyo.. Kwa ushauri ikiwa huitaji kelele za madalali ukishuka usiwahoji fika sehemu unaona unaeza mhoji muhusika kama vile machinga kukuonesha njia ya kuelekea huko itakusaidia zaidi.
 
Ukifika tu raia wa tiketi wanakupokea na kama una mafurushi kama unaenda Kigoma baaaasiii wanakubebea kabisa
 
Ninasafiri kesho asubuhi sana. Je, nikipandia daladala za Mbezi hapa Ubungo Riverside nashukia kituo gani huko Mbezi?

Je, Daladala zinazitokea Buguruni na Mbagala kwenda Mbezi zinaishia stendi ya Magufuli/Mbezi?

Pana umbali gani kutoka stendi ya daladala Mbezi mwisho hadi stendi ya Magufuli?

Msaada wenu ndugu zangu mimi sio mtembeaji sana ndio maana nimeuliza haya.
Utakaposhuka Stand ya Daladala utaiona Stendi Mpya ile paler upande was pili. Ni kiasi cha kuvuka Mor Road tu.
Na kama umebeba begi basis no rahisi zaidi.
Utagombewa na Waliga Debe was Kiume na was Like...!!?
 
Asante sana mkuu.
 
Back
Top Bottom