Sumaye usilalame, leta malalamiko-Mukama

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
4,803
1,416
"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakiwezi kutoa maoni yoyote juu ya kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kwamba chama hicho kinaandamwa na rushwa mpya za kimtandao, kwa kuwa kauli hiyo siyo rufaa wala malalamiko yaliyowasilishwa naye kwenye chama dhidi ya uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho.

Mukama alisema hayo alipotakiwa na NIPASHE jana kutoa maoni ya CCM baada ya Sumaye kutoa kauli hizo katika mkutano na waandishi wa habari, ulioitishwa naye (Sumaye) jijini Dar es Salaam juzi.

“Hayo ni maoni yake. Siyo rufaa wala malalamiko,” alisema Mukama kwa kifupi.

Alisema CCM ni chama kikubwa, ambacho Tanzania Bara kina wilaya 149 na Zanzibar kina wilaya 12, hivyo hakiwezi kutoa maoni yanayotolewa na kila mwanachama kama hatakuwa amekata rufaa au kulalamika katika chama.

Hata hivyo, Mukama alisema kama waandishi wa habari wataona kauli zilizotolewa na Sumaye dhidi ya CCM kuwa ni za kweli, basi wafanye uchunguzi badala ya kuzimeza nzima nzima, kwani kuna kanuni ambayo inamzuia mtu kuzungumza kama hajafanya utafiti (uchunguzi). " end

Kama huyu aliyesema haya ndiye katibu mkuu wa CCM, basi Chama hiki kimefilisika. Huyu jamaa ndiye aliyekuja na fikra za kujivua GAMBA? Mukama ndiye aliyetakiwa kutoa barua kwa MAFISADI? leo hii anasema haya?

Mhe. Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, usifikiri wewe ndo msafi sana kuliko hao wenzako, kwa kuwa umepigwa chini ndo unalalamika, ungeshinda ungesema hayo yote??? Acha unafiki!
 
Chama chetu cha Mapinduuuziii chajenga nchiiii
Mafisadiii aaa,Magamba yajenga nchi
wanafikiii aaaaa,wala rushwa wajenga nchiii!

nimekimbia naogopa bomu la machozi au risasi ya tumbo!!
 
Mhe. Waziri Mkuu Msafafu, Fredrick Sumaye, usifikiri wewe ndo msafi sana kuliko hao wenzako, kwa kuwa umepigwa chini ndo unalalamika, ungeshinda ungesema hayo yote??? Acha unafiki!

Au kwa sababu mwiba umemchoma yeye ndo maana ametoa mapovu?? Rostam yeye alishtuka akaamua kuachana na siasa za majitaka. Karibuni fruit salad bana..

fruit-salad-500x500.jpg
 
Sumaye ameingia choo cha kike apumzike siasa awaachie vijana....

Anakula pension hadi atakapokufa na ni waziri Mkuu mstaafu aliyekaa muda wa miaka 10 kwa nini asibaki na heshima ya kuwa mshauri wa chama???

Anakimbizana na akina Mary Nagu kwenye NEC akibwagwa ni aibu.
 
"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakiwezi kutoa maoni yoyote juu ya kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kwamba chama hicho kinaandamwa na rushwa mpya za kimtandao, kwa kuwa kauli hiyo siyo rufaa wala malalamiko yaliyowasilishwa naye kwenye chama dhidi ya uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho.

Mukama alisema hayo alipotakiwa na NIPASHE jana kutoa maoni ya CCM baada ya Sumaye kutoa kauli hizo katika mkutano na waandishi wa habari, ulioitishwa naye (Sumaye) jijini Dar es Salaam juzi.

"Hayo ni maoni yake. Siyo rufaa wala malalamiko," alisema Mukama kwa kifupi.

Alisema CCM ni chama kikubwa, ambacho Tanzania Bara kina wilaya 149 na Zanzibar kina wilaya 12, hivyo hakiwezi kutoa maoni yanayotolewa na kila mwanachama kama hatakuwa amekata rufaa au kulalamika katika chama.

Hata hivyo, Mukama alisema kama waandishi wa habari wataona kauli zilizotolewa na Sumaye dhidi ya CCM kuwa ni za kweli, basi wafanye uchunguzi badala ya kuzimeza nzima nzima, kwani kuna kanuni ambayo inamzuia mtu kuzungumza kama hajafanya utafiti (uchunguzi). " end

Kama huyu aliyesema haya ndiye katibu mkuu wa CCM, basi Chama hiki kimefilisika. Huyu jamaa ndiye aliyekuja na fikra za kujivua GAMBA? Mukama ndiye aliyetakiwa kutoa barua kwa MAFISADI? leo hii anasema haya?

Mukama anataka sumaye naye athibitishe kwanini Dr. Slaa haamini kupeleka malalamiko kwa magamba.
 
Naam, angalau Sumaye anajitambua na kukitambua chama chake "kinachonyooshea mambo wafanya biashara". Na anaujua vizuri mchezo unaochezwa humo. Kwa mtaji huo, kasema kweli kusema hawezi kuhama chama wala kupeleka malalamiko popote baada ya kuzidiwa dau. Ajabu ni kule kuitisha "press conference" ili kupayuka kilicho dhahiri.
 
Kuhamia upinzani si kosa la jinai, ni utashi wa mtu binafsi, Hamad alikuwa waziri kiongozi ZNZ sasa yuko CUF, japo ni aibu kwa Sumaye kuhamia upinzani (akiwa waziri mkuu mstaafu) akiona dhamira haimshtaki ruksa tu aende upinzani. JK kasema 'anayetaka kuhama ahame, sio kuwa na ndimi mbili' mtu akishinda uchaguzi 'CCM oyee'...akishindwa 'CCM inanuka rushwa'...nonsense!!??
 
Aende upinzani akafanyaje? ameshakuwa W/M inatosha akalime mashamba yake, apishe wengine, uroho wa ving'ora utamtokea puani
 
Huyu Mukama anawaza kwa kutumia kiungo gani cha mwili? Hivi ni kazi ya Sumaye kutaja watu waliotoa na kupokea rushwa au ni kazi ya Takukuru na vyombo vya usalama vya ccm gamba? Wanaolipwa mishahara kwa kodi za wananchi? Kwanini hizi taasisi ziwepo kama hazifanyi kazi?
 
Mukama amejibu vizuri sana.

Mtu anapiga mayowe barabarani huw hajibiwi unless apeleke malalamiko rasmi.
 
Kinachomuuma Sumaye ni kwamba ameumbuka!

Mimi ningekuwa Sumaye ningetulia tuli nisingetaka siasa tena.

Sijui nani alimdanganya kama na yeye ni heavy weight!

Aiubu imempata mzee mzima sasa anawayawaya.
 
Nahisi CCM wamepanga kumzima SUMAYE kisiasa sababu huyu jamaa tangu astahafu sijasikia kupewa vyeo vingne kama walivyo wengne sumaye amekuwa kimya sana me najiuliza huyu jamaa wanampango gani naye CCM me najua CCM ni watu wakupeana lakini SUMAYE wanamtosa me naona ni mwaka mbaya kwake atafute mbinu mbadala ya kurudisha Heshima yake na Umaarufu wake
 
Ni sawa na demu wako akiwa pros.. halafu kila siku unalalamika tu ooohh demu wangu hivi wakati bado unae. Watu si watakushangaaa. Ndio hii ya Sumaye.

Tatizo wanaojidai wapiganaji humu CCM nao ni walewale ndio maana wanaogopa kutoka.
 
Nimependa hii ya kumfananisha Mh Sumae na demu, lakini unajua ni baba wa watu?
 
Back
Top Bottom