Swala la simba kuhonga mtibwa;hosea usilikalie kimya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swala la simba kuhonga mtibwa;hosea usilikalie kimya

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, Sep 30, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,165
  Likes Received: 5,592
  Trophy Points: 280
  Nahisi inapoelekea sasa rushwa itatuvua nguo
  kwa wale wapenda michezo nafikiri ni wakati muafaka sasa wa kuwam makini kama tunataka kuwa na timu nzuri ya taifa...nakumbuka nililalama sana kipindi fulani viongozi wa maji maji walikamatwa nkwa kutoa rushwa matokeo yake viongozi wakaishia kufungiwa miezi kadhaa...nikamuuliza mwakalebela ndugu yangu kipindi hicho iweje mnapindisha sheria za tff..amjui akaitokea mwingine anakuja kunukuu mlichomfanyia waterwater..leo hii kwa sheria za tff atukutakiwa kuwa na majmaj ligi kuu

  swala la ulimboka mwakingwe hili si la kuachia wazi..watu wamelalamika sana mechi za simba na yanga waamuzi wananuliwa tff ikakaa kimya sasa leo hii wachezaji wameanza kununuliwa tunapeleka wapi soka letu jamani??je ni tenga tff imekushinda ama??

  Leo hii viongozi wanapiga makocha wanaachwa...nilitarajia viongozi wa kagera kupewa adhabu kali ya kuheshimu watu uwananjani lakini akuna kipya ni ule ule upupu wakina ndolanga sasa umehamia kwa tenga

  nadhani imefika tuwe na mpira wa kudhamiria na si bora timu..hivi majuzi nimejua kwa nini tukienda klabu bingwa tunaishia kuagiza tea cofee kwenye ndege na kurudi kama tulivyoenda...ni huzuni kubwa na ya kusikitisha...waziri husika nilifikiri wakati huuu ambao mhusika aliepelekewa akikiri ulimboka alitaka kumpa acheze kiwango duni ni wakati muafaka wa kutafuta wakina ulimwombka tupunguze makelele ya waamuzi...

  Leo hii nimejua kwa nini timu za simba na yanga na azam zimanza kulalama adharani ili hali wakijua timu za sasa ziongeki nafikiri wameanza kuwa na kichaa ...sitashanga kusikia idelphonce amlima akipewa jukumu la kuwahonga wachezaji wa simba..kumradhi kaka nimekutumia kwa kuwa ulikuwa bora kiwanjani na sibora mchezaji..naona simba wanajitete walimfukuza jamaa oohh sijui akuondoka kwa amani amani ipi wanayotaka atoke dar mpaka moro yeyey ana kichaa jamani

  mkuu hosea tunaomba rushwa sasa ianze kupungua hata kama itachukua muda kuisha basi iishe kwenye vizazi vya wajukuu vyetu tukiwa hai...
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Acheni unoko kwani Uli alishikwa akimpa hizo rushwa kipa wa mtibwa au alikuwa na pesa zake mfukoni ila akaenda kumtembelea rafikie kipenzi Kado?Hapo hakuna kesi mkuu!
   
 3. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Huyo huyo rafikie kipenzi ndiye ametoa taarifa kuwa jamaa amemfuata ili kumhonga laki 4! Kwani unafikiri story yenyewe ilianzaje??
   
 4. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hebu sikia nikwambie,hadithi ilianza mbali sana pale Tenga na kamati yake walipoingia madarakani kupitia rushwa hiyohiyo(hapa naweza kutunga kitabu,maelezo ni mengi).
  ---soka la bongo,dorminants wake ni wahuni,kwa hiyo basi, wanakaa wahuni ngazi ya vilabu, wilaya na mikoa kuchagua wahuni wenzao tena kwa rushwa hiyohiyo.
  ---hawa wahuni waliochaguliwa kwa rushwa tunawatuma waende kutuchagulia viongozi wa kitaifa,unategemea nini?
  ---kamati inapochaguliwa inateua kamati ndogo ndani ya TFF ktk mtindo wa kulipana fadhila(hiyo ni rushwa hata kama hujaona hela hapo).
  ---sasa unategemea system kama hii inaweza kudhibiti rushwa?
  Sakata la Othman Kazi mwaka jana ni mfano hai kuwa TFF na TAKUKURU hawawezi kudhibiti rushwa ktk soka kwa sababu ya nguvu kubwa ya kimaamuzi iliyopo ktk Simba na Yanga.Timu zinazoitwa ndogo zinamezwa na kanuni za kijingajinga zilizopo TFF ili ku-favour hivi vilabu vikubwa na si ajabu kusikia kuwa TFF kwao ni bora ligi ikawa ya timu mbili kuliko kuipoteza mojawapo ya hizi timu.
  Hatutafika kwa mtindo huu,tunaumia sana sisi mashabiki wa soka bongo hasa tunapoona timu zenye uwezo mkubwa wa kuzi-challenge hizi timu,zinahujmiwa makusudi ili zishuke daraja. No problem ipo siku yatakwisha haya.
  NB:Kama TAKUKURU watawakamata Uli na Kado,ndo tutajua kama Simba ilihonga au la,vinginevyo hii itabaki kuwa story.
  Na vipi kuhusu matokeo ya mechi yenyewe,unadhani nayo yana athari ya ULI na Kado?
  Na unafikiri kuwa Mtibwa walifanya juhudi ya kutosha uwanjani ili kushinda mechi lakini wakaathirika na sakata la Uli na Kado? Au walifungwa kwa vile kufungwa na Simba kwao ni kawaida?
   
 5. M

  Magehema JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii itakula kwa Ulimboka, Kado kakiri hadharani kwamba Uli alitaka kumpa rushwa, na bahati mbaya sana kwa Uli na Simba pia na mpira wa bongo kwa ujumla wake Kado alirekodi mazungumzo yote kati yake na Uli. Umefika wakati wa kuichukia rushwa katika sura zote. BTW: Ile kesi ya yule aliyefoji signature ya Athuman Idd iliishia wapi? TAKUKURU Mpooo au mmelala?
   
Loading...