Sumu ya ubaguzi wa udini ni mbaya kuliko tunavyoifikiria

Jan 24, 2012
32
21
Wapendwa watanzania wenzangu,imefika sasa tuseme basi kuhusu kuendekeza mijadala ya udini,maana hapo zamani tulikuwa hatuwezi kuongea maswala ya ubaguzi wa udini hata mbele ya watoto zetu,lakini sasa hivi hili neon udini kila kitu kinapongelewa chenye maslahi ya jamii au kila kosa linalotokea kwenye jamii tunaelekeza UDINI kwanza kama ndio chanzo badala ya kuangalia nini hasa kiiini cha tatizo.Leo nimesoma gazeti linajaribu kuelezea matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na uhusiano wa UDINI.Watanzania inapaswa tujue kwanza hizi dini zinazotusumbua sisi leo zilitukuta sisi watanzania tukiwa na njia zetu za kuabudu na tulikuwa tukiishi kwa amani na upendo,tofauti zetu za wakati ule zilikuwa kati ya mfugaji na mkulima ambazo mpaka sasa bado zinasumbua.Hata wale walioleta dini hizi hawakuwa na nia mbaya ya kutugawanya kama tunavyojigawa sisi leo,wao waliongelea zaidi kuhusu upendo na kuiga staarabu za kwao ambao wao waliziona nzuri kuliko zetu.Na kitu muhimu kukumbuka hizi dini zote zilitokea sehemu moja na ndio zikaennea na kugawanyika kutokana na utawala wa kila mtu alivyokuwa akifikiria ni sahihi.ukitaka kujua kirahisi kabisa angalia vazi linalotumiwa kama vazi la heshima kwa kuabudu(KANZU).Wapendwa Watanzania hakuna vita ngumu na isiyokuwa na mwisho kama tutapandikiza tofauti zetu za imani katika maisha yetu,watoto wetu na wajukuu.kwa umaskini huu tulionao wakushindwa kununua hata net ya mbu je tukiingia katika vita hiyo tutaweza hata kuvaa hata hizo KANZU?Binafsi vuguvugu hii ya UDINI imeshika kasi sana baada ya viongozi na wanasiasa wakubwa katika nchi walipoanza kuitoa katika vinywa vyao,hapo mwanzo ilikuwa ngumu sana kumsikia kiongozi yoyote Yule anataja kitu kama hicho mbele ya uma.Sasa imekuwa neno la kawaida kuandikwa na kutamkwa mbele ya kadamnasi.wapendwa maneno huwa yanatabia ya kuingia kichwani na kujenga taswira,na yakishajenga taswira kinachofuata huwa nikutelekeza taswira hiyo katika uasilia.Watanzania tuna makabila zaidi ya 100,na kila kabila lina dini tofauti ndani yake,je yakitokea hayo tunayoyasema kila siku tutabaki na kabila zaidi ya 300.Ushauri wangu kwa Serikali na viongozi wote wa serikali na dini zote,ni wakati sasa wakurudisha imani na upendo tuliokuwa nao tangu enzi zetu,JE YULE KIJANA ALIYEANDIKA MISTARI YA BONGO FLEVA KWENYE MTIHANI WAKE NAYE NI UDINI?
Huo ni mtazamo wangu.
 
Back
Top Bottom