Sumaye: Tujitahadhari 'wauza unga' wasije wakaongoza nchi

Sumaye: Tujitahadhari 'wauza unga' wasije wakaongoza nchi

Huyu kigogo mstaafu naanza kuamini kuw akuna kitu anakifahamu juu ya hii biashara haramu na hatari , na pia kuna kitu anakinyemelea (vr vital), ngoja tuzid fatilia mwenendo wake na matamko yake , then muda mwafaka ukifika tutathibitisha yale ayasemayo.
 
Serikali ya ccm bwana, kila anayetoka anaona matatizo ya waliopo. Japo bwana mkubwa alisema anawajua wauza unga lakini naye hajawataja, kwa kifupi biashara ya dawa za kulevya itaendelea kustawi kwa utawala huu wa ccm
 
Cha ajabu nikuwa, akikamatwa mtu mdogo na gari la wizi, watatafuta up direction mpaka wampate nguli wa mambo hayo... Lakini suala la madawa, mateja wanawafahamu tena wengine wanakutana na raisi (e.g RAY C), kwa nini wasianze na hao mateza mpaka wakawafikia manguli wa shughuri hii..??? Hii inaonyesha kuwa wakubwa a.k.a vigogo wa nchi hii ndo wafanya biashara wakubwa wa madude hayo... NA HAYA MADUDE YANAKOTUPELEKA NI KUKABIDHI BANDARI ZOTE KWA WACHINA... Kwani nani asiyependa kumuokoa mtoto wake toka kwenye kifo..??


Anza na Teja wapi anapata Kete then wakala kisha Maboss then wasafirishaji na mwisho kabisa unakotengenzwa.
Simple n clear. Cha kushangaza, Teja wanakwenda mpaka Ikulu sijui haulizwi swali hilo? Mbaya zaidi kuna watu wameaanzisha Rehab Centre! Yaani muuze madwa ya kulevya nyinyi kisha muaanzishe vituo vya mateja nyinyi. Kweli biashara ni kuzungusha akili kwenye akili. Munatengenezeana ajira tu kupitia Uchafu huo. Suruhisho ni kutokuingizwa kwa madawa ya kulevya nchini.
 
Ndiyo maana ya kauli ya Sumaye kwamba hizo pesa nyingi anazozitoa kwenye misikiti na makanisa pamoja na rafiki zake ni pesa za biashara ya unga.

kama ni kweli pesa hizo ni za unga, sio muda mrefu tutasikia makanisa na misikiti wanazirudisha kwa Lowasa kwa sababu ni pesa zilizopatikana kwa njia isiyostahili, hahhahahh!
 
Hii ni ajabu kweli, yaani nchi yetu kila mmoja analalamika? nani mwenye kuchukua hatua sitahili kuondoa hawa watu? siamini kwamba mtu kama Sumaye Waziri Mkuu mstaafu anaweza akatoa kauli kama hii bila ushahidi! ni kwa nini sasa mtu kama huyu asiweke majina ya hao watu hadharani na watanzania wawaepuke wasije wakawachagua? Nani mwenye kufunga paka kengele?!!! Tuna shida kubwa hapa
 
Huu ujinga wa kuogopa kutajana utaisha lini? Hivi huyu Sumaye asipowataja hao wauza, unga mpiga kura atawajuwaje? Na akiwachaguwa na huku hakujajiwa watamlaumu nani..???

Hebu cheki
1. Raisi alisema anawajuwa wae wezi wa bandari..... HAKUWATAJA
2. Raisi anawajuwa waliorudisha fedha za EPA.... HAKUWATAJA
3. Alisema akiwa kanisa la RC jimbo la Mbinga kuwa anawajuwa wauza unga..... HAKUWATAJA
4. Nape alisema anawajuwa magamba na akawapa siku tisini .... HAKUWATAJA
5. pinda alisema bungeni, Meremeta watatikisa nchi.... HAKUWATAJA
6. Sumaye naye anataka tusiwachague wauza unga kuwa viongozi.... HAJAWATAJA
7. Wanasemasema tu kuwa uchaguzi wa ndani ya CCM mara zote huwa unagubikwa na rushwa.... HAWAWATAJI HAO WALA RUSHWA, LAKINI NA HAO WALA RUSHWA WANAENDELEA TU KUWA MADARAKANI

Tutabaki kutaka huruma ya wananchi kwa kujifanya tunawaonea huruma akina Ray C na wengine wakati waliowafikisha hapo HATUWATAJI

"Politic as a game has never had many fans unlike many games we know to exist in the world." Mi Maiself 2013
 
Sumae alikaa madarakani lakini hakufanya lolote, nashangaa eti ukiwa ndani husemi kitu! Ukiwa nje unasema,why? Kama sio unafiki. Lowasa 2015 hata kama. Sumae utakumbukwa kwa lipi? Uchu wa madaraka tu unakusumbua, hii nchi mmeifanya kuwa changudoa. Kila mtu akitaka anadonoa! When you think Right, think also left. I'm tired of your senseless words.
 
Fedha za wauza unga zishapokelewa makanisani, misikitini, walimu wamechukua chao, nk. Bado zitaendelea kugawa. Si unajua hadithi ya mfuga kuku na kuku? Sumae naye anautaka uraisi, alibanwa mpaka akashindwa kupita NEC. Hapo anamuonea gere EL tu, ndio wale wale
 
kwa nchi hii biashara ya unga inahusisha watawala wengi walioko madarakani, na hasa hii wamu ya nne, ndy imebariki biashara hii kwani hata mtoto wa mfalme ni mmoja wa vinara wa hyo biashara na ya pembe za ndovu. Na mpka sasa tunavyoongea inchi inaendeshwa na wauza unga kwa kiasi fulani. lazima tujiulize polisi anakamatwa na bangi, mwanajeshi na pembe za ndovu, hawa watu mpk wanaamua kufanya hivyo ni kwamba wanaona wakuu wao wakifanya hayo na hata mara nyingine kutumiwa wao kusafirisha kutoka mahali fulani mpk kungine. Tafakari we mtanzania tukifikia mahala nchi ikawa kma colombia au mexico tumekwisha.
 
LOWASA????????? hata kama si yeye hafai kuwa Rais wa Tanzania
 
kama ni kweli pesa hizo ni za unga, sio muda mrefu tutasikia makanisa na misikiti wanazirudisha kwa Lowasa kwa sababu ni pesa zilizopatikana kwa njia isiyostahili, hahhahahh!

Sio kweli makanisa yatarudisha kwani kuna baadhi ya wachungaji ndo ishu zao pia kwani hadi mkuu wa kaya alisema ana majina yao.
 
Mimi namuunga mkono sana Sumaye anayosema yanaweza kuwa na ukweli...ila nachochukia tu ni unafiki wa kutokutaja watu kila mtu anaishia kulalamika ....sijui kuna kaugonjwa gani kakushindwa kuataja...o
1. MWAKYEMBE WALIMNYONYOA NYWELE MPAKA KUCHA LAKINI HAKUWATAJA!
2. ULIMBOKA WALINGOA MENO NA KUCHA LAKINI HAKUWATAJA!
3. KIBANDA WALIVUNJA MENO NA KUTOBOA MACHO LAKINI HAKUTAJA!
4. SINA HAKIKA KA SAID KUBENEA ALITAJA!
5. ZITO ALISEMA ANAWAJUA WENYE MAPESA USWISI LAKINI HAJAWATAJA!
6. FREEMAN NAYE KASEMA WANAWAJUA WALIOTUPA BOMU LAKINI BADO KUTAJA
7. WANANCHI WENGINE WANAKAA MTAANI NA MAJAMBAZI LAKINI HAWAWATAJI!
8. SITAJI SITAJI SITAJI NDIO SYSTEM YETU SASA KWA STAILI HIYO TUTAFIKA KWELI

NB: NDIO MAANA SIKU ZOTE NAMKUBALI DR SLAA JEMBE LA UKWELI YEYE ALIWATAJA MAFISADI WOTE PALE JANGWANI NA SEHEMU NYINGINE...HUYU NDIE MZALENDO NA KIONGOZI ANAYESTAHILI
 
Wazo kichwani hua haliji bure, hadi kuconnect wauza unga na uongozi, na bado mtu kuongelea swala la uongozi na still ukawa na wazo la unga kichwani ni dhahiri kabisa kuna kitu unakijua na sio kusikiasikia tu mtaani, maana kiongozi safi kabisa hatofata ya mtaani tu, atayachunguza kwanza na kama kuna evidence basi anaweza akatoa comments. Huyu jamaa ni dhahiri anajua kua ni kweli viongozi wengi wanajihusisha na hizi mishe... Watu bna, hata hawajui kujificha, hahahahaha!!
 
Anayetakiwa kuwataja ni Rais mwnyew coz alitutangazia kuwa anawafahamu so tusitafune maneno..
hana nia ya kuwataja kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe na hataki sisi wananchi tuzijue sasa kama Sumai na yeye unaungana na Rais Kikwete kutuficha sababu za kutowataja basi wasubiri nguvu ya umma
 
Mimi namuunga mkono sana Sumaye anayosema yanaweza kuwa na ukweli...ila nachochukia tu ni unafiki wa kutokutaja watu kila mtu anaishia kulalamika ....sijui kuna kaugonjwa gani kakushindwa kuataja...o
1. MWAKYEMBE WALIMNYONYOA NYWELE MPAKA KUCHA LAKINI HAKUWATAJA!
2. ULIMBOKA WALINGOA MENO NA KUCHA LAKINI HAKUWATAJA!
3. KIBANDA WALIVUNJA MENO NA KUTOBOA MACHO LAKINI HAKUTAJA!
4. SINA HAKIKA KA SAID KUBENEA ALITAJA!
5. ZITO ALISEMA ANAWAJUA WENYE MAPESA USWISI LAKINI HAJAWATAJA!
6. FREEMAN NAYE KASEMA WANAWAJUA WALIOTUPA BOMU LAKINI BADO KUTAJA
7. WANANCHI WENGINE WANAKAA MTAANI NA MAJAMBAZI LAKINI HAWAWATAJI!
8. SITAJI SITAJI SITAJI NDIO SYSTEM YETU SASA KWA STAILI HIYO TUTAFIKA KWELI

NB: NDIO MAANA SIKU ZOTE NAMKUBALI DR SLAA JEMBE LA UKWELI YEYE ALIWATAJA MAFISADI WOTE PALE JANGWANI NA SEHEMU NYINGINE...HUYU NDIE MZALENDO NA KIONGOZI ANAYESTAHILI
wote hao wanafuata nyayo za mkuu wa kaya
 
Back
Top Bottom