SUNDERLAND FOOTBALL CLUB 1960s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,978
30,324
SUNDERLAND FOOTBALL CLUB 1960s

Picha hizi nikiziangalia leo zinanikumbusha udogo wangu nikienda Ilala Stadium kuangalia mpira.

Wengi katika wachezaji hawa wametangulia mbele ya haki na baadhi wachache bado wako hai.

Katika ujana wangu miaka ya 1970 nilikuja kuwajua baadhi ya wachezaji hawa wengine wakawa wazungumzaji wangu wa karibu sana.

Wengi wao wakishangazwa jinsi nilivyokuwa nawahadithia historia zao wenyewe wakati wa uchezaji wao.

Siku ya maziko ya Athmani Kilambo nilipata fursa ya kuzungumza na Hamisi Kibunzi mchezaji wa Sunderland.

Nikamweleza kuwa Athmani Kilambo akimsifia sana uchezaji wake kama halfback kwa stamina na staili ya kusukuma mipira mbele golini.

Nikaendelea kumweleza kuwa pamoja na yeye Kilambo akimuusudu sana Arthur Mambeta.

Arthur yeye alikuwa hodari wa kupangua walinzi na ball control ya kutisha kiasi mlinzi hawezi kuchukua mpira kwenye miguu ya Arthur.

Nikamwambia kuwa Kilambo alikuwa akitamani sana kama Kibunzi na Mambeta wangeletwa Young Africans kuja kuongeza nguvu.

Kilambo akamaliza mazungumzo yake kwa kuniambia kuwa suala la wachezaji hawa lilikuwa gumu kwa President wa Yanga Mangara Tabu kulipa uzito kwa kuwa yeye Kilambo akimwambia Mzee Mangara kuwa Kibunzi na Mambeta wana mapenzi makubwa sana na Sunderland wakija Yanga hawataweza kucheza mpira kama wanapokuwa wamevaa zile jezi nyekundu za Sunderland.

Kilambo akipenda sana kunambia kila tukizungumza, "Wale watoto wakipenda sana Sunderland wasingeweza kucheza mpira Yanga."

Hamisi Kibunzi alishangaa sana kwani hakuwa anajua kuwa Young Africans wakimtaka.


 
Waqt huo mpira ulichezwa na wanamume wa shoka mahaba makubwa kwa timu zao ujira mdogo sana wakipatiwa nafasi za kazi kama bandarini au posta waliridhika
 
huyu Kilomoni ndio huyu mzee kilomoni anaye piga kelele pale msimbazi?
 
huyu Kilomoni ndio huyu mzee kilomoni anaye piga kelele pale msimbazi?
Chillah,
Ndiye yeye Hamisi Kilomoni.
Alikuwa mlinzi makini sana.

Ilikuwa wakati mwingine Sunderland wakimchezesha kama mshambulizi.

Mara nyingine kama Sunderland imeelemewa inataka iapte goli au irudishe goli na muda unayoyoma mara utamuona Kilomoni yuko mbele na goli linapatikana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom