Wazo zuri sana..! Hata mie najiuliza CDM ni chama cha demokrasia gani. .. Yakupiga matofari wanao whistleblow! Kuonekana msaliti unapo tumia haki yako ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa!Hili hawawezi kujibu hili
Mchungaji heshima kwako,ila naonmba tupishane kidogo.Ulichondika ni dhambi nyingine ya kutojua na inapotosha wengine wengi zaidi.Hii ndio maana makanisa yetu hayajui wapi si sehemu ya kukomboa watu na wapi wamejiweka ktk kuwa ukuta wa kuwashikia watu ktk mateso.Hawa watu unaowashikilia wanamkufuru Mungu zaidi ya unavyojaribu wafanya wamtukuze na kurudishia heshima yake ktk maisha yao. UNAFAHAMU KABISA KTK DEMOCRASIA WENGI HUWEZA BADILI MAMBO,SASA KM SHERIA ZA CCM ZILIRIHUSU KUANGUKA KWA NIDHANI KIASI CHA VIONGOZI NA WANACHAMA WAO WAKAAMUA ISHI KTK UVU BILA YEYOTE KUONA KUWA KAVUNJA SHERIA.NI WAZI NAO SASA NI WENGI KIASI CHA KUIFANYA CCM IFANANE NAO.CCM HAIWEZI KUWA NZURI KM IMEZAA ZAIDI YA NUSU YA WATU WABAYA,NA KUWAPA HAO WABAYA NAFASI YA KUKIPAMBA NA KUKIPA CHAMA SURA.UHAI WA CHAMA NI WATU NA CHAMA KINAKUWA NA MVUTO KM KILA KITU CHAKE KINAFANYA KAZI YA MATAMANIO YA WAOVU.CCM kama Chama si kibaya, walio wabaya ni watendaji na viongozi wake. Ni viongozi na Watendaji ambao wamekidhalilisha Chama cha Mapinduzi na kukifikisha mahali kilipo. Kama tunavyoongelea Chadema na Ukabila, Chadema kama chama si cha Kikabila, ila ni uongozi ambao umefanya kionekane kuwa ni cha Kikabila, same with CCM na Ufisadi. Viongozi na watendaji wengi wa CCM, hawafuati kwa undani imani ya Chama chao, ndio maana kinaonekana kupoteza mwelekeo. Kinachoipa CCM nguvu ni wanachama wakweli, Wakulima na Wafanyakazi ambao wamekuwa katika chama na kushuhudia uimara wake, na bado wanasubiri siku ya nuru ambapo kitarudia hadhi na heshima yake.
ccm bado ni chama cha mapinduzi kwa sababu kimefukuza mafisadi wakapokelewa upawa,na kukumbatiwa na chademTarehe 5 mwezi februari mwaka 1977 nikiwa mwanafunzi wa Form 3, nilikuwa mmojawapo wa waliochukuliwa kutoka shuleni kwetu kuunda gadi moja ya kucheza halaiki tukishirikiana na wanafunzi wa shule za msingi.
Katika hotuba yake Mwalimu Nyerere aliyoitoa kutokea uwanja wa Aman kule Zanzibar alituahidi kuwa waliamua kuunganisha vyama vya TANU na ASP ili kuunda chama kiomoja chenye nguvu kitakacholeta mapinduzi ya haraka kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa watanzania wote. Wakati huo TANU ilikuwa imefikisha umri wa miaka 23 wakati ASP ilikuwa na umri wa miaka 20 tu. Katika kipindi cha uhai wa vyama hivyo vya TANU na ASP vilikuwa vimeshaleta mafanikio makubwa sana nchini. Vyote viliondoa ukoloni nchini na vilikuwa vimeshaanza kuboresha maisha ya mtanzania. Vilijenga mazingira ambamo wanachi walikuwa wanajivunia nchi yao na viongozi walikuwa wanajua kuwa wao ni watumishi wa wananchi; malalamiko ya wananchi yalikuwa yakichukuliwa kwa uzito sana na ule msingi wa CHEO NI DHAMANA ulikuwa na uzito sana.
Leo hii ni miaka 31 tangu CCM izaliwe; huo ni umri mkubwa sana zaidi ya ule wa vyama vilivyoizaa. Mazingira yaliyojengwa na chama hiki ni yale ambamo wananchi hawana imani na utawala, na vile vile watawala wamekuwa hawaogopi malalamiko ya wananchi. Yote hayo kwa pamoja yameondoa uzalendo kabisa miongoni mwa watu wetu ambapo, viongozi wetu bila woga wanaweza kusaini mkataba wa kukodisha yetu kwa mtu mwingine milele!! !!. na mtu akiuliza kulikoni, basi anapewa vitisho vikali.
Mfano mzuiri ni hili tishio lililotolewa na Katibu Mkuu wa CCM dhidi ya kijana Nape Nnauye kufuatia tamko lake kuhusu ufisadi ndani ya UVCCM. Tihio hilo linaonyesha jinsi gani chama hicho kinavyoheshimu mafisadi na kuwapuuza wananchi tofauti na ilivyokuwa wakati wa TANU na ASP. Kwa nini Makamba amtishie kijana yule badala ya kumtaka alete ushahidi ili yeye (Makamba) aweze kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watuhumiwa hao badala ya kutoa onyo kabla ya kuangalia ushahidi unasemaje. Huko siyo kujenga mazingira ya mapinduzi.
Ndiyo maana najiuliza, je kweli chama hiki bado ni chama cha Mapinduzi yale tuliyoahidiwa mwaka 1977?