Sumaye: Tujitahadhari 'wauza unga' wasije wakaongoza nchi

Sumaye: Tujitahadhari 'wauza unga' wasije wakaongoza nchi

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye wamewatadharisha Watanzania kuwa makini na watu wanaotaka Madaraka kwa kugawa fedha katika sehemu mbalimbali za nchi au majimboni akionya kwamba wanaweza kujikuta wakimweka madarakani kiongozi anayejihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

"Hivi kama mtu anaweza kuhonga sehemu kubwa ya wapigakura katika jimbo la uchaguzi au hata katika nchi kama nafasi anayosaka ni urais; tumeshajiuliza hizo fedha nyingi hivyo anapata wapi? Kama anajihusisha na biashara hizo chafu akipata nafasi hiyo watoto wetu watapona?" alisema Sumaye jana na kuongeza:

Haya ni maswali muhimu ya kujiuliza tunapoelekea mwaka kesho kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Alisema hayo mjini Morogoro kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata).

Akizungumza kwa tahadhari alisema haizungumzii Serikali yake iliyoko madarakani wala mtu yeyote, bali tabia mbaya, Sumaye alisema biashara ya dawa za kulevya inahusisha fedha nyingi na mitandao mipana ambayo isipodhibitiwa inaweza kulitumbukiza taifa katika janga.

Alisema Katiba Mpya siyo mwarobaini wa matatizo yanayolikabili taifa bali, utekelezaji na usimamizi wa sheria na kwamba jambo muhimu ni kuwa na Serikali itakayosimamia na kutekeleza sheria ili kulinda yale yaliyoelekezwa katika Katiba.

Katiba haiwezi kumzuia mwizi kwenda kuiba na sheria haitamzuia mwizi kwenda kuiba ila itatamka adhabu ya kupewa huyo mwizi. Kwa hiyo ili vyote hivi viwe na maana ni lazima awepo mtu au chombo cha kumkamata huyo mwizi na kumfikisha katika mikono ya sheria na chombo hicho ni Serikali. Kama haiwezi kufanya hiyo kazi kwa ukamilifu tutaishia kulalamika tu na maonevu na maumivu yataendelea kuumiza jamii.

Kwa hiyo hata Katiba iwe nzuri namna gani na ikatamka kuwa rushwa ni adui wa haki na hata ikatoa adhabu kali sana kwa kosa hilo; kama tutaweka viongozi madarakani kwa rushwa, hiyo Katiba wala haitatusaidia. Hivyo Katiba nzuri mpya lazima iambatane na Serikali safi yenye kusimamia masilahi ya umma. Huwezi kumweka madarakani mwenyekiti wa kijiji au diwani au mbunge au hata Rais kwa rushwa ya kuwanunua wapigakura halafu utegemee Katiba Mpya itajibu matatizo ya jamii.

Azungumzia Mviwata Sumaye alisema Mtandao huo wa Wakulima Wadogo Tanzania ndiyo unaojua tatizo la kilimo na shida zao na ndiyo unaotakiwa kuulizwa cha kufanya ili kilimo chetu kibadilike na mkulima afaidike...Kama hatuwahusishi na kuwashirikisha katika sera, mipango na programu za kilimo, basi tujue kuwa sera, mipango na programu hizo zitashindwa.

Alisema Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wengi wanategemea kilimo kwa maisha yao na uchumi wa taifa pia kwa kiasi kikubwa hutegemea sekta hiyo, lakini bado ni duni na hakijamkomboa mkulima mwenyewe wala uchumi wa taifa...

Nchi na watu wake bado ni maskini pamoja na kuwa watu wachapakazi wapo na ardhi kubwa na nzuri yenye rutuba ipo.Alisema suala la usindikaji wa mazao lazima lipewe kipaumbele vinginevyo kilimo hakitamwondoa mkulima katika umaskini.

Kama tutaendelea kuuza mazao ghafi ambayo bei yake katika masoko ya nje ni duni na haitabiriki, basi wakulima wetu na uchumi wa taifa letu vitazidi kudidimia. Mazao yaliyoongezwa thamani kwa usindikaji yanapata bei nzuri na usindikaji nao pia hutoa ajira kwa watu wetu.

Kwa mfano, badala ya kuuza pamba ghafi tubadilishe pamba yetu kuwa nyuzi na vitambaa, katani yetu iwe katika kamba na mazulia, chai na kahawa ziwe katika paketi za kutumia, matunda yasindikwe katika makopo na kadhalika. Kwa msaada wa Serikali yetu, Mviwata inaweza kabisa kufanya kazi hii ama peke yake au kwa kushirikiana na wadau wengine wa uwekezaji ili kujenga viwanda vya usindikaji mazao. Tusiisubiri Serikali peke yake haitaweza na tutajichelewesha.

MWANANCHI
 
Kama kweli Sumaye ameokoka awataje wauza unga vinginevyo na yeye anautaka urais
 
Huu ujinga wa kuogopa kutajana utaisha lini? Hivi huyu Sumaye asipowataja hao wauza, unga mpiga kura atawajuwaje? Na akiwachaguwa na huku hakujajiwa watamlaumu nani..???

Hebu cheki
1. Raisi alisema anawajuwa wae wezi wa bandari..... HAKUWATAJA
2. Raisi anawajuwa waliorudisha fedha za EPA.... HAKUWATAJA
3. Alisema akiwa kanisa la RC jimbo la Mbinga kuwa anawajuwa wauza unga..... HAKUWATAJA
4. Nape alisema anawajuwa magamba na akawapa siku tisini .... HAKUWATAJA
5. pinda alisema bungeni, Meremeta watatikisa nchi.... HAKUWATAJA
6. Sumaye naye anataka tusiwachague wauza unga kuwa viongozi.... HAJAWATAJA
7. Wanasemasema tu kuwa uchaguzi wa ndani ya CCM mara zote huwa unagubikwa na rushwa.... HAWAWATAJI HAO WALA RUSHWA, LAKINI NA HAO WALA RUSHWA WANAENDELEA TU KUWA MADARAKANI

Tutabaki kutaka huruma ya wananchi kwa kujifanya tunawaonea huruma akina Ray C na wengine wakati waliowafikisha hapo HATUWATAJI
 
UJI NGA mwingine, Biashara ya Unga imeanza awamu ya Nne? If no, Atutajie majina ya wauza unga wakubwa na mashuhuri ambao akiwa waziri mkuu walihukumiwa vifungo? Huyu Sumaye akiwa waziri mkuu, alizubaa mpaka Nkapa akauza kiwira, wizi wa EPA ukatokea na Ikulu iligeuzwa genge la Mafisadi, leo anajifanya mlokole. Kama alishindwa akiwa kijana mwenye nguvu, ataweza uzeeni?
 
Tujihadhari au tuwaondoe madarakani wauza unga. Magunia ya madawa yanakamatwa yakitokea wapi. Mbona wasanii ndiyo kipenzi cha familia nzima ya mtemi wa kaya. Wakifa michango ya nguvu Sumaye muongo saana. Ukiwa mwenye chongo usiifiche kwa mawani meusi. Na matokeo ya srrikali ya namna hii ni mabomu ya arusha, aache unafiki bado ameng' ang' ania huko. Aseme watanzania lazima wawaondoe wauza unga madarakani na anawajua
 
Sumaye ulikamata kiwanda cha unga kunduchi enzi hizo,kesi iliishia wapi? Sumaye huna usafi wowote wala hauuziki ktk urais
 
Kwa hili namuunga mkono Mr. Sumaye.

Kikwete amepewa majina yeye ameyakalia eti kwasababu wauza unga ni mojawapo ya viongozi wa serikali na wachangiaji wakubwa wa CCM. Madhara yake ndio hayo Sumaye kayaweka wazi. Soon inchi itakuwa inaoongozwa remotely na wauza unga kama ilivyo Mexico au Columbia.

Shame on you Kikwete>

CC: Ritz, Private Lukosi FaizaFoxy na other CCM Foxes out there.
 
Kwn EL na unga anauza pia?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwn EL na unga anauza pia?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Ndiyo maana ya kauli ya Sumaye kwamba hizo pesa nyingi anazozitoa kwenye misikiti na makanisa pamoja na rafiki zake ni pesa za biashara ya unga.
 
Kama ujasiri wa kutaja hadharani kila mtu angekuwa nao, basi ''wahuni'' wote wangekuwa na hali mbaya, yeye nyeusi huiita nyeupe.
 
Muasisi wa Takrima huyu. Aliishasema mfanyabiashara utafanikiwa uwapo na kadi ya Magamba
 
KWA UFUPI

Alisema Katiba Mpya siyo mwarobaini wa matatizo yanayolikabili taifa bali, utekelezaji na usimamizi wa sheria na kwamba jambo muhimu ni kuwa na Serikali itakayosimamia na kutekeleza sheria ili kulinda yale yaliyoelekezwa katika Katiba kujikuta wakimweka madarakani kiongozi anayejihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

“Hivi kama mtu anaweza kuhonga sehemu kubwa ya wapigakura katika jimbo la uchaguzi au hata katika nchi kama nafasi anayosaka ni urais; tumeshajiuliza hizo fedha nyingi hivyo anapata wapi? Kama anajihusisha na biashara hizo chafu akipata nafasi hiyo watoto wetu watapona?” alisema Sumaye jana na kuongeza:

“Haya ni maswali muhimu ya kujiuliza tunapoelekea mwaka kesho kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu.”

Alisema hayo mjini Morogoro kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata).

Akizungumza kwa tahadhari alisema haizungumzii Serikali yake iliyoko madarakani wala mtu yeyote, bali tabia mbaya, Sumaye alisema biashara ya dawa za kulevya inahusisha fedha nyingi na mitandao mipana ambayo isipodhibitiwa inaweza kulitumbukiza taifa katika janga.

Alisema Katiba Mpya siyo mwarobaini wa matatizo yanayolikabili taifa bali, utekelezaji na usimamizi wa sheria na kwamba jambo muhimu ni kuwa na Serikali itakayosimamia na kutekeleza sheria ili kulinda yale yaliyoelekezwa katika Katiba.

“Katiba haiwezi kumzuia mwizi kwenda kuiba na sheria haitamzuia mwizi kwenda kuiba ila itatamka adhabu ya kupewa huyo mwizi. Kwa hiyo ili vyote hivi viwe na maana ni lazima awepo mtu au chombo cha kumkamata huyo mwizi na kumfikisha katika mikono ya sheria na chombo hicho ni Serikali. Kama haiwezi kufanya hiyo kazi kwa ukamilifu tutaishia kulalamika tu na maonevu na maumivu yataendelea kuumiza jamii.”

“Kwa hiyo hata Katiba iwe nzuri namna gani na ikatamka kuwa rushwa ni adui wa haki na hata ikatoa adhabu kali sana kwa kosa hilo; kama tutaweka viongozi madarakani kwa rushwa, hiyo Katiba wala haitatusaidia. Hivyo Katiba nzuri mpya lazima iambatane na Serikali safi yenye kusimamia masilahi ya umma. Huwezi kumweka madarakani mwenyekiti wa kijiji au diwani au mbunge au hata Rais kwa rushwa ya kuwanunua wapigakura halafu utegemee Katiba Mpya itajibu matatizo ya jamii.”

Azungumzia Mviwata

Sumaye alisema Mtandao huo wa Wakulima Wadogo Tanzania ndiyo unaojua tatizo la kilimo na shida zao na ndiyo unaotakiwa kuulizwa cha kufanya ili kilimo chetu kibadilike na mkulima afaidike...

“Kama hatuwahusishi na kuwashirikisha katika sera, mipango na programu za kilimo, basi tujue kuwa sera, mipango na programu hizo zitashindwa.”

Alisema Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wengi wanategemea kilimo kwa maisha yao na uchumi wa taifa pia kwa kiasi kikubwa hutegemea sekta hiyo, lakini bado ni duni na hakijamkomboa mkulima mwenyewe wala uchumi wa taifa... “Nchi na watu wake bado ni maskini pamoja na kuwa watu wachapakazi wapo na ardhi kubwa na nzuri yenye rutuba ipo.”
 
KWA UFUPI

Alisema Katiba Mpya siyo mwarobaini wa matatizo yanayolikabili taifa bali, utekelezaji na usimamizi wa sheria na kwamba jambo muhimu ni kuwa na Serikali itakayosimamia na kutekeleza sheria ili kulinda yale yaliyoelekezwa katika Katiba.

Chukua jembe ukalime........
 
Kwani EL anauza na powder pia?basi kama ni hvyo huyu mzee ni mafia la ukweli ndo mana milioni 900 sio kitu kwake na ni wa kuogopwa zaidi ya Tsunami nashangaa akina Mwigulu Wanajitoa akili kumtetea kwa manufaa yao ya tumbo lao!!Lakini msihofu kuna mtabiri ninaye anasema huyu mzee hafiki 2015

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
I have to agree with Sumaye, in fact anarejea yaleyale alosema mwalimu miongo kadhaa ilopita/
 
Sumaye alishindwa kazi akiwa waziri mkuu..leo anautafuta Urais?
 
Back
Top Bottom