hapo ndipo ninaposhangaa. Ina maana ubora hauangaliwi kwenye hizi filamu? Kwa lugha nyingine hata kama filamu mbovu mradi kuna staa ndani basi! Pia hao mastaa walishushwa na ustaa wao? Uzuri wa mambo ya burudani ni kuwa mtu anakuwa staa kufumba na kufumbua. Tutawapiku tu hao wadosi soon
Raia Fulani,
Unachokishangaa pia ni chanzo zha kudorora kwa tasnia yetu, ingawa wanadhani majina
ndiyo yanayouza. Kutokana na utafiti wangu, kuna vigezo muhimu viwili ambavyo vinaweza
kutuongoza katika dhana nzima ya mafanikio katika usambazaji filamu; (1) Maudhui/Mahitaji
ya Watazamaji (
Content/Audience Connection) na (2) Jukwaa la Uwasilishaji (
Media Delivery Platforms).
Maudhui/Mahitaji ya Watazamaji:
Kwa miaka kadhaa, sekta ya filamu Tanzania imeshuhudia utofauti mkubwa kati ya maudhui
katika hadithi zetu na kile watazamaji wanachokihitaji, na matokeo yake yameendelea kuyumbisha
mikakati ya soko na sera za usambazaji. Maudhui lazima yahusishwe moja kwa moja na mahitaji
ya watazamaji ili kuwe na nafasi ya mafanikio kwenye soko.
Maudhui yanayofaa katika kizazi cha leo ni yale yanayokwenda sambamba na watazamaji ndani
ya akili zao na kuihusisha jamii moja kwa moja. Mafanikio yanayotokana na maudhui yanategemea
sana mmenyuko wa watazamaji, na kujenga maudhui yaliyo kwenye mstari na mwelekeo wa
watazamaji na matarajio yao imekuwa vigumu, na sasa inahitajika kwa watayarishaji/ waandishi wa
script kujihusisha moja kwa moja na mtazamo wa watazamaji katika mazingira waliyomo. Kwa matokeo
haya, utafiti ni suala la kupewa umuhimu mkubwa kabla ya kuandaa kazi husika.
Kitu ambacho mtayarishaji/ mwandishi anapaswa kujua kuhusu watazamaji wake ni muhimu sana
kwa mafanikio katika biashara ya usambazaji. Kujenga maudhui bila uelewa mkubwa na ufafanuzi kwa
walengwa, ni kama kufunga safari ya kwenda mahali bila kufikiria jinsi ya kufika huko. Kama maudhui
yako hayakushikamana na aina ya maisha au matarajio ya watazamaji wako, jua umewapoteza.
Kundi la kwanza la watazamaji wa filamu ni la akina mama wa nyumbani, wafanyakazi wa ndani, na
vijana wasio na ajira. Kundi la pili ni la watazamaji linalotokana na matokeo ya moja kwa moja ya kituo
cha Africa Magic kuonesha filamu kwenye familia za watu wa tabaka la kati na la juu wenye uelewa
mpana kwa maana ya kwenda shule.
Na bila shaka kuna kundi la tatu linalotokana na watazamaji Watanzania walio nje ya nchi na Waafrika
(hasa wanaojua au kukipenda Kiswahili) katika bara la Afrika na maeneo waliko. Ni muhimu kuelewa
kwamba kila moja ya makundi haya ya watazamaji yana muundo na mawazo ambayo ni tofauti sana
na kundi jingine.
Katika utazamaji filamu hizi, kuna dhana ambayo huendana na mitazamo ya watazamaji (matamanio,
maadili, na mtazamo wa mtu binafsi kulingana na uzoefu wake katika kuangalia kazi mbalimbali) na vitu
hivi huathiri namna watazamaji wanavyohusiana na dunia inayowazunguka, ikiwa ni pamoja na maudhui.
Kama mtayarishaji wa filamu, suala la kwanza unatakiwa kuwajengea msingi watazamaji katika maudhui
uliyoyakusudia, ukielewa kwamba unaweza kuwa bosi kwenye kampuni yako ya production; LAKINI
UNACHOKIFANYA SI KWA AJILI YAKO! NI KWA AJILI YA WATAZAMAJI NA HADITHI ZAO!
Jukwaa la Uwasilishaji:
Watazamaji wanahitaji pia majukwaa ya habari kama wanavyojali kuangalia maudhui. Falsafa hii
ni muhimu wakati unaposhughulikia maudhui yanayowafaa watazamaji. Maudhui ya jukwaa la
uwasilishaji katika dunia ya kisasa ya filamu hayaishii tu kwenye kazi ya usambazaji, yanakwenda
ndani zaidi ya kile hasa soko la filamu lilivyo leo. Jukwaa litasaidia kuwasilisha mawazo kwa watu
katika njia itakayojumuisha mitazamo yao.
Mustakabali wa biashara ya usambazaji wa filamu na masoko Tanzania unatokana na watazamaji
vijana. Watoaji filamu wanatakiwa kuandaa kwa uangalifu demography hii ya watazamaji na
kukutana nao katika dunia yao. Dunia hiyo hustawi kwenye kundi la kweli la teknolojia ya digitali.
Katika hatua hii itakuwa vizuri pia kuuchunguza mfumo wa usambazaji ili kupata ufumbuzi wa
kutangaza na kusambaza (promotion and distribution solutions) ambao umesaidia kurekebisha
tasnia katika nchi nyingine, ili uigwe katika sekta ya filamu Tanzania. Film is a brand, kama zilivyo
brand nyingine, kuzitangaza na kuzisambaza ni vitu vyenye umuhimu sawa.
Ili tuweze kupiga hatua kwenye suala hili tunahitaji nguvu kubwa kuielimisha jamii faida za kutumia
mitandao ya jamii inayoweza kusaidia utoaji habari za filamu na kujenga jamii yenye wafuasi, na humo,
mijadala inaweza kujadilika, kipengele muhimu kabisa cha kuleta ufahamu au kampeni ya kujitangaza.
Jumuiya hizi ni maeneo ambayo watu wanaotembelea wanaweza kupata habari zaidi, kushiriki katika
mijadala, kujiunga na majarida, na kubadilishana ujuzi na mawazo na watu wengine, kwa lengo la
kupanua wigo mkubwa wa watazamaji.
Katika miaka michache iliyopita, mitandao imesaidia sana kufanya uwepo wa gharama nafuu katika
promotion and marketing kwa watengeneza filamu na hata kwa studio. Katika baadhi ya tasnia za
filamu za nchi zilizoendelea, ni nadra na kosa kubwa kutokuwa na tovuti ya kutangaza filamu kabla
haijaoneshwa kwenye majumba ya sinema.
Tunahitaji kuelekeza namna nzuri mitandao ya jamii inavyoweza kusaidia na kufanya kampeni yenye
kuleta mwamko wa namna ya kujitangaza kwa ajili ya watoaji filamu. Njia ya haraka na madhubuti ya
kujenga jamii ya watazamaji kupitia vyombo vya habari za mtandao ni kutengeneza dedicated website
ili kutoa makala, film clips, ku-downloads picha, miziki, soundtrack, wallpapers, na kadhalika.
Pia kuwapa mashabiki fursa ya kupata habari kuhusu maudhui/hadithi, wasifu wa waigizaji, na kuchangia
maoni yao na hata kuonesha interest zao katika filamu kwa jumla kutasaidia kuenea kwa taarifa au tetesi
za filamu. Mbali na kuwa na tovuti ya kujitolea, Kuweka filamu yako kwenye mitandao ya kijamii iliyopo ni
njia nyingine nzuri ya kuongeza jamii ya watazamaji/wafuatiliaji wa filamu.
Pia matamasha ya filamu husaidia kueneza taarifa miongoni mwa wakosoaji wa filamu na watazamaji,
na inaweza kuongeza umaarufu wa filamu na watazamaji kuwa wengi kama mapitio yake yatakuwa ya
kuvutia. Wakati sisi tukiendelea kukaa katika ulimwengu wetu wa 'uvivu wa fikra' sehemu nyingine ya
dunia inasonga mbele kwa kasi zaidi kuliko tunavyodhani.