Suzuki Jimny , Manual or Automatic

Mavindozii

JF-Expert Member
Oct 20, 2012
2,109
2,752
Hello team Magari ,naombeni ushauri wenu ,nina mpango wa kuagiza hii Suzuki Jimny sasa sijajua ni ipo Bora Kati ya Manual Transmission au Automatic transmission msaada wa ushauri please
 
Unataka kuagiza generation ipi? Zipo generation 4.

Weka hata picha tutakushauri.

Ila kwa transmission chukua manual.
 
Chukua Manual Hasa Ile Yenye Kidonge (4WD)
Zipo Nyingi Suzuki
Suzuki Maruti
Suzuki Gypsy
Suzuki........
Suzuki Jimny
 
Ndio hiyo nimechukua manual transmission
IMG-20210721-WA0025.jpg
 
Binafsi ningekushauri kuchukua manual lakini ambayo haina turbo (obvious itakuwa 1300cc), kinyume na hapo chukua automatic lakini yenye turbo 650cc.

Sababu za msingi ni hizi.
-Kuhusu Turbo: Gari ikishakuwa na turbo maana yake engine inakuwa na nguvu zaidi na imara (inaweza kupiga masafa na with long life span of engine) lakini itatumia mafuta zaidi. Hivyo chukua isiyokuwa na turbo lakini yenye cc kubwa lakini vyema ikawa manual ambayo itakuwa ni original version ya suzuki jimny.

-Kuhusu Manual transmission vs Automatic transmission: Kiasili Suzuki Jimny ni manual car without turbo (uimara wake ulipojidhihirisha kwa watu na mafundi), ujio wa Suzuki Jimny yenye Automatic transmission haukupunguza uwezo wake lakini ulishindwa kuwafanya watumiaji wake kuweza kuamini kama ni imara kama mwanzo na hiyo ni kwa sababu mafundi wengi (hawa wa kitanzania) walishindwa kuifanyia repair gearbox yake pale ilipoleta shida kwa kuwa hawakuwahi kujifunza kuitengeneza. Lakini kwa wenzetu huko ulaya ni tofauti kabisa kwa kuwa mafundi wao ni certified ambao wanajifunza kila mara kitu kipya kinapoletwa sokoni. Wao wanaona automatic ni bora!

Ni imani ya watu wengi kuwa gari ikiwa manual maana yake ni old model&durable na ikiwa automatic ni new model&luxury. Lakini yote kwa yote kiujumla gari nyingi ambazo ni automatic ni user friend but less durable ikiwa utazilinganisha na manual.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom