Sumaye-Serikali imechangia kidato cha nne kufeli!

Sumaye-Serikali imechangia kidato cha nne kufeli!

Frank Sojo

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Posts
343
Reaction score
97
Wakati tume maalumu ya kuchunguza kiini cha matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka huu bado inaendelea na kazi hiyo,Wazir mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema matokeo hayo mabaya kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na serikali yenyewe....

Sumaye ametaja sababu kuu nne kuwa ni moja,mfumo wa upanuzi wa Elimu ya sekondari uliofanywa na serikali bila maandalizi ya kutosha,

Pili,kutozingatiwa kwa dira ya taifa ya maendeleo 2025,

Tatu,Ni serikali kushughulikia matatizo ya jumla ya watumishi wa umma kwa kisekta!

Nne,Ni serikali kushughulikia mgomo wa walimu kimakosa,

Kuhusu upanuzi wa elimu sumaye anasema,"Tatizo hili la kufeli linaweza kuwa limesababishwa na mfumo wetu ma upanuzi wa elimu ya sekondari,kuna dalili kuwa tumepanua mfumo wetu wa elimu bila maandalizi muhimu ya walimu,vifaa vya kufundishia,vitabu na hata majengo yanayokidhi haja,hali hii lazima itatoa elimu duni".

Source:Raia Mwema.

My Take:

Mfumo huu mbovu umeanza wakati gani? Je si wakati wa serikali ya awamu ya Tatu kwa kuua michepuo? Je wakati huo Sumaye akiwa Waziri mkuu hakuyaona haya?

Tutafakari!
 
Hawa viongozi wanatufanya sisi wajinga.Mtu akishastaafu basi anataka kuonekana mzalendo!Hivi Sumaye anafikiri tumesahau jinsi serikali ya awamu ya tatu ilivyoshughulikia kibabe mgomo wa madakatari wakati ule akiwa wazir mkuu!

Kweli nyani haoni kundule!
 
Sumaye bana!!! Arrrh! yeye si ndo alikuwa bosi wake na Mungai?!!! Destructions alizotengeneza Mungai hakuziona!! Aache zake bana, wakome Dr. Kawambwa na Mulugo wale bata bana...
 
Sumaye aeleze walichofanya kwenye Elimu kabla ya kukosoa walichofanya wenzie, ndo mana Ndugai alimwambia kama ana uchungu na nchi basi arudishe marupurupu apewayo kama PM maana ni makubwa kuliko ya Naibu spika!
 
Anatafuta urais kwa hali na mali ......power monger
 
Msikurupuke katika kujibu bila hoja za msingi nyinyi,kwa tatzo la mishahara ya watumishi hususani hao walimu iliboreshwa na SUMAYE akiwa na MKAPA ikumbukwe kuwa Mh.Mwinyi aliacha watumishi hususani hao waliosahaulika(walimu) wakiwa wanakimbia fani na waliona bora wafanye kazi za uvuvi kuliko ualimu na wengine walijiingza ktk biashara,hapo ikumbukwe kuwa serikali haikuwa na pesa kwani pesa zilisambaa kwa raia hasaa wafanyabiashara.BIG UP SANA SUMAYE NA MKAPA, NA JK.
 
Nilifikiri una hoja kumbe ushabiki!!
 
mkuu Tatizo siyo maneno aliyoyatamka yanaweza kuwa na ukweli kabisa Tatizo ni msemaji/ au mtoa neno kwa maana he is a part of the problem.
 
Ukiwa nje ya uwanja unauona mchezo vizuri kuliko ukiwa ndani mkuu
 
Mbona wadau wengi mnamponda sumaye, sumaye alifanya vizuri kwenye uwaziri wake ndio maana kipindi chake wanafunzi hawakufeli kidato cha nne na licha ya hivyo matunda ya sumaye yalidumu mpaka utawala wa lowassa kama waziri mkuu. Je mliyatazama hayo?
 
I have to declare my interest,si shabiki wa chama cha siasa/mwanasiasa. Ili tupate matunda ya this "topic" ni vyema tujikite kujadili hoja na siyo kumjadili "sumaye". Je,ni kweli matokeo mabaya yamechangiwa na hizo sababu alizozitaja? Hapo tutao maoni yenye mtazamo wa kupata suluhu ya janga la elimu. Ila nimkumbushe Sumaye,wakati tulio nao sasa,hali ilivyo sasa,sidhani kama ni muafaka kujadili sababu za kuporomoka kwa elimu na kutoweka kwa mapana suluhisho. Tumekua tukiimba wimbo wa "sababu" za kufeli,ila kiitikio cha "utekelezaji wa maazimio" kimekua na sauti ya "ku-kwama kwama". "KAMA HATUONI UMUHIMU WA ELIMU,NI WAZI TUMEKUBALI UMUHIMU WA UJINGA". Sent via mng'olewa kucha na meno bila ganzi.
 
Msikurupuke katika kujibu bila hoja za msingi nyinyi,kwa tatzo la mishahara ya watumishi hususani hao walimu iliboreshwa na SUMAYE akiwa na MKAPA ikumbukwe kuwa Mh.Mwinyi aliacha watumishi hususani hao waliosahaulika(walimu) wakiwa wanakimbia fani na waliona bora wafanye kazi za uvuvi kuliko ualimu na wengine walijiingza ktk biashara,hapo ikumbukwe kuwa serikali haikuwa na pesa kwani pesa zilisambaa kwa raia hasaa wafanyabiashara.BIG UP SANA SUMAYE NA MKAPA, NA JK.
Hoja yako ina ukweli! Lakini hapo kwa JK Mmmmh! Kama mgonjwa alikuwa mahututi basi JK ndio kamuua kabisa huyo mgonjwa! Mgonjwa alikuwa analalamika yuko hoi,JK akasema utarudi kutibiwa ukiwa na bandeji usoni!
 
Wasimamiaji wa elimu wenyewe walioteuliwa ndio akina Mulugo unategemea nini? Mtu kafoji vyeti(majina) toka shule ya msingi mpaka chuo kikuu, leo anapewa dhamana ya kusimamia elimu,Sidhani kama watu watafaulu hapo!
 
Back
Top Bottom