Kiturilo
JF-Expert Member
- Sep 27, 2021
- 709
- 2,858
Nimepitia maktaba yangu ya mambo ya siasa nimegundua pasi na shaka siku Tundu Lissu mwaka 2014 akikutana na Tundu Lissu wa mwaka 2022 'watauana' .
Tundu (2014) hakuwa kwenye gubu. Alikula kiapo asilani hatochangamana na Lowassa na team yake. Ni Tundu aliyepinga kwa namna yoyote ile Raisi wa nchi kusafiri nje ya nchi kiasi cha kumuita JK mtalii. Aliamini kuwa ili nchi inufaike na rasilimali ni lazima mikataba ivunjwe bila kusita kwani aliamini Barrick, wamiliki wa vitalu vya uwindaji n.k wanaiba hivyo wataifishiwe. Alitumia vema jukwaa la Leat kufikisha ujumbe wake.
Tundu (2022) ni mwenye unyenyekevu mkuu wa wazungu na wanyonyaji, pia yupo radhi kutoa ushirikiano kwa maadui wa taifa ili tushindwe. Anaamini bila wazungu yeye na wenzake hawawezi kushika dola. Yupo radhi nchi iingie machafuko ili wapate fursa ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa ili na yeye siku moja awe kiongozi wa serikali.
Hakika, orodha ni ndefu lakini kama ikatokea Tundu (2014) akikutana na Tundu (2022) 'watauana'.
Nitaendelea kuwaletea Mbowe, Lema, Msigwa nk wa mwaka 2014 jinsi watakavyogombana na wale wa mwaka 2022.
Karibuni