ashidodi
JF-Expert Member
- Sep 4, 2016
- 291
- 341
Poleni na majukumu wana jamii wenzangu,
naomba kufahamishwa zaidi kwa hiki ambacho nimezoea kukiona bila kukifuatilia kwa undani, maziwa huzuiaje madhara ya sumu mwilini?
Nawasilisha
MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
Sent using Jamii Forums mobile app
naomba kufahamishwa zaidi kwa hiki ambacho nimezoea kukiona bila kukifuatilia kwa undani, maziwa huzuiaje madhara ya sumu mwilini?
Nawasilisha
MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
Ni kwa namna gani MAZIWA hufanya kazi kupunguza makali ya sumu mwilini ?
Katika ukurasa wangu huu nitakua nikizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu mambo kadha wa kadha yanayohusu mifugo/wanyama, ufugaji na wafugaji. Nitaelezea masuala kadhaa yanayohusu, historia, tamaduni, tabia, teknolojia na mambo ya kustaajabisha ya mifugo na mazao yake hali kadhalika wafugaji.
JE, MAZIWA YANAFANYAJE KAZI KUPUNGUZA SUMU ? JE, YANAPUNGUZA UWEZO WA DAWA MWILINI ?
Maziwa ni kimiminika cheupe ambacho huzalishwa kutoka kwenye kiwele cha mamalia jike kwa ajili ya chakula cha mtoto wake mara baada ya kuzaa.
Maziwa dhidi ya sumu, dawa na pombe;
Kwa asilimia kubwa maziwa ni protini, umbo la protini linaweza kuharibiwa (protein denaturation) kwa joto, pombe, asidi, besi au chumvi ya metali nzito (salts of heavy metals).
Asilimia kubwa ya sumu zilizopo ni chumvi za metali nzito hasa Mekyuli/Zebaki na Fedha (Lead). Unapokua umekunywa sumu za aina hiyo kisha ukanywa maziwa, metali zilizopo kwenye sumu zitakwenda kwenye maziwa kuchanganyikana ili kuiharibu protini iliyopo kwenye maziwa. Kwa kufanya hivyo kiwango cha sumu amabacho kingeudhuru mwili kinapungua (badala ya sumu kuudhuru mwili inayadhuru/inachanganyikana na maziwa). Kutilia mkazo nizungumze kakimombo hapa “the poison acts on the protein in milk rather than on the proteins of various body parts”
Baada ya hapo mtu anatapika ili kuondoa sumu iliyochanganyika kwenye yale maziwa.
Kwa upande wa dawa (ambazo ndani yake kuna asidi,besi au matali nzito) na pombe, maziwa yanapunguza nguvu ya dawa na pombe hiyo kwa kuifanya dawa IYATIBU maziwa na pombe KUYALEWESHA maziwa kuliko mwili au mtu.
Ukiamua kunywa sumu basi fanya hivyo siku amabayo ni zamu yako kukamua na ukiwa baa usimchekelee muuza maziwa utapata hasara.
“RAHA YA BIERI (BIA) KULEWA”
Credit; Kwa Jamaa Fulani Facebook
Sent using Jamii Forums mobile app