VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Bungeni wanasimamishwa ili Wabunge wa CCM wajimwage watakavyo. Bungeni,Wabunge wa upinzani kila wanapochangia,kuuliza au kujenga hoja,Wabunge wa CCM yetu hujaa woga,hasira za hasara na 'mihemko'.
Wabunge wetu wa CCM,wanapoongea wapinzani,husikika wakisema:'Taarifa!','Kuhusu utaratibu!', 'Mwongozo!' na kadhalika. Woga juu ya woga.
Kwakuwa Wapinzani wamepungua na wakati mwingine kutoka anapoketi kitini Naibu Spika,sasa Bunge lina utulivu. Wabunge wa chama tawala chetu wana amani na uhuru wa kusema chochote. Ni kama kikao cha chama tu.
Uraiani,wapinzani wamepigwa marufuku kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa. Wamepigwa marufuku na polisi. Uraiani hukuhuku,wapinzani wanahojiwa na polisi kwa hotuba zao kwenye majukwaa ya kisiasa (mf. Maalim Seif na Zitto).
Watanzania wamekuwa wakiambiwa kuwa tangu kuanza utawala wa awamu ya tano wa Rais Magufuli,wapinzani hawana hoja za haja wala nguvu. Ikiwa hivyo ni kweli,kwanini wabanwe mbavu kila kona kiasi hiki?
Mzee Tupatupa-Kilaza wa Lumumba,Dar es Salaam