SWALI: CHADEMA inaakisi chama kilichoondolewa madarakani?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Habari za Alhamisi?

Nimeona leo niulize swali ambalo kwa baadhi litawazingua,lakini ni muhimu kwa mustakabali wa siasa zetu.Kijana mmoja katika pitapita zangu mjini Arusha kaniuliza..."hivi ni kwanini chadema imekuwa na taswira kama ilikuwa madarakani?"..nikamuuliza kwanini? akanijibu "watu wengi makini wanalaumu walipotosha wananchi kwenye uchaguzi"..akaniambia "nieleze ni upotoshaji upi walifanya?"...nikaona ni vema nilete hapa JF hoja zangu kwa mfumo wa maswali.

1.Je taswira hii imesababishwa na usajili wa maveterani waliokuwa CCM?..Luwasa na marafiki zake ambao walilaumiwa kuifilisi nchi?

2.Je tatizo ni Mbowe na wasaidizi wake kupinga utekelezaji wa hoja walizoziunga mkono?

3.Je tatizo ni kutangazia ulimwengu kususia bunge....bila kuwatangazia wananchi kwanini wamerudi bungeni?

4.Je Baadhi ya viongozi hasa wakuu wa idara kumgomea Dr.Mashinji?..inaaminika kwamba Dr.Mashinji kawekwa kwa amri ya Luwasa ili kuepuka siasa za "kupayuka"

5.Je uwepo wa kundi la 4U umeimeza bavicha?

Nimeka hoja hizo ili kuibua hoja zaidi.....Pinga kwa hoja.Nyote mnakaribishwa.
 
Arusha hii hii ninayoijua mimi au kuna chumba kinaitwa arusha kwenye majengo ya Lumumba?
 
Naona umeingia shift tayari,singidadodoma alishapiga nyuzi kama 4 so kazana umpiku!
 
CHADEMA kilikosea sana sana kumchukua bwana lowasa, na kuja kwake CHADEMA ni kama upepo uliosomba machafu yoote yaliyowahi kufanyika ndani ya CCM, na hii imepelekea kuzitelekeza sera zake na kui purify CCM.
 
Katika kipindi hiki, watanzania wako busy na suala zima linalohusu maendeleo yao pamoja na kuzibaini changamoto zinazowakabili kama taifa. Kuna issue ya uhaba wa sukari ambayo hata mbunge wa Nzega (CCM) alijaribu kuiibua pale bungeni hivi majuzi kabla hajazimwa na Naibu Spika ambaye inasemekana amewekwa kwa shughuli maalum ya kuitetea serikali. Changamoto nyingine ni ufisadi kama ule uliofanywa na jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kampuni ya Lugumi. Kuna suala la wanafunzi kukalia mawe madarasani pamoja na changamoto nyingine lukuki. Cha kushangaza, wewe kila siku umekalia kuwatoa watu kwenye mstari wa kujadili mambo hayo ya msingi na badala yake unaleta upuuzi hapa kwa kuandika mambo yasiyo na kichwa wala miguu yahusuyo CHADEMA. Hivi huoni aibu kujadili mambo ambayo hayana umuhimu kwa wakati uliopo? Au ndo unalazimisha kupatiwa hiyo elfu saba toka Lumumba kwa kuandika utumbo namna hii? Badilikeni nyie vijana wa CCM, mnajidhalilisha nyie binafsi pamoja na chama chenu.
 
  • Thanks
Reactions: J C
Cdm kilikosea sana sana kumchukua bwana lowasa, na kuja kwake cdm ni kama upepo uliosomba machafu yoote yaliyowahi kufanyika ndani ya ccm, na hii imepelekea kuzitelekeza sera zake na kui purify ccm.
kuna mdau aliongeza kwa kusema..."betri ya CHADEMA imenyonywa chaji yote na betri chakavu"
 
Katika kipindi hiki, watanzania wako busy na suala zima linalohusu maendeleo yao pamoja na kuzibaini changamoto zinazowakabili kama taifa. Kuna issue ya uhaba wa sukari ambayo hata mbunge wa Nzega (CCM) alijaribu kuiibua pale bungeni hivi majuzi kabla hajazimwa na Naibu Spika ambaye inasemekana amewekwa kwa shughuli maalum ya kuitetea serikali. Changamoto nyingine ni ufisadi kama ule uliofanywa na jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kampuni ya Lugumi. Kuna suala la wanafunzi kukalia mawe madarasani pamoja na changamoto nyingine lukuki. Cha kushangaza, wewe kila siku umekalia kuwatoa watu kwenye mstari wa kujadili mambo hayo ya msingi na badala yake unaleta upuuzi hapa kwa kuandika mambo yasiyo na kichwa wala miguu yahusuyo CHADEMA. Hivi huoni aibu kujadili mambo ambayo hayana umuhimu kwa wakati uliopo? Au ndo unalazimisha kupatiwa hiyo elfu saba toka Lumumba kwa kuandika utumbo namna hii? Badilikeni nyie vijana wa CCM, mnajidhalilisha nyie binafsi pamoja na chama chenu.
Kila jambo muda wake,kuna nyuzi za sukari nenda huko...ila ukiwa humu jikite kwenye mada.
 
CCM wanachama wao wengi ni matahira na baadhi wana tatizo la mtindio wa ubongo...yaani mambo muhimu yanayohusu taifa kama sukari..lugumi ..wao kwao hayana maana zaidi ya kuwaza uteuzi tu...kusifia upuuzi ili uteuliwe...kujitoa ufahamu kwenye mambo ya msingi imekuwa fation ...kujipendekeza kwa kuongea hovyo hovyo imekuwa tiketi ya kuukwaa UDC....daah ...
 
ccm wanachama wao wengi ni matahira na baadhi wana tatizo la mtindio wa ubongo...yaani mambo muhimu yanayohusu taifa kama sukari..lugumi ..wao kwao hayana maana zaidi ya kuwaza uteuzi tu...kusifia upuuzi ili uteuliwe...kujitoa ufahamu kwenye mambo ya msingi imekuwa fation ...kujipendekeza kwa kuongea hovyo hovyo imekuwa tiketi ya kuukwaa UDC....daah ...
Sukari kibali kimeshatolewa,Lugumi kamati imeundwa..tunasubiri majibu....anzisha nyuzi kuhusu hayo kijana hujazuiwa.Jenga hoja na sio kulialia.
 
Katika kipindi hiki, watanzania wako busy na suala zima linalohusu maendeleo yao pamoja na kuzibaini changamoto zinazowakabili kama taifa. Kuna issue ya uhaba wa sukari ambayo hata mbunge wa Nzega (CCM) alijaribu kuiibua pale bungeni hivi majuzi kabla hajazimwa na Naibu Spika ambaye inasemekana amewekwa kwa shughuli maalum ya kuitetea serikali. Changamoto nyingine ni ufisadi kama ule uliofanywa na jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kampuni ya Lugumi. Kuna suala la wanafunzi kukalia mawe madarasani pamoja na changamoto nyingine lukuki. Cha kushangaza, wewe kila siku umekalia kuwatoa watu kwenye mstari wa kujadili mambo hayo ya msingi na badala yake unaleta upuuzi hapa kwa kuandika mambo yasiyo na kichwa wala miguu yahusuyo CHADEMA. Hivi huoni aibu kujadili mambo ambayo hayana umuhimu kwa wakati uliopo? Au ndo unalazimisha kupatiwa hiyo elfu saba toka Lumumba kwa kuandika utumbo namna hii? Badilikeni nyie vijana wa CCM, mnajidhalilisha nyie binafsi pamoja na chama chenu.
Unafikiri chadema isipoongelewa wakati huu,ikosolewe lini?
 
R
Hapa chuga amna m2 mwenye mambo kama ayo ata cheq chadema ilivyo badilisha chuga chuga ilikuwa ishaa potea man
Rudia kusoma ulichoandika kama unaweza kuelewa au watu wasio wahuni ni ngumu kukuelewa kijana.
 
Na litambua ilo nime andika makusudi ivyo cha msingi usi jadili mambo ya vyama hapa tafuta mjadala mwingine ishu ya ccm na chadema achana nayo 2ongelee kuhusu mushitakabali la kuli endeleza inchi yetu kwani 2ko mbali kii uchumi mambo ya lumumba achana nayo.
 
Hili ni jukwaa la siasa,kuna majukwaa mengine nenda huko.
 
CCM wanachama wao wengi ni matahira na baadhi wana tatizo la mtindio wa ubongo...yaani mambo muhimu yanayohusu taifa kama sukari..lugumi ..wao kwao hayana maana zaidi ya kuwaza uteuzi tu...kusifia upuuzi ili uteuliwe...kujitoa ufahamu kwenye mambo ya msingi imekuwa fation ...kujipendekeza kwa kuongea hovyo hovyo imekuwa tiketi ya kuukwaa UDC....daah ...
Kiuhalisia hakuna tatizo la sukari, hili lililopo ni la kutengenezwa tu na viongozi wetu, sijui ni kwa faida ya nani!?
 
Habari za Alhamisi?

Nimeona leo niulize swali ambalo kwa baadhi litawazingua,lakini ni muhimu kwa mustakabali wa siasa zetu.Kijana mmoja katika pitapita zangu mjini Arusha kaniuliza..."hivi ni kwanini chadema imekuwa na taswira kama ilikuwa madarakani?"..nikamuuliza kwanini? akanijibu "watu wengi makini wanalaumu walipotosha wananchi kwenye uchaguzi"..akaniambia "nieleze ni upotoshaji upi walifanya?"...nikaona ni vema nilete hapa JF hoja zangu kwa mfumo wa maswali.

1.Je taswira hii imesababishwa na usajili wa maveterani waliokuwa CCM?..Luwasa na marafiki zake ambao walilaumiwa kuifilisi nchi?

2.Je tatizo ni Mbowe na wasaidizi wake kupinga utekelezaji wa hoja walizoziunga mkono?

3.Je tatizo ni kutangazia ulimwengu kususia bunge....bila kuwatangazia wananchi kwanini wamerudi bungeni?

4.Je Baadhi ya viongozi hasa wakuu wa idara kumgomea Dr.Mashinji?..inaaminika kwamba Dr.Mashinji kawekwa kwa amri ya Luwasa ili kuepuka siasa za "kupayuka"

5.Je uwepo wa kundi la 4U umeimeza bavicha?

Nimeka hoja hizo ili kuibua hoja zaidi.....Pinga kwa hoja.Nyote mnakaribishwa.
Njozi za kwenye mkeka kijiweni lumumba. Mchana mwema
 
Back
Top Bottom