Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,604
Aliyekuwa Mbunge wa Mlimba 2015-2020 kupitia Chadema, Susan Kiwanga ambaye sasa ni mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) amechukua fomu kuomba ridhaa ya chama chake kipya kuwania ubunge wa Mlimba katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Kiwanga amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumatano, Julai 23, 2025, Ifakara Mjini na Naibu Katibu Mkuu wa Chaumma-Bara, Benson Kigaila.
Kiwanga amechukua fomu hiyo sambamba na wanachama wengine wa CHAUMMA wanaotia nia kugombea nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge katika majimbo ya Ulanga na Kilombero, wakati wa kikao cha ndani cha chama hicho kilichoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila.