SUMTRA Ifungie mabasi ya Green Star

SUMTRA Ifungie mabasi ya Green Star

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
4,225
Reaction score
869
Wakuu,

Naomba nilisema hili na tusaidiane.

Kuna mabasi yanaitwa Green Star ambayo yanafanya safari zake kila siku kati ya Dar-Mz lakini yamekuwa ni tatizo kubwa sana kwa abiria wake.

Haya mabasi yamekuwa yakiharibika mara kwa mara njiani wakati wa safari hali ambayo inawasababishia abiria usumbufu mkubwa ambapo wamekuwa wakifika mwanza ama Dar usiku wa manane wakati mwingine saa sita,saba,nane ama tisa.

Kibaya zaidi wakati mwingine abiria wamelazimika kubadilishiwa gari wakiwa njiani kutokana na Green Star kuharibika,cha ajabu kuna wakati mabasi haya yanaondoka yakisuasua Ubungo ama Mwanza na abiria wanapohoji wanaambiwa hakuna tatizo na baada ya mwendo wa kama masaa mawili ama matatu tatizo linajidhihirisha na safari inaishia hapo wabiria wanaanza kuhangaika.

Wanafanya hivyo ili kuwaondoa abiria kwenye kituo cha basi kwa sababu wanaamini kwamba wakiendelea kuwaacha pale stendi kuna trafic na watu wengine ambao wanaweza kuwawajibisha ama kuwapigia kelele,hata juzi tu liliharibika Manyoni na abiria walika hadi usiku,kwa kifupi mabasi haya yansumbua sana abiria swali la kujiuliza hapa ni kwanini mambo haya yote yanafanyika huku wapo na wanaangalia tu,au labda ni ya kigogo fulani jmani hebu tusema kwa sababu ni ngumu kwa abiria anayesafiri nayo kwa mara ya kwanza kubaini hali hiyo,lakini mtu kama mimi ambaye yameshanikuta zaidi ya mara 10 njiani siwezi kuyapanda tena.
 
NAFIKIRI NI BUSARA ILA KABLA AYAJAFUTWA NAKUSHAURI ULETE MABASI YAKO KUYAREPLACE YAWE KM THELATHINI IVI TENA MAPYA NA YAWE SCANIA MARCOPOLo
 
NAFIKIRI NI BUSARA ILA KABLA AYAJAFUTWA NAKUSHAURI ULETE MABASI YAKO KUYAREPLACE YAWE KM THELATHINI IVI TENA MAPYA NA YAWE SCANIA MARCOPOLo

Wee kichaa inaonekana una share kwenye haya mabasi ninyi ndo tunaowatafuta kwa sababu mnawafisadi wananchi na nchi kwa ujumla,nonsense.
 
wanakimbia sana, safari za kahama na mwanza ni ndefu zinahitaji mabasi imara na sio youtong ya kichina yale ya greenstar, wiki ile nilipanda toka mwanza, tairi lilipasukia njiani, al manusura, tunashukuru Mungu. safari za mbali hizo zinahitaji ndege wala si mabasi haya. ukiangalia mabasi ya kanda ya ziwa toka dsm ni mabovu sana, hata sumri karibia anakufa. ni kwasababu ni mbali mno kupeleka basi kule linakufa mapema kabla hujapata faida, hivyo unaenda kwa kubangaiza tu ivoivo au la panda ndege. ukiangalia mabasi ya mbeya songea iringa, arusha moshi etc ni mazuri ya kisasa kuliko ya mwanza kahama anakoenda green star na hao wengine, kwasababu maeneo hayo nimetaja ni mafupi kuliko kahama/mwanza.
 
wanakimbia sana,
safari za kahama na mwanza ni ndefu zinahitaji mabasi imara na sio
youtong ya kichina yale ya greenstar, wiki ile nilipanda toka mwanza,
tairi lilipasukia njiani, al manusura, tunashukuru Mungu. safari za
mbali hizo zinahitaji ndege wala si mabasi haya. ukiangalia mabasi ya
kanda ya ziwa toka dsm ni mabovu sana, hata sumri karibia anakufa. ni
kwasababu ni mbali mno kupeleka basi kule linakufa mapema kabla hujapata
faida, hivyo unaenda kwa kubangaiza tu ivoivo au la panda ndege.
ukiangalia mabasi ya mbeya songea iringa, arusha moshi etc ni mazuri ya
kisasa kuliko ya mwanza kahama anakoenda green star na hao wengine,
kwasababu maeneo hayo nimetaja ni mafupi kuliko kahama/mwanza.

Musoma Express kwa waliwahi kusafiria watakubaliana na mm, Lake zone yote hakunaga.
 
Nina wasiwasi KASHORO umeambukiza laptop yangu virusi kwa mashudu unayoongea..kalagabaho
 
kashoro ana hangover ya mnazi + viroba c akili yake msameheni bure
 
SUMATRA wako DSM tu, huku mikoani hata nauli na trafic nao ndiyo kabisa na hawasimamii hawa, huku madongo kuinama tunabamizwa nauli, hatuna mtetezi
 
Green Star ni untouchable wewe!
Hakuna mtu mwenye jeuri ya kuyasimamisha!
Route za kusini wanajaza watu hadi kusimama, lakini Sumatra wanawaruhusu, wakati mabasi mengine wanatozwa 250,000/= onspot.
Chezeya Bunge wewe!
 
Wabheja sana,

Unachokisema ni kweli kabisa, mimi ilinitokea live kama miezi 6 iliyopita, sita kaa nisahau. Nikiwa kwenye basi, na kabla ya kufika kibaha baada ya kuhisi kuna tatizo kubwa na basi hilo, nilimpigia trafik mwenye cheo cha juu pale Ubungo, nikamtaarifu awambie vijana wake pale Kibaha mzani walisimamishe basi hilo wamhoji dereva, conductor na abiria wasikie watakacho ambiwa, jamaa alikubali ombi hilo lakini hakuna alichofanya.

Tatizo sio wamiliki wa mabasi hayo, tatizo ni wasimamizi wa utaratibu pamoja na watawala,

Hii inamaanisha nini basi, tatizo ni ukosefu wa umakini ndani ya vitengo vya serikali ya CCM, kwa hiyo tatizo kuu kabisa ni CCM

Utapiga kelele mpaka utachoka, hayo mabasi yataendelea kudunda barabarani, mpaka hapo mojawapo litakapodumbukia mtoni ndio angalau watawala watashituka kidogo.

Japo watasema, taili la mbele lilitobolewa na kitu kizito chenye ncha kali........ kama kawaida yao
 
Green Star ni untouchable wewe!
Hakuna mtu mwenye jeuri ya kuyasimamisha!
Route za kusini wanajaza watu hadi kusimama, lakini Sumatra wanawaruhusu, wakati mabasi mengine wanatozwa 250,000/= onspot.
Chezeya Bunge wewe!
Unaikumbika Scandnavia Express? (ScExp = Green Star) Unajua mmiliki na alipata wapi mapesa ya fasta akawa untouchable kila mahali anakiuka utaratibu na kujenga vituo binafsi hata ndani ya vituo vikuu kama Ubungo? Ukilijua hilo utajua kwanini SUMATRA hawawezi sema kitu wala traffic police. Period.
 
SUMATRA wako DSM tu, huku mikoani hata nauli na trafic nao ndiyo kabisa na hawasimamii hawa, huku madongo kuinama tunabamizwa nauli, hatuna mtetezi

hao SUMATRA hawapo kikazi wapowapo 2 MBONA TRENI YA MWAKYEMBE UBUNGO STATION HAINA LECEN NA WANA WANA BEBA ABIRIA MAKA IUWE NDIO SUMATRA WATASEMA KUA HATA SISI TULIWANYIMA LECEN LIKINI WATU WAMEISHA KUFA WAKATI HUO...HIYO NDIO TANZANIA MAISHABORA KWA KILA MTU.....
 
chezea riz1 weye.. nchi iko mikononi mwa walaji mkuu,kwa ushauri pandeni mengine bangosha.
 
NAFIKIRI NI BUSARA ILA KABLA AYAJAFUTWA NAKUSHAURI ULETE MABASI YAKO KUYAREPLACE YAWE KM THELATHINI IVI TENA MAPYA NA YAWE SCANIA MARCOPOLo

Acha umaandazi ww!! Yaani kila mara tunanyanyasika road then unaongea pumba km hizooo!!!!!!!
 
Mabasi ya kichina hayo, MARCOPOLO moja unanunua YUTONG tatu nne hivi unategemea nini? Niliwahi kuambiwa kuwa mzee wa kulia mjengoni ana mkono wake hapo, kama ni kweli basi inawezekana SUMATRA watakuwa wanaogopa ugomvi na BOSS!
 
wanakimbia sana, safari za kahama na mwanza ni ndefu zinahitaji mabasi imara na sio youtong ya kichina yale ya greenstar, wiki ile nilipanda toka mwanza, tairi lilipasukia njiani, al manusura, tunashukuru Mungu. safari za mbali hizo zinahitaji ndege wala si mabasi haya. ukiangalia mabasi ya kanda ya ziwa toka dsm ni mabovu sana, hata sumri karibia anakufa. ni kwasababu ni mbali mno kupeleka basi kule linakufa mapema kabla hujapata faida, hivyo unaenda kwa kubangaiza tu ivoivo au la panda ndege. ukiangalia mabasi ya mbeya songea iringa, arusha moshi etc ni mazuri ya kisasa kuliko ya mwanza kahama anakoenda green star na hao wengine, kwasababu maeneo hayo nimetaja ni mafupi kuliko kahama/mwanza.
yaani badala ushukuru mepona na deleva alikuwa makini ww unataka yafungiwe acha ushamba ww kwani mataili ni ya chuma yale yasipasuke panda trini basi
 
Hata hizi PRINCE MURO, nazo zishakua vimeo na mbaya zaidi hawa jamaa wanajifanya wanaharaka
ile mbaya, ni juzi kati nikiwa naelekea Mz,kuja kufika Singida limeharibika mara tatu, kilichofuatia ni
kupanda gari nyingine kwa garama nyingine................................... inauma lakini!
 
Back
Top Bottom