Sumaye Kung'oka CCM leo?

Status
Not open for further replies.
Kukutana na waandishi wa habari leo saa 5.00 asubuhi katika hotel ya courtyard Hotel jijini dar es salaam


Source: Tanzania daima

Sidhani kama anataka kung'oka ssm bali anataka kutoa msimamo wake kuhusu uvccm.
 
itakua neema kwa chama pekee cha upinzani CDM, lkn kwa mtazamo wangu si rahisi kwa mtu kama uyu kukimbia ccm kwani watamfilisi kila kitu alicho vuna CCM:juggle:
 
Kweli funika kombe mwana haramu apite
Sumaye aligubikwa na skendo nyingi mpaka akaamua kwenda masomoni marekani alikaa kimya watu tumesahau maovu yake leo anaonekana mwema.

Uliza alivyomfanya kitu mbaya Mzee Jackson Makwetta moja ya wazee safi na wahafidhina wa CCM, kisa alimuendesha alipokuwa naibu waziri wa Kilimo enzi hizo.

Hivi story ya shamba la kibaigwa iliishia wapi.
Na yale mabilioni aliyosadikiwa kaiibia serikali.

Yasemekana alikuwa waziri mkuu wa kwanza aliyepewa nafasi hiyo kwa fadhila nayo ni kumrudisha BMW nyumbani enzi hizo akikaa peke yake akiwa waziri huku akiwa chakari kule upanga wakiwa wamekunywa kijiweni palm beach.

Siyo siri BMW alikuwa anakunywa mpaka anajikolea na Sumaye alikuwa anamsaidia kumrudisha home na asubuhi anapita kumchecki kama kaamka na ndio siri ya Sumaye kuwa waziri mkuu wa kwanza aliyekaa muda mrefu.

Ingawa nafurahia anavyowachana UVCCM.
 
Nisilolifahamu hadi sasa ni nani atakuwa Rais wetu mwaka 2015. Ninalolifahamu ni FT Sumaye, EN Lowassa hawawezi kuwa marais nchi hii.
 
tegeme lolote kutoka kwa huyu jamaa anaeitwa jina la utani kama ile katuni ya bwana Z..o.
 
MHHH??SIDHANI KAMA SUMAYE ANATAKA URAISI ILA NAFIKIRI NI MMOJA YA WATU MAKINI WALIOBAKI CCM AKITANGAZA KUONDOKA NITAFURAHI SANA
aje CDM ananafasi na bado ana nguvu

Du! Mtu makini? Aisee kweli Watz tunausahau mambo mapema. Si huyu PM ambaye mlitaka aondoke kipindi kile hata kabla ya kumaliza muda wake? Si huyu aliye jimilikisha mashamba ya wananchi kule Kibaigwa na Kilosa? By the way, mtu makini! unamaanisha nini?
 
hasa huu mradi wake wa Loliondo unamjenga sana kisiasa. Ndo maana Mtanzania na magazeti mengine uchwara hayaishi kuhubiri ya Loliondo. Wenye akili, macho na masikio tunafuatilia kwa makini, tunaona na kusikia vema.

tunasubiri tu siku ya loliondo yatakapoanza kutumika kama turufu ya kisiasa. time will always tell
Sumaye hawezi kuondoka ccm watamuweka kweli listi ya kushughulikiwa na al shabab
 
Tuwe makini hawa wanajuana wanajifanya kuwa na ligi kati yao ili kutufumba macho, sumaye nae sumu tu, mangapi katuingiza mkenge na kutuona sisi makenge?
 
sumaye nae mchafu tu,mi simuoni msafi hapo,acheni kumpigia chapuo!kwani wakulima wa mvomero waliporwa mashamba na nan?

Sisiem kila mtu anatakataka zake, lakini wanatofautianatofautiana, Mfano Huyu JAKAYA Sielewi anawezaje kutengwa na IPTL ma DOWANS?
Ila mpaka sasa najaribu kumtafakari Sumaye, naona Angalau chembe chembe ndogondogo za Uzalendo wa kweli, Halafu lazima mkumbuke kuwa huyu Jamaa amechafuliwa sana, tena sana, Na kikubwa Hawezi kujitenga na Madudu ya DENJAMAN MKAA- HAPA.
 
Watu wakini?
Hivi sio huyu nilisikia enzi hizo alivo maliza mda wake kuwa ana trilion11 ambazo haijulikani zilipo?
Leo msafi au kwa kuwa alikaa kimya mda mrefu?

Ngoja arudi tena,niliambiwa hata kama huwajui wazazi wako ingia kwenye siasa,watu wanajua kila kitu kuhusu wewe na utakisikia!!!!

Wewe badili jina, huwezi kuitwa speaker halafu ukawa mjinga. propaganda against Sumaye unazimeza nzima nzima bila kuchambua. Waziri Mkuu wa Tanzania awe na trilioni 11/- kaziiba wapi kwenye nchi ambayo haina hizo hela? umesahau gazeti la Tanzania Leo lililoandika mhariri akiwa Muhingo Rweyemamu lilishindwa kesi na kumlipa sh milioni 100, kati yake alitoa 5,000,000 akawapa Jukwaa la wahariri 'ili zitumike kuelimisha waandishi wajua maadili ya kazi yao.
 
hawezi kung'oka ccm hata iweje....anaendeleza tu nipasho yao na uvccm
JK kageuza UVCCM mdomo wake mwingine wa kusemea wenzake, sasa Sumaye naona anataka kuwatolea uvivu UVCCM hivyo indirect atakuwa amemtolea uvivu JK! Usiniulize je hana nafasi ya kumshauri kama kiongozi mstaafu, jiulize kwa nini JK ageuze UVCCM mdomo wake mwingine wa kusemea?
 
Wewe badili jina, huwezi kuitwa speaker halafu ukawa mjinga. Apropaganda against Sumaye unazi,eza nzima nzima bila kuchambua. Waziri Mkuu wa Tanzania awe na trilioni 11/- kaziiba wapia kwenye nchi ambayo haina hizo hela? umesahabu gazeti lililoandika mhariri akiwa Muhingo Rweyemamu lilishindwa kesi na kumlipa sh milioni 100, kati yake alitoa 5,000,000 akawapa Jukwaa la wahariri 'ili zitumike kuelimisha waandishi wajua maadili ya kazi yao.
Rula kama hizi ndiyo tunazohitaji, ukiwa mwana JF ni lazima ujifunze kuwa na kumbu kumbu za matukio mengi ili usije shusha heshima yako bureee.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom