Sumaye avuna wanachama wapya 50 Ukonga

View attachment 568104

View attachment 568105

Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani Kamanda Fredrick Tluway Sumaye leo amekabidhi kadi na kuwapokea wanachama wapya 51 katika Jimbo la Ukonga. Tukio hilo limefanyika leo Jumatano tarehe 15/08/2017 wakati wa Ziara ya Kamati Tendaji Kanda Jimboni hapo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kurudisha kadi za CCM na kukabidhiwa za CHADEMA, aliyekuwa kada maarufu na Mwenyekiti wa Serikali ya kwa awamu tatu Bi. Joyce Temu amesema ameamua kujiunga na CHADEMA baada ya kukerwa na mwenendo wa Serikali ya awamu ya tano ambayo ni matokeo CCM kupoteza Dira. Katika hatua nyingine kamanda Sumaye amemkabidhi kadi ya CHADEMA wakiliMsomi Amani Taslima, Mtoto wa Mbunge Mstaafu wa Afrika Mashariki.

Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza kweli
Safi sana kamanda wa kweli!
 
HIVI UKONGA NI JIMBO LA CHAMA GANI?....EBU ACHENI KUJITEKENYA....afu mbna hamn picha wakirudisha kadi za CCM?....yaani wacheza singeli wa chama cheni ndio mnawaita CCM?....ONA IBU WASI

Kwani Rais wa nchi ni wa Chama gani?, yaani kama Jimbo linaongozwa na Chadema ndio hakuna wanaCCM, au tukisema nchi inaongozwa na Rais wa CCM basi nchi haina mfuasi wa vyama vingine?
 
HIVI UKONGA NI JIMBO LA CHAMA GANI?....EBU ACHENI KUJITEKENYA....afu mbna hamn picha wakirudisha kadi za CCM?....yaani wacheza singeli wa chama cheni ndio mnawaita CCM?....ONA IBU WASI
Hivi Mwita Waitara ni mbunge wa jimbo gani na ni mwanachama wa chama gani?
 
Kwenye headlines zetu tena nafikiri ndio mgombea wetu wa urais mtarajiwa 2020,ccm imepoteza dira hapo umedanganya nafikiri sisi chama cha wajikongoja ndio tupo hoi!
 
Akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kurudisha kadi za CCM na kukabidhiwa za CHADEMA, aliyekuwa kada maarufu na Mwenyekiti wa Serikali ya kwa awamu tatu Bi. Joyce Temu amesema ameamua kujiunga na CHADEMA baada ya kukerwa na mwenendo wa Serikali ya awamu ya tano ambayo ni matokeo CCM kupoteza Dira.

Huyo anayeponda ni TEMU wa kilimanjaro kaenda kujiunga na wa kilimanjaro wenzie CHADEMA .Alikuwa pandikizi la chadema ndani ya CCM
 
Huyo anayeponda ni TEMU wa kilimanjaro kaenda kujiunga na wa kilimanjaro wenzie CHADEMA .Alikuwa pandikizi la chadema ndani ya CCM
Acheni ujinga bhana kwahyo wale waliohama ccm na kuhamia chadema huko mara jana nao ni wachagga??? grow up acheni utoto chadema mbona ilipata kura nyingi mikoani kuliko hta kaskazini kwenyewe??? Ukabila hauwasaidii lolote
 
Hizo ni zitakazoharibika! Chadema watapata za wanachama wao tu kama laki 5 hivi!
Sasa kumbe mnajua mtashinda ssa kwanni mnazuia mikutano na mnaogopa tume huru!!! Ssa mnaonaje mlete tume huru na mruhusu mikutano maadam ssa mmeshajua tutaambulia 15% pekee
 
Kata MTI panda MITI

Back
Top Bottom