VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Uchaguzi wa mwaka jana ulifutwa naye kiutatautata. Aliufuta kibabe na kinyume cha sheria. Kwa baadhi ya Wazanzibari, Jecha Salum Jecha ni 'public enemy'. Ndiye aliyesababisha mtifuano unaoendelea Zanzibar bila ya sababu za msingi. Kwa wengine, hasa wa chama changu CCM, Jecha ametenda haki na alikuwa sahihi.
Rais wa Zanzibar anayesubiri uchaguzi mwingine, Dr. Ali Mohamed Shein amenukuliwa akisema kuwa Zanzibar inasubiri tu tarehe ya uchaguzi wa marudio. Rais Shein ameyasema hayo kwenye Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kutokana na matendo na yaliyotokea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kule Zanzibar, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha, asimamie tena uchaguzi wa marudio? Akiufuta tena itakuwaje? Akipendelea anaowataka washinde itakuwaje?
Natoa wito kuwa Jecha awekwe pembeni kwakuwa hana credibility ya kusimamia uchaguzi wa marudio!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam