Arafat
JF-Expert Member
- Nov 17, 2009
- 2,581
- 758
CCM imeibuka na Msemo mpya 'Kijivua Gamba!'
Kila mwanchama wa CCM anaimba huo wimbo hadi Rais ambaye ndie M/kiti wa CCM pia anaimba huo wimbo, chorus inasema 'tumewapa siku 90 Mafisadi wajiondoe katika Chama la sivyo tutawatimuwa' Mwimbishaji ni Nape, sauti ya nne anaimba Mkama, 'CCM imezaliwa Upyaaaa!'
Kweli sikio la kufa halisikii dawa, nani aliyewaambia CCM kuwa sisi bado ni Wadanganyika! Hivi CCM haijui kusoma alama za nyakati na kujua kuwa Watanzania wa leo sio wa jana! Eti kwa kuwa Mwinyi alikuwa Rais kwa kugombea na giza hivyo CCM bado inaota ndoto za aina hiyo!
Chama kilichoshika Dola kina lalama, nani atawakamata Mafisadi na wauza madawa ya kulevya kama CCM na Kikwete wote wanawaomba Mafisadi kujitoa ndani ya CCM, 'Wanawaomba!' maajabu kama siyo kiini macho.
Wezi wa EPA pia waliombwa kurudisha fedha na kuwa waliorudisha hakufikishwa mahakamani! Majina ya Wauza madawa ya kulevya Kikwete ameyalali! Chadema iliposema kuna list ya Mafisadi kumi na moja Kikwete na CCM walipinga kwa sauti moja leo Kikwete na CCM wote kwa sauti moja wanapita na kuwaomba Mafisadi waondoke ndani ya CCM, kumbe ukiwa Fisadi huwezi kukamatwa? Mahakama na Jela hutoshi humo!
Hivi kwanini Polisi wanawaonea Raia wasio na hatia na kuwabambikiza kesi za uongo wakati kuna watu wanajulikana hadi na Rais kuwa ni wahujumu uchumi wa Taifa hili lakini hawachukuliwi hatua yoyote? Kama Kikwete na CCM haiwezi kuwafikisha Mahakamani Mafisadi nani ataweza? Dola anayo nani amsaidie kikwete kushugulikia Mafisadi! Hii inatofauti gani na ile ya kuwa Mafisadi hawakamatiki!
Kwanini Kikwete hasijiuzuru kama kuna watu anawaogopa na hawezi kuwashugulikia hata kama wakifanya kosa lolote lile! Hivi swala la kushughulikia Mafisadi ni Swala la Chama au serikali? Sawa, Nape anapiga kelele kuwaomba waondoke CCM, vipi Serikali ya kikwete mbona haichukui hatua yoyote? Polisi, PCCB na UWT hawana la kuwafanya hawa Mafisadi! Hivi hamna Sheria yeyote ya Tanzania waliovunja? Taarifa za weakleaks za kikwete Kumzua Hoseah kuwashughulikia Mafisadi itayeyuka vipi? Mtoto wa Mkulima anamuenzi vipi Sokoine katika eneo hili?
Je CCM wanadhani uchafu walionao ni huo wa Mafisadi 11 peke yake, ingawa wao wanasema watatu (3) tu!? Mbona Nape na kikwete hawatwambii hawa watatu wamefanya Ufisadi upi? Sasa tunahitaji Kila watakapo pita wataje majina ya hao Mafisadi wanaotakiwa kuondoka ndani ya CCM na pia wataje Ufisadi walioufanya kila mmoja na Ufisadi wake, la sivyo Tutaendelea kuwaona CCM kama mnafanya kiini macho.
Huu ni muda wa vitendo siyo maneno matupu.