Surpriiiiiiiiise my dear!

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,723
Hivi ikitokea mpenzi wako kaamua kukufanyia bonge la surprise kwa kukununulia zawadi,
We umetulia una watch TV mpenzi wako yupo chumbani mara akaja kutoka chumbani akakuambia "Supriiiiiiiiiiiise funga macho baby,usifungue mpaka nikuambie baada ya sekunde kadhaa akakuambia fungua macho,
Ghafla ukakutana na suti ambaye yeye anaamini utaipenda mno ila kiukweli wewe ku icheki hivi the way kitambaa chake kinang'aa hukuifurahia.

Sasa utafanayaje huku mleta zawadi keshafungua mikono yote miwili anasubiri hug la nguvu na thanks darl nyingi?

Na hata baada ya kushukuru utadhubutu kumwambia haujaifurahi zawadi na huku yeye anataka uivae Jumapili inayofuata.
Ukiwa umempa hug anakuambia nilijua tu honey utaipenda yaani nimepata shida kuitafuta mpaka nikaipata hii.

Na si lazima iwe suti huu ni mfano tu,
Assume ni zawadi yeyote umeletewa ikawa hivi utafanyaje?
 
Hata kama zawadi kutoka kwa mama yangu mzazi kama siipendi nitasema hasante, halafu nitamueleza nikiwa namuangalia usoni kwamba SIIPENDI na sitoitumia.
 
Hata kama zawadi kutoka kwa mama yangu mzazi kama siipendi nitasema hasante, halafu nitamueleza nikiwa namuangalia usoni kwamba SIIPENDI na sitoitumia.

Mkuu mi nina mawazo tofauti na wewe!! hivi unafikiri kila mtu ana bahati ya kupata zawadi? wengine wanakata hata mwaka mzima hakuna mtu aliyemkumbuka kwa zawadi!! na isitoshe zawadi huichagui anachagua anayekuletea.Kwa kuyasema hayo maneno unaondoa nafasi ya zawadi kwa mara nyingine, mtoaji anavunjika moyo, kumbuka amenunua kwa upendo huku akifikiria kukufuraisha, itamuumiza.
 
Pokea tu. Be happy for the efforts she put in it. Baadae (few days) unaweza kuongea nae na kumwambia unacho fikiria kuhusu zaawadi. Kumbuka kumshukuru na kumsifu kwa efforts zake, halafu mwambie angetaka ufurahi zaidi maybe angetafuta ambayo iko hivi, na hivi. Just find the right time and her right mood before you discuss.
 
Kabla ya hapo inabidi watu tujifunze kuwasoma wenzi/ndugu na marafiki zetu. Jua style yake ya mavazi na mapambo, vitu vya ndani, aiana ya mitoko mpaka na vyakula anavyopendelea.

Yani ukimpa mtu kitu huna wasiwasi moyoni, unajua kabisa atapenda tena sana.

BTT. . .ntashukuru ila ntamwambia haitonipendeza/haiendani na mimi. Ntajitahidi aelewe kwamba kanifurahisha sana japo siwezi kuivaa.
 
Usimuonyeshe kua hujaipenda on the spot,onyesha kufurahi hata kama ni kwa unafiki then baada ya muda kupita ndio unamwambia indirect ili asijisikie vibaya! Mfano kama ni viatu vya rangi nyeupe unamwambia baby hivi unajua mimi napenda rangi nyeusi?ningepata vyeusi ningefurahi zaidi..hapo ujumbe utakua umefika na haitomuumiza..
 
hii ni very good thread kwa wanawake

most ya zawadi zao huwa hivyo...

unaletewa shati la njano au pink...

unajifanya tu kufurahi lol
 
Mambo ya kuiga ni pasua kichwa kweli! Mpenzi wako ana haraka ya kufa mtu, mpenzi na hamfahamiani kiasi hicho?! Hajui unapendelea kitambaa/rangi gani, bila shaka hajui unalala saa ngapi, unapenda misosi gani, kinywaji gani... Ndiyo maana kwa mfano tu, ukijadili na wanaume bongo kuhusu uvaaji wa suruali kwa akina dada wengi watakwambia haziwavutii kabisa! Lakini ukiuliza kama wanawake wao wanavaa? Utapata jibu 'ndiyo' Tatizo nini? Kila kitu ni vululu vululu wizi mtupu, hakuna mawasiliano ya maana. Unafiki na uongo kibao. Kama mkeo/mumeo anawaza kukupa zawadi na hawezi kujua zawadi gani itaku-touch, hapo kuna tatizo tena kubwa sana.
 
Hata kama zawadi kutoka kwa mama yangu mzazi kama siipendi nitasema hasante, halafu nitamueleza nikiwa namuangalia usoni kwamba SIIPENDI na sitoitumia.
Da jamaa jasiri sana wewe.
 
kwa mie binafsi nitaipokea kwanza nampongeza kwa zawadi aloniletea, kadri cku zinavoenda ntakuwa najitahd kumwambia vitu ninavyopendelea. dada Lizzy kaongea vyema kwamba ni vizur kuwasoma wenzi wetu,kwa kujazia pia ni vizur pia kuwa na tabia ya kuuliza anapendelea nini. mf. unaweza kujitanguliza "baby me huwa napenda skin jeans, hv we wapenda jeans aina gan atakujibu" cku ya cku utakuwa umepata jibu mwez wako anapendelea nini,pia unaweza kuangalia nguo zake huwa anapendelea nguo/viatu...
 
Last edited by a moderator:
Pokea tu. Be happy for the efforts she put in it. Baadae (few days) unaweza kuongea nae na kumwambia unacho fikiria kuhusu zaawadi. Kumbuka kumshukuru na kumsifu kwa efforts zake, halafu mwambie angetaka ufurahi zaidi maybe angetafuta ambayo iko hivi, na hivi. Just find the right time and her right mood before you discuss.
Hahahahahah Roulette na jpili inatakiwa uivae ili yeye aridhike so utaivaa?
 
Last edited by a moderator:
Kabla ya hapo inabidi watu tujifunze kuwasoma wenzi/ndugu na marafiki zetu. Jua style yake ya mavazi na mapambo, vitu vya ndani, aiana ya mitoko mpaka na vyakula anavyopendelea.

Yani ukimpa mtu kitu huna wasiwasi moyoni, unajua kabisa atapenda tena sana.

BTT. . .ntashukuru ila ntamwambia haitonipendeza/haiendani na mimi. Ntajitahidi aelewe kwamba kanifurahisha sana japo siwezi kuivaa.
Lizzy well said ila saa ingine inatokea unaghafilika mimi nakumbuka tukiwa kwenye u boy friend na u girl friend nilishawai kumnunulia mpenzi wangu nguo ya ndani yenye msg ya I LOVE U nikiamini ni bonge la zawadi kumbe hakuipenda na kuniambia alishindwa yaani mpaka nimekuja muoa ndo nagundua bado ipo sandukuni.
Kumwuliza akaniambia kweli hakuipenda ila ni miaka kama 10 ishapita.
 
Last edited by a moderator:
kwa mie binafsi nitaipokea kwanza nampongeza kwa zawadi aloniletea, kadri cku zinavoenda ntakuwa najitahd kumwambia vitu ninavyopendelea. dada Lizzy kaongea vyema kwamba ni vizur kuwasoma wenzi wetu,kwa kujazia pia ni vizur pia kuwa na tabia ya kuuliza anapendelea nini. mf. unaweza kujitanguliza "baby me huwa napenda skin jeans, hv we wapenda jeans aina gan atakujibu" cku ya cku utakuwa umepata jibu mwez wako anapendelea nini,pia unaweza kuangalia nguo zake huwa anapendelea nguo/viatu...
I like it.
Hiyo baby inavyotajwa sasa mimi huwa hoi kabisa.
 
huyo labda awe ndio kwanza mmejuana..kama ni mpenzi wako na anakujua fresh basi atajua taste zako so atakua analeta kitu ambacho ana uhakika utapenda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom