Sumaye usigeuze CHADEMA kichaka cha UFISADI wa ardhi.

Sumaye usigeuze CHADEMA kichaka cha UFISADI wa ardhi.

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
"Kama mtu ukijua majukumu na mipaka yako utakuja kubaini kuwa hiki ninachokifanya mpaka mpaka wake ni huu na mwisho wake huu"

Maneno hayo ya utangulizi yametolewa na Mbunge wa Hanang' Dk Mary Nagu alipokuwa akirudisha na kukabidhi shamba lake la heka 12,000 kwa Halmashauri ya Hanang' mkoani Manyara baada ya kushindwa kuliendeleza.

Lakini si Mary Nagu pekee ambaye alitakiwa na Serikali kurudisha shamba kwa kushindwa kuliendeleza, Philipo Marmo - Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Kipi Warioba nae ametakiwa kurudisha hekari 4000 anazomiliki eneo la Mperamumbi pamoja na Mohamed Dewji mmiliki wa Mohamed Enterprises Tanzania Limited aliyetakiwa kurudisha shamba la mkonge analolimiliki mkoani Lindi. Watajwa hapo juu ni wanachama wa CCM, makada waaminifu kwa Chama na Serikali, lakini uanaCCM wao na vyeo vyao haviwakingi na sheria za nchi.

Sumaye - Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alipotakiwa kurudisha shamba ambalo haliendelezi mabwepande, amesikika akitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa Serikali ya CCM inamnyang'anya mashamba yake ili kumshawishi ama kumlazimisha arudi kuwa mwanachama wa CCM. Akiwa anajua kuwa ni sheria wala sio U-CHADEMA wake unaomfanya anyang'anywe ardhi hiyo.

Ni bahati mbaya sana kwa wananchi wa nchi hii kuwahi kuwa na Viongozi wanafiki kwa kiwango hiki. Ikiwa mafisadi wa aina zote walikimbilia chadema wakidhani itakuwa ndio salama yao kwa kuwa watageuza kila jambo kuwa ni sehemu ya siasa za upinzani, nadhani wamekosea sana.
 
Chadema ni chama cha madalali....kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake.
 
Wanapaswa na wanao wajibu wa msingi kabisa kupinga jambo hilo. Nitawashangaa kama nilivyokuwa nawashangaa hapo kabla wakilishabikia na hili na kulitungia nyimbo.
Ndugu yangu TandaleOne , chama kikishageuzwa kuwa kichaka cha majambazi hakika kinapoteza uwezo wa kukemea ufisadi. Ni sawa na kijiji ambavho wananchi wake wote wanajisaidia kichakani ama ziwani. Hakuna mtu atakayejitokeza kukemea kitendo hicho kwa vile ni kawaida ya wananchi wote wa eneo husika
 
Chadema ni chama cha madalali....kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake.
Mkuu samahani jana nilisoma sehemu kwamba mkuu wetu wa nchi ataongea na vyombo vya habari hizo taarifa ni za kweli?? na kama ni kweli itakuwa saa ngapi?? Heshma yako.
 
Ukipakua uchafu wa chooni ukauingiza chumbani kile chumba kitageuka choo na kile choo hakitanuka tena alisema DR SLAA mafisadi walipo ingia chadema
 
kwani amekuwa yule Mh wa bukoba pesa za mboga.



swissme
Alikuchukulia bwana nini make kati ya wanaosemwa huyu mama unamsema kweli kweli, kana kwamba kwako wewe kama si yule mama basi Tz yooote ni safi.

Pole sana swiss me
 
Alikuchukulia bwana nini make kati ya wanaosemwa huyu mama unamsema kweli kweli, kana kwamba kwako wewe kama si yule mama basi Tz yooote ni safi.

Pole sana swiss me
ukweli unauma


swissme
 
Sumaye anajikanyaga. Mimi nilitegemea akanushe kuwa hana Shamba analolimiliki na ameshindwa kuliendeleza. Haya ya U-Chadema na U-CCM anajidhalilisha.
Ndio mjumbe wa Kamati Kuu anayetegemewa kukishauri chama na kukipa miongozo....
 
Ukipakua uchafu wa chooni ukauingiza chumbani kile chumba kitageuka choo na kile choo hakitanuka tena alisema DR SLAA mafisadi walipo ingia chadema
Amesema kweli Dr Slaa.
 
Ninachoamini, Hivi vyama vimeweka wachumia tumbo wengi mno, ndio maana hata humu watetezi wa vyama ni wengi.
 
Back
Top Bottom